HAKUNA aya hata moja ya Biblia inayomtaja mtu yeyote aliyeona sura ya Yesu hasa wakati akifa pale msalabani. Yesu alidhaniwa tu kuwa ni Yesu aliyeuawa msalabani, lakini baada ya siku chache Yesu huyo akaonekana yu hai, wala hakurudi kama pepo (ghost)! Kung'ang'ania kuwa ni Yesu aliyeuawa pale msalabani ni utani mgonjwa, hususan tukizingatia ushahidi wote huo hapo nyuma, vipofu na hata kuwafufua watu. Kwa upande mwingine twaambiwa eti kumtesa Yesu kwa kumpiga, kumchoma kwa ncha kali, na kumpigilia misumari mtini eti ilitosha kumuuwa Yesu. Hii haiingii akilini kimantiki labda kwa kuiamini tu kiupofu (blindly).
Isitoshe, Yesu angalisubuliwa kweli, ingekuweko aina moja tu ya msalaba aliouliwa. Lakini Catholic Encyclopaedia peke yake ina aina 40 za misalaba.
Kwa sababu zisizo dhahiri, msalaba ule wa vipande viwili vinavyosigana yaani +, ndio umependelewa zaidi na Waingereza wakauita "Cross", ingawa neno la awali la msabala kwa Kigiriki ni "Stauros" ambalo halina dhana ya vipande viwili ila kimoja tu. Biblia chche tu kama ile ya Mashahidi wa Yehova ndio imetaja waziwazi kuwa Yesu aliangikwa kwenye mti (stauros) na usulubisho kwao wao sio "cricifixion" bali "stafixion". Dhehebu jingine limesema Yesu aliangikwa kwenye mti wenye umbo la T. Ke bado Wakristo wengine wanauabudu msalaba huo wa alama ya kujumlisha +.
Gazeti la Newsweek la Aprili 4, 1994 liandika: "Kifo cha Yesu - Fikra mpya za siku zake za mwisho". Limesema kuwa, kama Yesu kweli aliuliwa msalabani, basi lazima iweko aina moja tu ya msalaba. Katika gazeti hilo hilo, Padri wa Kikatoliki Raymond Brown kaandika kitabu chake, "The Death of the Messiah (Kifo cha Masihi)". Doubleday na wanaseminari wenziwe 2000 amesema kuwa hadithi za Yesu kuhusu kuhubiri, kuponya wagonjwa, kufanya miujiza, hizo zaweza kuwa kweli; lakini hadithi nyingine (kama ya kusulubiwa Yesu) hazina usahihi wa kihistoria (historical accuracy). Hii anasema ni kwa sababu waandishi wote wa Injili hawakuwa mashahidi wa macho (eye witnesses) kushuhudia hata moja ya yale wayoyaandika mnamo miaka 35-70 baada ya Kristo; na mpaka leo hatuna hakika ni nani hasa aliyeandika Injili zote hizo, ambazo kila inatofuatiana na yenzie.
Yesu asingekosa kutabiri kuuliwa kwake msalabani, akatabiri juu ya kuteswa tu:
"Mt 23:35 Hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habil, yule mwenye hakika hata ... Zakaria ... mliyemuua kati ya patakatifu".
"Lk 22:15 ... Nimetamani sana kula pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa"
Yesu asingekosa kutabiri kuuliwa kwake msalabani, atabiri kuteswa tu
"Mt 23:35 Hivyo ni ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habil, yule mwenye haki, hata... Zekaria... mliyemuua kati ya patakatifu..."
"Mt 17:12 .. Vivyo hivyo mwana wa Adamu naye yuenda kutesa kwao". "Lk 22: 15... Nimetamani sana kula pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu". Hata baada ya huko "kusulubiwa" kwake, Yesu alitaja kuteswa kwake tu:
"Lk 24:25... Enyi msiofahamu... 26: Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya ni kuingia katika utukufu wake?"
Jamani, na tujihadhari sana na utatanishi wa lugha ya Biblia. Hata aya anazosemewa Yesu kuwa kauawa huenda zimetiwa chumbi, kama Paulo alivyotia chumbi usemi wake wa mtu kufa (kwa maana ya kuteswa) kila leo, kama Biblia inavyoumbua:
"1Kor 15:31 ... Kwa huku kujisifu kwangu niliko nako juu yenu katika Kristo Bwana wetu, nimekufa kila siku".
Kwa hiyo kama kulikuwepo mpango wa kumuuwa Yesu, basi hakuujua na Mungu, akina Plato na kadhalika waliunda njama za kumuokoa na kifo cha laana cha msalabani, na ni dhahiri kabisa kwamba Yesu hakufa wala hakusulubiwa.
