KWA karne kadhaa sasa
kumekuwa na mitazamo potofu katika kuingalia dini. Mitazamo hiyo imezaa
maandiko, hotuba na utekelezaji wa mambo yanayoitwa ya kidini kinyume na
uhalisia wa suala lenyewe. Wanaojiita waumini wa dini leo hii wanaogelea
katika dimbwi hili upotofu kwa staili ya aina yake. Mtazamo huu wa dini
umewafanya wayagawe maisha yao katika kambi mbili zisizo na uhusiano. Vitendo
vya dini kwao(Ibada) vimekuwa kama tambiko(taboo) la kuosha dhambi na kupata
thawabu bila kuathiri au kuhusisha matendo hayo na maisha ya kila siku.
Kwa Waislamu wenye mtazamo huu, dini kwao ni kule kuingia msikitini na
kufanya ibada ya swala, vile vile kufunga na kwenda kuhiji kwa mwenye uwezo.
Mambo ya ziada ni mihadhara ya kulingania, sherehe za Idd na Maulid, ndoa,
na kilele cha yote mtu kupata bahati ya kuzaliwa na wazazi Waislamu au
kuwa na "jina la kiislamu" hatimaye umauti unapomfika kuzikwa kiislamu.
Hawa huwaona wale wote wanaojaribu kuieleza na kuitekeleza dini kwa kuihusisha
na maisha ya kila siku kuwa ni watu hatari, wanaoharibu dini kwa kuichanganya
na siasa na wasioitakia mema jamii iliyowazunguka kwa kutaka kufanya jambo
linaloweza kuvuruga amani na utulivu wa nchi. Kwa Wakristo dini kwao ni
kule kuhudhuria misa kanisani siku ya jumapili na kuimba nyimbo za kumsifu
Yesu Kristo, baadhi yao wameamua kuwa watawa yaani kujitenga kabisa na
maisha ya kila siku ili kumtumikia bwana Mungu, wengine wamekwenda mbele
kujiita walokole! Endelea...
Wale wakanao kuwa na dini wameondokea kujiepusha na yale matendo ya kiroho, wanachokijua wao ni kuushughulisha mwili kwa ajili ya lishe, mavazi, makazi, jimai huria na starehe kulingana na kiwango cha teknolojia iliyofikiwa.
Mafundisho haya yanakusudia kuonesha namna ilivyochipua mizizi ya mkanganyiko huu na jinsi ulivyoathiri maisha ya wanaadamu kwa ujumla. Tutaangalia kwanza kanisa lilivyoshiriki kukandamiza watu kule ulaya mpaka kuibuka harakati dhidi yake, baadaye tutaangalia mgogoro ulioibuka ndani ya Uislamu wakati wa Khalifa Uthman ambao ulipelekea vita vya wenyewe kwa wenyewe wakati wa khalifa Ali ambavyo vilizaa mgawanyiko na kuibua Uislamu wa ukoo wa banu Umayya na banu Abbas na kisha kutokea hapo kuingia kwenye Ufalme(kingship) na kutenganisha dini na siasa kama inavyoonekana leo hii katika mataifa yanayoitwa ya kiislamu.
Kwa muda mrefu kumemekuwepo na mitazamo potofu katika kuiangalia dini na nafasi yake katika maisha ya mwanaadamu. Mtazamo huo umeathiri utendaji wa wale wanaoitwa wanadini na wanaokana kuwa na dini.
Wengi wameitazama kama ni imani juu ya kuwepo Mwenyezi Mungu. Katika makamusi ya lugha za kiingereza na kiswahili athari ya mtazamo huo inajitokeza, kamusi ya kiingereza inasema:
"Ni imani ya kuwepo nguvu kuu iliyo na uwezo juu ya kila kitu. Inayomiliki Ulimwengu, ambayo imempa binaadamu roho ambayo huendelea kuishi baada ya kifo cha mwili".
