HALI ya utata uliyokuwepo katika suala la uvaaji wa Hijaab mashuleni umeondoka baada ya Mhe. Rais Benjamin William Mkapa kutoa ufafanuzi na maelekezo juu ya suala hilo.
Mhe. Rais Mkapa amesema kuwa kuvaa Hijaab na kuhudhuria swala ya Ijumaa ni haki ya Waislamu na hakuna wa kuizuia.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara Agosti 7 katika viwanja vya Mburahati Barafu Mhe. Rais Mkapa alisisitiza kuwa ni ruksa kwa Waislamu wanawake kuvaa Hijab wawapo shuleni na kwamba ni wajibu na haki ya wanafunzi Waislamu kuswali swala ya Ijumaa.
Pamoja na maelekezo hayo ya Mhe. Rais Mkapa imeelezwa kwamba Wizara ya Elimu iwajibike kutoa maelekezo kwa Wakuu wa mashule na Vyuo kwani wapo baadhi wanaoihujumu haki hiyo ya wanafunzi Waislamu.
Hujuma hiyo imeelezwa kufanyika kwa walimu kuwaruhusu watoto waende kuswali huku ratiba ya masomo ikiendelea kama kawaida.
Katika hotuba yake Rais Mkapa aliwaonya watu wa aina hiyo ambao alisema lengo lao ni kuleta mfarakano katika jamii.
Kwa ajili hiyo Waislamu kadhaa
walioongea na gazeti hili wamesema kuwa ni lazima Wizara isimamie utekelezaji
kwa kuhakikisha kuwa ratiba za masomo haizendelei wakati wanafunzi wengine
wamekwenda kuswali.
--
|
|