WAKATI Waislamu sehemu mbalimbali nchini wakitaharuki kwa hasira viongozi wa Msikiti wa Manyema wamesema kuwa hawako pamoja nao kupinga kauli za Wabunge zinazokemea utekelezaji wa maamrisho ya Uislamu kwa wanafunzi Waislamu na hawataki kuhusishwa na lolote linalofanywa na Kamati inayoitwa Shuura ya Maimamu.
Aidha, uongozi huo umekiri kuwa ukiwatoa Waislamu wanawake waliokuwa Msikitini hapo kwa polisi.
Akinukuliwa na gazeti la Majira la Juni Jumatano Bw. Said Hilal msemaji wa Msikiti huo amesema kuwa waliwaruhusu polisi waingie Msikitini kuwachukua wanawake.
Wakizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Msikiti huo Jumanne Agosti 3, mwaka huu viongozi wa Kamati ya Utendaji ya Msikiti wa Manyema walisema Manyema haina Uislamu wa fujo wala vurugu na wanapenda amani.
Msemaji wa Msikiti huo Bwana Said Hilal alisema Msikiti wa Manyema hautaki kuhusishwa kwa vyovyote na maandamano ya Julai 30, kwani uongozi wa Msikiti huo hawayajui, hawayatambui na wala hawayaungi mkono.
Alisema viongozi wa Msikiti wa Manyema hawakushiriki katika maandamano hayo na wala maandamano hayakuanzia wala kuishia katika Msikiti huo.
Bwana Hilal alisema lililotokea ni vijana aliowaita wahuni ambao alidai waliokuwa wakitumia lugha chafu walifika Msikitini hapo na kuingia ndani ndipo kiongozi mmoja wa Kamti ya Utendaji wa Msikiti wa Manyema alipopiga simu kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dar es Salaam kumuarifu kuwa waandamanaji wamevamia Msikiti wa Manyema.
Bw. Hilal alisema kuwa taarifa alizonazo waandamanaji hao walisema waliambiwa na viongozi wao waende Msikiti wa Manyema ili wakapange cha kufanya baada ya maandamano yao kuvurugika.
Alisema madai ya kuwa polisi waliwatoa Waislamu ndani ya Msikiti si ya kweli kwani Waislamu hao walitolewa katika jengo la Msikiti huo na viongozi wa Msikiti na waliwakabidhi polisi.
Walipoulizwa kufanya hivyo si kuwasaliti Waislamu wenzao, walijibu kuwa wako radhi waambiwe hayo kuliko kuchafua jina zuri la Msikiti wa Manyema.
Vile vile Bwana Hilal alizihusisha fujo hizo na kikundi cha Ansar Sunnah ambao alidai kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakifanya chokochoko dhidi ya Msikiti wa Manyema ili waweze kuuteka kama walivyoiteka Misikiti mingine jijini.
Alisema gazeti hilo kwa muda mrefu lilikuwa likimsakama Imam wa Msikiti huo Sheikh Hamid Jongo kwa madai kuwa hana msimamo wakati msimamo wanaoutaka wao ni kueneza itikadi ambazo Jamaat Ansar ndizo wanazoziona za sawa.
Walipoulizwa je hawaoni kuwa
madai ya Waislamu ni ya haki na kwa wao kuwakana wenzao ni sawa na kukana
wanawake kuvaa hijab na wanafunzi kuruhusiwa kwenda kusali sala za Ijumaa.
--
|
|