Nayo kamusi ya Kiswahili sanifu ina mtazamo huo huo:
"Imani inayohusiana na mambo ya kiroho baina ya binaadamu na Mwenyezi Mungu, au njia ya kuhusiana na Mwenyezi Mungu"
Kutokana na tafsiri hii ya "dini" baadhi ya watu wamedai kuwa hawana "dini" kwa kuwa hawana imani juu ya kuwepo Mwenyezi Mungu.
Kwa hivyo, wazo la kuwepo Mungu Muumba ambalo limezaa dini, limekuja baada ya mwanaadamu kushindwa kuzielewa na kuzikabili nguvu za mazingira zilizokuwa dhidi yake. Ili kujiliwaza katika hali hiyo ya kushindwa, ilibidi mwanaadamu ajiwe na fikra za uwepo Mwenyezi Mungu. Ni katika mtazamo huu walahidi hudai kuwa kuwepo kwa Mungu Muumba si jambo halisi bali ni dhana tu iliyoibuka katika fikra ya mwanaadamu baada ya kushindwa kutatua maatizo yake ya kiuchumi, kijamii nakadhalika. Katika kuliweka wazi jambo hili, F. Angels katika Anti-Duhring anazidi kusisitiza:
"Kwa ujumla dini zote si chochote ila ni matokeo ya fikra ya mwanaadamu juu ya nguvu za maumbile zinazomiliki maisha yake ya kila siku, mtazamo ambao huzipa nguvu za kawaida umbile la nguvu za kiungu".
Ni katika mtazamo huu, dini imedaiwa kuwa ni matokeo ya uduni wa maendeleo ya mwanadamu na kila anavyosonga mbele katika maendeleo ya Sayansi na teknologia ndivyo hoja ya dini inavyopungua. Kwa mtazamo wao wale waliopea katika maendeleo ya Sayansi na teknologia hawana hoja ya kuwa dini kabisa kama anavyodai Lenin katika kitabu chake Socialism and Religion:
"Kila mtu hanabudi kuwa huru kabisa kufuata dini yoyote anayoitaka au asiwe na dini kabisa, yaani awe kafiri jambo ambalo linambidi kila mjamaa awe hivyo........."
Dai hili kuwa dini inatumika kama chombo cha kuwanyonyea wanyonge, limetokana na dhuluma waliyofanyiwa watu katika jamii kwa kisingizio cha dini katika nyakati mbalimbali za historia ya mwanaadamu. Hebu turejee jamii chache tuone kina cha ukandamizaji huu uliofanywa kwa kutumia kisingizio cha dini. Ukirejea historia ya Ulaya Magharibi utalikuta Kanisa likipita hatua mbalimbali za matatizo na maendeleo ya utamaduni wa Kimagharibi hadi kufikia hatua ya leo, ambapo "dini na sayansi" vinaonekana ni vitu visivyoweza kukaa pamoja wala kuwafikiana kwa hali yoyote.
Wakati wa zama zinazoitwa za Giza (400-900 A.D.) Kanisa likiwa na nguvu za dola Ulaya lilishiriki moja kwa moja kuwanyonya na kuwakandamiza watu kwa njia mbalimbali. Ukristo ulifanywa dini rasmi ya utawala wa Kirumi (Roman Empire) baada ya Constantine kurithi kiti cha Kaizari mnamo mwaka 305 A.D. Kipindi hiki Ukristo ukiwa ni zao la mchanganyiko wa mafundisho ya Paulo na itikadi za kipagani (za mfalme wa Kirumi), ulikuwa na nguvu kubwa sana. Wakuu wa Makanisa pamoja na taasisi zake walijimilikisha ardhi kama ilivyokuwa chini ya mfumo wa ukabaila (wachache wahodhi ardhi na kuwatumia vibarua kwa ujira mdogo kuwazalishia au kuwakodisha ardhi hiyo kwa kulipa mazao, nguvu na fedha wakati wa baadaye). Kipindi hiki na kilichofuatia istilahi kama "tithe" zilianza kutumika zikimaanisha sehemu ya kumi ya mazao kwa ajili ya Kanisa au watumishi wake kutoka kwa waumini.
