WAISLAMU mbalimbali wamelaani vikali kitendo cha serikali kumkamata Amir wa Waislamu Sheikh Juma Mbukuzi na kusema kuwa ni kitendo asichostahiki kufanyiwa kiongozi yeyote wa dini.
Wakiongea na gazeti hili kwa nyakati tofauti walisema kuwa anayekamatwa usiku anakuwa ni mhaini au muuaji inakuwaje Sheikh "avamiwe" usiku wa manane kama mhaini".
Chifu Yusufu Masanja akizungumza kwa uchungu aliItahadharisha serikali ikae ikijua kuwa dhulma daima haidumu. Aidha, amesema kuwa wanaonyanyaswa na kuteswa leo wana watoto na wajukuu na bado wanaendelea kuzaliana na kwamba "vizazi hivi siku moja vitakaporejea historia ya baba na babu zao walivyoteswa moto utakaowaka hakuna atakayeweza kuuzima".
Aidha, Chifu Yusufu Masanja ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mabadiliko ya Katiba nchini amesema kuwa hakuna raia yeyote mwenye akili timamu anayeweza kuunga mkono na kufurahia vitendo vya unyanyasaji na mateso yanayofanywa na serikali ya CCM kinyume na sheria dhidi ya Waislamu.
Alisema serikali haikuwa na haki yoyote ya kimsingi kufanya kile alichokiita "ufedhuli" dhidi ya watu wasiokuwa na hatia kwa kuwa maandamano ni jambo halali kwa raia huru katika nchi zenye kufuata demokrasia ya kweli huachiwa waandamane kudai haki zao za kimsingi Kikatiba.
Alisema Waislamu bado wana haki kikatiba kuandamana kwa kuwa kimsingi madai yao ni ya kikatiba.
Lakusitisha alisema Waislamu wanaodaiwa kuandamana wamepigwa, kujeruhiwa na kukamatwa wakiwa Msikitini!
"Ninalaani wote wanaounga mkono vitendo vya kidhalimu vinavyofanywa na serikali dhidi ya raia wasiokuwa na hatia ... Ninaitaka serikali iache mara moja ufedhuli wa kutesa na kuwakamata watu ambao hawajatenda kosa, wanaopinga dhulma na kudai haki zao za kikatiba", alisema Chifu Masanja kwa uchungu.
Naye Bob Makani akiongea
na gazete hili alisema kuwa polisi hawakutenda haki kuwaweka ndani Waislamu.
Alisema si haki kwa sababu kitendo cha kuandamana hakijavunja sheria yoyote.
--
|
|