Taarifa za kusulubiwa Yesu katika Injili zote nne sio kweli kwa sababu zifuatazo:
Taarifa za Injili zinatafautiana mno, kama mifano michache hapa chini ionyeshayo:
Injili tatu zinasema Simoni ndiye aliyechukua msalaba wa Yesu (Mt 27:32; Mk 15:21-2; Lk 23:26); lakini Injili ya nne inasema Yesu aliubeba msalaba wake mwenyewe (Yn 19:17).
Mathayo yasema Yesu alipewa divai iliyochanganywa na nyongo akaionja na hakuinywa, Marko anasema Yesu hakuinywa, na Luka na Yohana wala hawalitaji tukio hilo.
Kuhusu saa aliposulubiwa Yesu, Mathao na Luka haiwaitaji kabisa, lakini Marko anasema ilikuwa ni saa tatu (Mk 15:25) na Yohana asema saa sita (Yn 19:14). Mathayo na asema ilipasuka kutoka juu hadi chini; na Luka sema ilipasuka kutoka upande hadi upande (horizontally), na ni Mathayo peke yake aliyearifu kuhusu matetemeko, kufunuka makaburi na miili kuinuka, miamba kupasuka.
Mathayo, Marko na Luka wanasema wanawake walisimama mbali na msalaba (Mt 27:55-6; Mk 15:40-1; Lk 23:49), lakini Yohana anasema walisimama jirani na msalaba (Yn 19:25). Yohana peke yake ndiye karipoti kuwa mamake Yesu naye alikuja kule msalabani. Pia Injili zatofautiana juu ya idadi ya wanawake hao.
Kuhusu giza, Mathayo, Marko na Luka wanasema lilitanda dunia nzima, lakini Yohana hataji kabisa na kadhalika.
Mifano iko zaidi ya 20 mingine, yote hii inazipinga aya ambazo hunukuu akina Batendi na kudai kuwa zinasema Yesu aliuliwa pale msalabani. Qur'an inasema akina Batendi hawana hakika, bali wanadhani tu. Maneno haya ya kupingana namna hii kweli yote ni ya Mungu au ya waandishi wapotofu?
Kuhusu itikadi ya "Dhambi ya asili (Original Sin) na Upatanishi (Atonement):
Hii nayo sio kweli, wala haingii akilini. Akili timamu inakataa kabisa nadharia hii ya Dhambi ya Asili na Kafara. Kusema eti dhambi walioitenda wazazi wetu Adam (a.s.) na Hawa (r.a.) maelfu ya miaka iliyopita - dhambi hiyo imerithishwa kwa kila mwanadamu hadi siku ya mwisho, kunapinga aya nyingi za Biblia na Qur'an zifuatazo:
"Kum 24:16 Mababa wasiuawe kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasiuawe kwa ajili ya baba zao; kila mtu auawe kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe".
Aya ya 2 Fal 14:6, na 2 Nya 25:4 zasema vivyo hivyo pia.
"Yer 31:30 Bali kila mtu atakufa kwa sababu ya uovu wake mwenyewe..."
"Eze 18:20 Roho itendayo dhambi ndio itakayokufa, mwana hatachukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanae, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na haki yake mwenye uovu itakuwa juu yake".
Hata Yesu mwenyewe kaipinga hii nadharia ya "Dhambi ya Asili" kwa kusema kuwa watoto wadogo hawana dhambi (Mt 18:2-4, 19:14; Mt 18:2)
Qur'an nayo imesisitiza kuwa kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe:
"17:15 Anayeongoka, basi anaongoka kwa maslahi ya nafsi yake mwenyewe, na anayepotea basi anapotea kwa hasara ya nafsi yake mwenyewe. Wala hatabeba mbebaji mzigo wa mwingine...".
"53:36 Au hakuambiwa yaliyomo katika vitabu vya Mussa? 37: na vya Ibrahimu aliyetimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu? 38: Ya kwamba haichukui nafsi yeyote dhambi ya nafsi nyingine? 39: Na kwamba mtu hatapata ila yale aliyoyafanya 40: Na kwamba amali itaonekana. 41: Kisha atalipwa malipo yaliyo kamili..."
Ukifika hapa, yanazuka masuali mengine mengi tata kwamba: Je, Mariamu, mama wa Yesu naye anayo dhambi ya kurithi au hana? Iwapo Mariamu anayo dhambi ya urithi kutoka kwa Adamu na Hawa, Yesu naye ameirithi hiyo dhambi kutoka kwa mzazi wake pekee Mariamu?
Hii ndio itikadi ya Dhambi ya Asili aliyoizusha Mt. Paulo ili apate kuhalalisha itikadi yake nyingine ya Fidia (Kafara, sadaka Cacrifice, Atonement) kwa njia pekee ya kufa Yesu msalabani (Rum 5:12-15, 1 Kor 15:22).
|
|