Waasisi na Wataalamu wa Kanisa walilazimika kukaa na kuandika nadharia ambazo zilichukuliwa kuwa ni sehemu ya mafunzo na sheria ya Kanisa Mt. Ambrose (340-397), Mt. Augustine (354-430) na Papa Gregory the great (540-604) walishikilia kuwa milki ya ya utawala wa kiroho na ule wa kupita (wa dunia) vyote vinatoka kwa Mungu. Papa Gelasius I (492-496) alipokuwa akifafanua nadharia ya panga mbili nguvu za kanisa na dola-alisema kuwa nguvu hizi zote ni muhimu kwani dola kuweka njia ya kwendea peponi kwa kuhakikisha usalama na kanuni wakati kanisa lina dhamana ya maendeleo ya kiroho (Kaizari mpe haki yake na Mungu mpe haki yake). Papa Gelasius I alitaka upanga wa kiroho uwe juu ya Papa asiwe na kumkalia juu.
Nadharia ya haki za kiungu kwa wafalme "divine right of Kings" iliasisiwa ili kuikanusha ile ya mgawanyo wa dola na kanisa. Kwa kuwa kipindi cha zama za kati (middle Ages) kilikuwa na mivutano ya utawala - na mfalme awe mwenye kuwajibika kwa watu wake au mwenye amri na nguvu za mwisho (absolute monarch). Akina Martin Luther (1483-1586) na John Calvin (1509-1564) ambao wanaitakidiwa kuwa wahuishaji wa kanisa (reformers) na waasisi wa madhehebu ya Kiprotestanti walianzisha nadharia zao za utii wa kibubusa (passive obedience).
Nadharia hizo zilitumika kuwanyonyea watu kwa jina la dini nchini Uingereza na Ufaransa hasa wakati wa utawala wa akina Stuart (Uingereza) na Louis XIV (Ufaransa). Hali hii ilikuwako Spain, Ureno, Italia na sehemu nyinginezo ambazo Kanisa lilishamiri.Kwa karne nyingi yaliendeshwa mauaji ya maelfu kwa mfano korti ya Papa (Inquisition) kwa kipindi cha miaka 1481 iliwaadhibu watu 340,000 ambao kati yao 32,000 walichomwa wakiwa hai wakiwemo wanasayansi Bruno na Galileo Galilei ambao nadharia zao za kisayansi kuhusu dunia zilipingana na mafundisho ya kanisa. Ni kutokana mauaji ya watu ndipo chuki dhidi ya dini ilipomea ambapo wanatafakuri waathirika waliiona kuwa ni kasumba na inapingana na sayansi. Wanafalsafa waliokuwa na fikra pana kuhusu makuzi ya ulimwengu(Cosmological evolution) kama Immanuel Kant(17755) waliyapinga wazi wazi mafumbo ya kibubusa ya kanisa. Kant alikuwa mufakir ambaye akili yake dadisi haikuweza kutoshelezwa mafumbo ya kiothodoxy ya kanisa, katika kitabu chake "Attempt to conceive and to explain the origin of the universe mechanically, according to the Newtonian Laws", alipinga vikali maelezo ya biblia kuhusu chanzo cha ulimwengu. Ni hali hiyo pia iliyochangia mapinduzi ya Ufaransa ya 1789 na kusababisha mali nyingi ya kanisa kutaifishwa na kuibuka nadharia za Secularism (kutenganishwa dini na dunia).
Harakati za kijamaa zililoasisiwa na wanachuoni wawili wa itikadi ya ujamaa Karl Marx na Frederick Angels nazo zilichochewa na upotofu huu wa dini zinazonasibishwa na Mungu ambazo zilimaliza mahusiano kati ya dini na maisha huko ulaya. Mwanachuoni F. Angels ameandika kwa jazba katika kitabu chake kuwa:
"Dini ni zao la ujima (uduni) unaotokana na kusinyaa kwa mawazo ya mwanaadamu........Baada ya kutambua kubakia mwanaadamu katika hali ya kiroho.....Wanaadamu katika kipindi cha ujima waliumba miungu. Mwanzoni miungu hawa waliwakilisha viumbe halisi vyenye uwezo mkubwa zaidi ya mwanaadamu, pole pole waliielekeza imani yao kwenye miungu ya kiroho iliyokuwa na roho bora kuliko zetu. Hivi ndivyo mwanaadamu baada ya kuumba miungu wengi kila mmoja na kazi yake, ilivyofikia fikra ya Mwenyezi Mungu" (Mungu mmoja).
Mwanachuoni mwingine wa itikadi hiyo aliandika kwamba:
"....Fikra ya kuwepo uwezo mkuu wa asili kwa ujumla haitokani na ushahidi wa milango ya fahamu... Lakini nini chanzo chake, ni namna gani fikra hii ilibuka kwa mara ya mwanzo? Na hatuwezi kukubali eti fikra hii ni zao la ufunuo au imetokana na Mungu Mumba kama dini zinavyotueleza. Fikra ya kuwepo Mungu Muumba au mawazo ya dini kwa ujumla chanzo chake ni ujinga na kukata tamaa kwa mwanaadamu katika kuyakabili mazingira yake".
Mawazo haya yalikuja kutafsiriwa kivitendo na Lenin wakati wa kile kilichojulikana kama mapinduzi makubwa ya ujamaa ya Urusi(The great Russian revolution) ya mwaka 1917. Rasmi yalianza kutekelezwa ilipofika mwaka 1924 baada ya kumalizika vita ya wenyewe. Lenin aliyaweka mbali mafundisho ya dini na utendaji wa shughuli za kila siku, baadaye dini ilipigwa marufuku, majengo ya ibada kugeuzwa kuwa majumba ya makumbusho, utamaduni na starehe.
Mabaki ya unyonyaji na ukandamizaji kwa kisingizio cha dini yangali yanaonekana mpaka zama hizi.
Kitabu kiitwacho Fisher; Behind the Lodge Door; Church, State anda Freemansory in America kinaeleza yale yanayoendelea katika kanisa katoliki. Kitabu hicho kimendika kwamba kanisa hilo limeweka mtandao wa kigaidi unaohakikisha wizi, mauaji na maovu mengine yanayofanywa na kanisa hilo yanadhibitiwa barabara yasijulikane na waumini wa kawaida wa kanisa hilo na wananchi kwa ujumla.
Ama wale wanaogundua au kutaka kufichua siri hiyo maisha yao huwa hatarini. Kwa mfano septemba 28,1978 Pope John Paul I(Albino Luciano) aliuawa baada ya kukalia kiti cha Upapa kwa siku 33 tu. Albiano alipoingia Vaticana aligundua kuwa Vatican indhibitiwa na majasusi wa Free Mansonry aidha majasusi hayo yameweza kuanzisha kitengo ndani ya Vatican yenyewe walichokiita Masonic Lodge-P2 kilichokuwa na mapadri, maaskofu na hata makadinali, ambao ndio waliokuwa wakiiendesha "Vatican city state" na ukatoliki kwa ujumla. Kupitia majasusi haya ya kimasonic na kimafia Vatican imekuwa ikijilundikia mali katika mabenki yake kupitia biashara haramu na utapeli ndani ya mabenki mbalimbali. Benki ya Vatican yenyewe ikawa imejilundikia mabilioni ya dola kupitia njia hizo za kitapeli na kimafia. Alipoingia Pope Albino Luciani(Pope John Paul) 1978, akataka kulisafisha kanisa katoliki. Kwanza kuivunja "Masonic Lodge-P2 kwa sababu kwa mujibu wa sheria za Vatican "Canon Law" kuwa mwanachama wa "Freemanson" ni kosa la kumfanya mtu atengwe na kanisa. Pili, akataka ufanywe uchunguzi wa kia ili ijulikane ni kwa njia gani Benki ya Vatican hujilundikia mapesa. Lakini Albino Luciani kabla hajapiga hatua ya kuliendea zoezi hilo, akauawa. Akaiacha Vatican ikiendelea na ujasusi wake na kujilundikia mapesa kwa njia mbalimbali za ulaghai. Pamoja na Albino Luciani, aliuawa Emilio Alexandrini aliyekuwa hakimu