SHERIA


Lugha ya mahakama

Na Dkt. Abdallah J. Saffari

Shughuli zote za mahakama ya Mwanzo ikiwa ni pamoja na kuendesha mashauri, kunakili ushahidi, kuandika hukumu, zinafanyika kwa lugha ya Kiswahili (F.25, Sheria ya Mahakama ya Mahakimu, i.h.j).

Kiswahili na Kiingereza huweza kutumiwa katika shughuli za mahakama ya Wilaya isipokuwa kumbukumbu za ushaihdi na hukumu lazima ziandikwe kwa Kiingereza (F.13(2), Sheria ya Mahakama ya Mahakimu i.h.j). Hata hivyo wakati wa kusikiliza mashauri ya rufani au kufanya masahihisho kutoka Mahakama ya Mwanzo, Hakimu anayehusika anaweza kutumia Kiswahili au Kiingereza kadiri anavyoweza (K.h.j).

Hivyo ni dhahiri kuwa kumbukumbu zote za ushahiri katika mashauri ambayo husikilizwa na mahakama hayo kwa mara ya kwanza lazima ziandikwe kwa Kiingereza. Sharti hili limeleta na litaendelea kuleta matatizo mengi mintaarafu ya utoaji haki sahihi kwa mujibu wa sheria za nchi hii.

Kabla ya uhuru, karibu mahakimu wote wa mahakama ya wilaya walikuwa wakoloni wa Kiingereza ambao hawakujua Kiswahili kabisa au kiasi cha kutosha. Hivyo isingewezekana kuandika kumbukumbu za mashauri waliyoyasikiliza kwa lugha ya Kiswahli. Sharti la kutumia lugha ya Kiingereza kutekeleza shughuli hiyo lilikuwa na shabaha ya kuwapunguzia au kuwaondolea kabisa wakoloni wazungu hao 'udhia' wa kujifundisha na kukielewa vyema Kiswahili.

Baada ya uhuru hali imebadilika sana mahakamu wote wa mahakama ya wilaya ni Watanzania ambao wanaelewa vyema Kiswahili. Hivyo hoja ya kuweka sharti la matumizi ya Kiingereza haina maana tena.

Uendeshaji wote wa mashauri katika mahakama ya wilaya kam avile kuhoji mashahidi hufanyika kwa Kiswahli. Ni mara chache sana huduma za wakalimani huhitajika. Ina maana, kwa hakika, kiutendaji, Kiswahili tayari ni lugha ya mahakama.

Kumtaka Hakimu kuandika kumbukumbu za ushahidi baadaye kuandika hukumu kwa Kiingereza ni kupuuza kweli bayana kwamba kwa hakika Kiswahili ndiyo lugha ya mahakama. Zaidi ya hapo kunawapa mahakimu mzigo mkubwa sana wa kusikiliza ushahidi unaotolewa kwa Kiswahili halafu wautafsiri kwa Kiingereza. Matokeo kumbukumbu za ushahidi hukosa usahihi, kutoeleweka vizuri, mchanganiko wa masuala pamoja na makosa mengi ya kisarufi. Na kwa vile hakimu huchukua muda mrefu kutafsiri maelezo ya mashahidi, mahojiano na mashahidi hufanywa taratibu. Jambo hili huwapa nafasi nzuri ya kutafakari majibu ya maswali wanayoulizwa, kitu ambacho huweza kuathiri ukweli wa ushahidi wao.

Usahihi wa ushahidi ni msingi wa utoaji haki. Hivyo basi kumbukumbu sahihi za ushahidi uliotolewa ni muhimu kwa kiasi kama hicho. Kwani ni kutokana na kumbukumbu sahihi za ushahidi ulionakiliwa na Hakimu ndipo hukumu nzuri inaweza kuandikwa. Katika shauri moja Hakimu aliandika 'tope' badala ya vumbi kwa vile alishindwa kutofautisha 'dust' na 'mud' upesi wakati ushahidi ulipokuwa unatolewa. Tofauti ya maneno haya ilileta athari kubwa sana katika hukumu iliyoandikwa baadaye. Utaratibu wa kuthibitisha kuwa ushahidi ulioandikwa awali sio sawa ni mgumu na haujulikani na wengi.

Wakati wa rufani mahakama Kuu hutegemea kumbukumbu za mahakama ya wilaya ambazo hudhaniwa kuwa sahihi. Zinapokuwa sio sahihi au kutoeleweka vyema husababisha matatizo makubwa na wakati mwingine haki kutotendeka.

Wakati wa ukoloni majaji wote walikuwa wazungu ambao hawakujua Kiswahili. Kwa hali hiyo wasingeweza kuzielewa kumbukumbu za ushahidi zilizoandikwa kwa Kiswahili na mahakama ya wilaya. Sasa hali hiyo nayo imebadilika.

Majaji wote wa mahakama kuu ni Watanzania wenye milki bora kabisa ya Kiswahili. Hapana shaka wataweza kabisa kuelewa pengine vizuri zaidi kumbukumbu za ushahidi na mahakama ya Wilaya kwa Kiswahili.

Linalosisitizwa hapa ni kuwa matumizi ya Kiswahli katika kunakii ushahidi ni muhimu mno na kwamba sheria inahitaji marekebisho hayo.

Kiingereza ndiyo lugha rasmi pekee ya mahakama kuu na mahakama ya rufani.

Hata katika mahakama hayo, hasa mahakama kuu, bado inadaiwa kuwa Kiswahili kiwe moja ya lugha rasmi (Katika makala yake aliyoyaita "A Critical Assessment of the Adjudicatory and Educative Role of the Court of Appeal as the Highest Judicial Organ in Tanzania". Dar es Salaam. 13 November, 1995. uk. 8. Jaji Robert Kissanga alisisitiza umuhimu wa kutumia Kiswahili katika mahakama ya Tanzania. (Haijachapishwa).

Sababu ni zile zile zilitozolewa awali lakini kuna moja ya nyongeza. Idadi kubwa ya warufani au warufaniwa katika Mahakama Kuu hawaelewi Kiingereza, pia hawana uwezo wa kutetewa na mawakili. Hivyo wao hutoa hoja zao za rufani kwa Kiswahili. Na hata mawakili nao wengi woa ni Watanzania ambao huweza kuyahutubia mahakama vizuri kwa Kiswahili. Kama hivyo ni sahihi hakuna sababu ya kumkataza Jaji anayependa, au anayekiri kuelewa vizuri Kiswahili, kuandika hukumu yake kwa lugha hiyo.

Kuhoji mashahidi

Madhumuni ya kuwahoji mashahidi ni kupata ushahidi muhimu katika uamuzi wa haki wa shauri linaloendeshwa. Lakini imeonekana kuwa kwa ajili ya sababu mbalimbali ushahidi huo muhimu haupatikani na ukosefu wa mbinu au ujuzi wa kuwahoji mashahidi. Athari hiyo inaweza ikawa kwa upande wa mashitaka au upande wa mshitakiwa. Hata hivyo matokeo yake ni yale yale: Kwamba ushahidi muhimu unaweza kufichika, shauri likaamuliwa kwa uzito wa ushaidi wa uongo, usiotosha na kadhalika. Hapo haki huwa haikutendeka.

--
 
--
Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook