Tahariri
Waliovunja daraja ndio wa kulijenga
YAWEZEKANA wapo watu wanajidanganya wakidhani kuwa kama wataweza kusimama bungeni na kufoka dhidi ya Uislamu huku wakishangiliwa na Wabunge watakuwa wameshinda. Yawezekana pia watu hao wakajidanganya kwa kudhani kuwa wakiwapa tegemeo la kupata ukiwa na kuwapata baadhi ya Waislamu waliopo bungeni waliosoma na wenye kuifahamu dini yao wakawafanya sifuri ya kushoto watakuwa wamefanikiwa.
Wanajidanganya kwa sababu hao hawawakilishi hisia za Waislamu wala Uislamu hautegemei vishindo au kimya cha Wabunge.
Kinachotia moyo ni huku mitaani kadiri vitimbi dhidi ya Waislamu vinavyoendelea ndivyo madaraja yanavyozidi kuvunjwa. Na kadiri khulka ya kuwakejeli Waislamu inavyozidi ndivyo Waislamu wanavyozidi kuimarika dhidi ya maadui.
Hata wale ambao walikuwa hawaamini kuwa kuna dhulma hawana haja tena ya kuwatafutia data wanaamini kuwa kuitambua Jumamosi na Jumapili kuwa siku za ibada lakini ukadai masaa mawili ya Ijumaa ni udini ni dhulma.
Inapokuja kuzungumzwa suala la amani yaelekea Wabunge wengine hulipa tafsiri tofauti. Kwamba kudumisha amani ni kudumisha Ukristo! Kuimarisha amani ni kuimarisha Ukristo na kulinda amani ni kulinda Ukristo! Ndio maana hatuwasikii wakihoji suala la 'Boxing day", Ubalozi wa Vatican", "Memorandum of Understanding" wala aliyosema Dk. Sivalon!
Lakini inapokuja suala la Uislamu ule msimamo hatuuoni. Ndio maana walishangilia walipoelezewa waliyofanyiwa Waislamu Mwembechai. Na ndio maana walimzomea Mhe. Prof. Kapuya juu ya suala la Hijaab na swala ya Ijumaa.
Walipokuwa wakimkejeli Prof. Kapuya kwa Ualhaj wake hawakujua kuwa kwa kufanya hivyo wamevunja daraja la kutuunganisha. Vinginevyo labda daraja hilo liwe ni migongo yetu ya wao kukanyaga wapite.
Lakini juzi Mhe. Kitwana Kondo aliposimama ilidhihirisha kuwa Wakristo wako ng'ambo ile na Waislamu ng'ambo hii. Wabunge Waislamu walishangilia huku Wakristo wakipiga kimya kama ambavyo Wabunge Wakristo walivyokuwa wakishangilia Kapuya akisulubiwa na Wabunge Wakristo. Daraja limevunjwa!
Kwa hapa tulipofika viongozi wetu wasitafute mchawi. Maadhali waliovunja daraja wanajulikana ni wao wa kulijenga. Na tusiulizane Waislamu wanakoelekea.
Tuliyoyadondoa katika hotuba ya Rais
Kuna dalili za kubomoka kwa mihimili ya umoja wa Taifa letu. Tumekuwa na umoja kwa sababu ya kuheshimiana bila kubaguana kwa dini, rangi, kabila au jinsia.
Wale wote wnaotenda vitendo vyenye kupelekea kuvunjika kwa umoja wetu wazomewe bila kuonewa haya.
Hata kama machafuko haya hayatatupata sisi yanaweza kuwafika watu wa vizazi vyetu. Ni nani anayetaka kizazi chake kije kiishi Somalia, Yugoslavia, Rwanda n.k.?
Yapo madai ya kubaguliwa kwa Waislamu kielimu, ajira, madaraka n.k.
CCM haina sera za ubaguzi kwa hiyo yeyote anayebagua siyo sababu ya sera bali ni yeye binafsi.
Bado sijapata ushahidi wa kutosha juu ya ubaguzi dhidi ya Waislamu. Walio na ushahidi walete.
Matatizo ya Waislamu ni matatizo ya taifa/jamii yanahitaji kutatuliwa kijamii.
Matatizo hayo ni ya kihistoria na yatahitaji muda mrefu kutatuliwa.
Nimeanza kushughulikia matatizo ya Waislamu mfanlo uteuzi ninaofanya mimi hivi sasa unazingatia dini.
Hili sio suluhisho la kudumu.
Suluhisho la kudumu litapatikana kwa kila mtu kupata fursa ya kupata elimu na huduma zote za jamii kwa uwezo wake wote bila kubaguliwa. Na katika kutatua matatizo haya ya jamii kusiew na mwenye kuona ameshindwa na mewnye kuhisi ameshinda.
Hata hivyo kuna sehemu ambazo hatuwezi kufanya uteuzi kwa kutumia dini. Zipo sehemu tunaweza kufumba macho. Sehemu zinazohitaji wataalam mfano Hospitali haziwezi kutazamwa kidini bali kitaaluma.
Kama kuna mtu anayebaguliwa shuleni au pengine popote kwa ajili ya dini yake nijulisheni nitachukua hatua.
Natoa onyo kali kwa yeyote anayebagua mtu kwa msingi ya dini, jinsia, rangi au kabila. Hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya yule ambaye itabainika kuwa anaendeleza ubaguzi.