huko Milan akisimamia kesi dhidi ya Benki(Calvis Banco Ambrosiano) ambayo ilikuwa ikishirikiana na benki ya Vatican katika shughuli za kimafia. Mwingine ni Hakimu Vittoria Occorsio aliyeuawa ili kuzuia uchunguzi dhidi ya harakati za "Order P2" ndani ya Vatican. Aidha aliuawa Mino Pecoreli ambaye alikuwa mwanachama wa P2 lakini wenzake wakamtuhumu kuwa alikuwa akitoa siri. Wauaji wa Albino Luciani waliona kuwa endapo atauwa kwa risasi basi patazuka mtafaruku mkubwa utakaolazimisha upelelezi wa kina. Kwa hiyo wakaamua wamuua kifo cha ghafla. Ilitumika sumu ambayo haikuwa na ladha wala harufu kwa kulenga kuwa akisha kufa ghafla dai kuwa kafa kwa ugonjwa wa moyo(heart attack) litakubalika. Albino Luciani akawekewa sumu katika dawa yake ya kushusha pressure ikiwa imepigiwa hesabu kuwa itamuua kabla ya Alfajiri. Na kweli akafa. Albino Luciani alikuwa mcha Mungu kwa mtizamo wa kanisa alke aliyeazimia kusafisha uchafu uliokuwa ndani ya Vatican. Lakini akauawa na genge la maaskofu, mapadri na makadinali ambao tayari walikuwa katika biashara za kimafia na Freemansonry. Aidha majasusi hawa mipango yao ni ya kilimwengu wana watu kila kona ya dunia; mauaji yao hayaishii ndani ya Vatican na Italia tu. Marais, wanasiasa, waandishi wa habari na viongozi wengi wa dini na wanaharakati mbalimbali duniani wameuawa pale walipoonekana kugusa maslahi ya P2 ndani ya Vatican. Mfano Mtafiti na aliyewahi kuwa Afisa katika kitengo cha Usalama jeshini Marekani(Military counter Intelligence), bwana Paul A. Fisher ameandika kuwa aliyekuwa Rais wa Marekani(1800-1864) Abraham Lincoln) aliuawa kwa amri ya Pope.
Hata hivyo kanisa katoliki katika kuuzuga Umma, kwa sura ya nje, hujijengea sifa kwa wema, upendo, huruma na utoaji wa misaada ya kibinaadamu kwa waathirika wa majanga mbalimbali. Lakini maovu wanayoyafanya ni mengi sana kuliko kiasi wanachotoa kama misaada. Kwa mfano Bwana William T. Still anasema "genge" moja la aina hiyo huko Marekani mwaka 1984 lilikuwa limejilundikia Dola 1.979 bilioni. Wakati walitumia kiasi cha 29.8% tu ya fedha hizo kwa misaada . Aidha David Yallop amemtaja Kadinali John Cody ambaye aliwahi kumpa zawadi Pope John Paul II(1979) ya dola 50,000. Lakini uchunguzi baadae ukaonyesha kuwa alikuwa akijilimbikizia mapesa katika mabenki yake huko Marekani kupitia njia za utapeli na wizi wa "kimafia".
Chini ya mauaji, ukandamizaji,utapeli
na wizi huu unaofanywa na watakatifu wa kanisa kama huu kwa kisingizio
cha dini inaposimama kauli ya wajamaa kuwa dini haina na nafasi katika
jamii bali ni pumbao la kiakili linalotumiwa na wajanja wachache kuhalalisha
kuficha maovu yao. Wajanja hawa kwa kushirikiana na watawala dhalimu wa
kisiasa huwapiga bumbuwazi wafuasi watiifu kwa kuwaahidi uokovu wa kiroho,
ufufuko na malipo ya mbinguni ambayo ni uzima wa milele.
--
|
|