CHAMA cha Wananchi (CUF) kimeibuka kuwa kimbilio la wananchi baada ya mamia kwa maelfu wakazi wa Manispaa ya Morogoro kujiunga na chama hicho katika zoezi linaloendelea kuanzia wiki iliyopita.
Kufuatia kufanyika kwa mkutano wa hadhara uliohubiriwa na Makamu Mwenyekiti (Taifa) wa chama hicho Maalim Seif Hamad matawi yamekuwa yakifunguliwa kwa kasi huku watu kwa mamia wakikata kadi.
Akiwahutubia katika mkutano huo Mhe. Seif Shariff Hamad alisema kuwa pamoja na propaganda za CCM, CUF inazidi kuimarika na kuiacha CCM ikiwa imefiliska.
Alisema kuwa kughushi barua na propaganda mbalimbali za kuisingizia CUF kuwa ni chama cha kidini na Wapemba ni ushahidi tosha wa kufilisika kwa CCM.
Akizungumzia majina ya matawi kama Chechnya na Kosovo, Mhe. Seif Sharif amesema kuwa majina hayo yanawakilisha hisia za watu wanaoonewa na kudhulumiwa kama ilivyo kuwa kwa raia wa Kosovo na Chechnya.
Aidha, alisema kuwa kila watu wana haki na wana uhuru wa kuchagua majina wayapendayo. Na kwamba watu kuchagua majina kama Kosovo na Chechnya ni kuonyesha na kudhihirisha hisia zao za uonevu wanaofanyiwa na CCM.
Mhe. Seif Sharif Hamad aliongeza kusema kuwa kama CCM wanayaogopa hayo majina basi waache uonevu. Aidha, aliwataka wananchi wasimame imara kudai Tume Huru ya Uchaguzi ili kuleta mabadiliko ya kweli katika jamii.
Mhe. Seif alieleza kusikitishwa kwake na hali ya Rais kusifia ufanisi wake katika kukusanya kodi huku kukiwa hakuna uwiano wowote na ubora wa huduma za jamii na afya.
Katika tukio lisilo la kawaida kwa viongozi wengi wa siasa, Makamu Mwenyekiti huyo wa CUF alizunguka mji mzima kwa miguu karibu masafa yapatayo Kilometa 10 akifungua matawi.
Mkutano huo wa hadhara wa
CUF uliofanyika Jumamosi Agoati 7, ulihudhuriwa pia na wanachama wa chama
hicho toka Dar es Salaam ambao walikwenda kwa msafara wa magari yapatayo
themanini na sita (86).
--
|
|