Misahama ya ushuru na forodha.Mwaka uliopita misamaha kwa mashirika ya dini shilingi 9.8 bilioni.
Kama yapo mashirika ya Kiislamu yanayopata usumbufu katika kupata misamaha hii nijulishwe.
Uhuru wa nchi hii umepiganiwa na watu wa dini zote, ranig zote, makabila yote na jinsia zote.
Tunapozungumzia dhulma je, Muislamu hayumo?
PENGINE ipo hoja inapozungumzwa kuwepo au kutokuwepo kwa dhulma ielezew kwanza ni tafsiri gani inazingatiwa. Tunasema hivyo kwa sababu yapo mambo hapa ambayo kila mtu anayaona lakini kwa vile yanawahusu Waislamu, ghafla kila mtu haoni anashangaa.
Mtu kuwekwa ndani na kunyimwa dhamana mpaka anakufa na ule utaratibu tu kawaida wa kisheria hutoa taaarifa ya tukio hilo usitumike, dhulma ni ipi kama hii haimo! Vipi Muislamu anatunguliwa risasi kama swala na alyefanya hivyo hata zile hatua za kawaida za kisheria hazichukuliwi! Inakuwaje hii haionekani ni dhulma vinginevyo isemwe kwamba Muislamu hayumo inaposemwa hakuna dhulma.
Hapa kazuka Paroko na madai yake kuwa Yesu anatukanwa, serikali yote imekwenda mbio mpaka ikakiuka hata katiba, sheria na taratibu za kuendesha nchi, matokeo ikaishia kuwadhalilisha akina mama Waislamu, kuwatia vilema vya maisha baadhi ya Waislamu na wengine kuwaua.
Wakati tuhuma tu za Paroko zilifanya serikali itumie misuli yake kwa kiwango kilichoikiuka kawaida, hakuna anayeonekana kuguswa na na kufumuliwa mafuvu Waislamu kwa risasi pale Mwembechai. Ndio maana serikali mpaka leo haioni haja si ya kuunda Tume ya uchunguzi wala kuwapeleka wahusika mahakamani.
Sasa kama hii haionekani kama ni dhulma, pengine tuambiwe " Muslims do not count"!
Leo inapotolewa wito wa ushahidi wa kuwpo 'Data' na ushahidi wa kuwepo dhulma wanachi wanashangaa kwa sababu hawajapata kusikia kamati ya Alhaj Madabida kupewa nguvu za mamlaka kwenda mashuleni, Wizarani, jela na mahospitali kupata hizo 'Data'.
Bila kupewa nguvu ya mamlaka vipi utakwenda hospitali umuhoji daktari ilkuwaje mtoto Chuki akafungwa pingu asitibiwe hadi akapooza! Bila nguvu ya mamlaka vipi utamhoji Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Ali Ameir aeleze kipi kilitangulia mtoto Chuki kupigwa risasi ndio akakutwa na makaratasi ya uchochezi kama alivyodai (Ali Ameir) au walimkuta nayo ndio wakamtwanga risasi!
Kamati ya Alhaj Madabida ingewahoji vipi Maafisa wa magereza juu ya madai ya akina mama Waislamu kwamba walinyanyaswa na kudhalilishwa huku wakipekuliwa katika tupu zao na askari wanaume bila ya nguvu ya mamlaka!
Na bila ya nguvu hiyo wangemhoji vipi Paroko Lwambano juu ya madai yake ya kutukanwa Yesu. Aidha, wangewezaje kufuatilia kujua ni nani yule aliyeamrisha "piga shaba, piga yule" na mamlaka hayo aliyapata kutoka wapi!
Data juu ya watoto wanavyofaulu na wanavyochaguliwa kuingia vyuo vya elimu ya juu na kupata nafasi za kusoma nchi za nje zipo serikalini. Zitapatikana vipi bila ya kuwepo tume iliyopewa mamlaka ya kuzifungua faili na kuhoji watu!
Kamati ya Alhaj Madabida itatoaje data za kisayansi kuonyesha dhulma katika utoaji wa fursa za kusoma nchi za nje (scholarships) kama haikupewa uwezo wa kupata orodha ya waliopelekwa sifa zao na walivyopasika!
Mara nyingine mtoto awza kulaumiwa kwa uchafu kumbe kanyimwa sabuni.
Zipo hisia na mwelekeo hasi kuwa Muislamu ndiye siasa kali, gaidi, na mvurugaji wa amani. Katika mtizamo huo huo huonekana kuwa mtu wa kufadhiliwa asiyestahiki hata kile ambacho ni haki yake. Ndio maana hata mtu kama Profesa Kapuya amekejeliwa anaonekana kapewa Uwaziri kwa sifa ya Ualhaj sio Uprofesa. Na akidumu hudumu kwa kudhaniwa ni kiungo cha Ma-alhaj wenzake.
Wanateuliwa wakuu wa wilaya na mikoa ambamo hata wa daraja la nne wamo lakini japo theluthi ya Waislamu haionekani! Zimeundwa Bodi wanakaa Wakristo watupu wala hawaoni vibaya - kwa sababu tangu hapo ishajengwa dhana kwamba hawa ni wafadhliwa. Hawana uwezo wala hawapo!
Katika mambo ambayo hayajapoteza
tafsiri yake ni ukweli kuwa Waislamu walileta uhuru wa nchi hii. Kinachoshangaza
vipi waliopigania uhuru waitwe wavurugaji!
--
--
|
|