Na Munnawar Mussa
NILIKUWA abiria katika moja ya mabasi yatokayo Ubungo kwenda Kariakoo. Ndani ya basi hilo msafiri mmoja alianzisha malumbano yasiyo rasmi baada ya kumuona Mama mmoja aliyevaa hijab.
Baada ya msafiri huyo kuanzisha malumbano hayo, watu kadhaa walidakia ikiwa ni pamoja na yule Mama aliyevaa hijab na vijana (wanafunzi) wengine ambao niliwafahamu majina yao baadaye. Malumbano hayo yalikuwa kama ifuatavyo:
Mwanamke (Mgala): Hivi inakuwaje mwanamke kujifunika miguo namna hiyo!!!?
Mama (wa Kiislamu): Hii ndiyo taratibu ya Kiislamu tena unatakiwa ujifunike kiasi ambacho usiweze kuonekana mapambo yako wakati wote ukitembea njiani.
Mwanamke (Mgala): Je? Ukiwa nyumbani?
Mama (Mgala): Pia unatakiwa ujisitiri kiasi fulani.
Mwanamke (Mgala): Ah!! Jamani, si mateso haya. Ebu angalia bi mkubwa ulivyojifunika, huonekani hata sikio, namna hii inakuwaje kama ndiyo mtu anatafuta mchumba?
Mama (Mgala): Kama ni mchumba si atakwenda nyumbani kwao tu (mpaka awe wazi ndio anapata mchumba)!!
Mara Mwanaume (Mgala) akawaona wanawake wengine wanaopita njiani waliovaa Niqabu. Ah! Haya waangalie wanatisha... waangalie wanatisha..."
Mwanafunzi (Hamisi): Wako wapi wanaotisha?
Mwanaume (Mgala): Wale pale waangalie.
Hamisi: Ah!! Wanapendeza wale, kiko wapi sasa wanachotisha, kujisitiri tu!!
Mwanaume (Mgala): Ah! Bwana hawaonekani wala huwezi ukamjua.
Hamisi: Kwani wewe unawatakia nini.
Mwanaume (Mgala): Ni lazima bwana ujue kwamba mwenzangu nani, Mzungu, Mwarabu, Mswahili au...
Hamisi: Jalia kuwa yeye ni Mzungu halafu inakuwaje?
Abdallah: Kwani wewe mkeo anavaa hijabu?
Mwanaume (Mgala): Havai, hata kama akivaa nitamkimbia au nitamfukuza!!
Abdallah: Sasa wewe kinachokuuma ni nini? Hivi nyie akina mama na wewe baba wale wanaovaa Hijabu wamekosa nini? Hivi wale wanaotembea uchi barabarani na yule anayevaa vizuri tena kwa kujisitiri ni nani wa kumlaumu na kumsuta hebu tumieni akili!!
Abiria wengine: Huyu Bwana (Mgala) ana udini sana.
Mwanaume (Mgala): Hapana.
Kondakta: Hallow kaka shuka basi, kituo!!
Imekuwa ni kawaida kwa wanawake wa Kiislamu kutukanwa na kuudhiwa kwa kule kuvaa kwao hijabu katika sehemu mbalimbali, na hii ni kwa sababu baadhi ya sababu zifuatazo:
Kwanza jamii imefikishwa hatua kiasi kwamba maovu ndiyo maendeleo na mema kuwa mabaya na hii ni miongoni mwa zao la vyombo vya habari.
Pili, udini unazidi kuota
mizizi siyo kazini, shuleni, bali hata kwenye magari.
--
|
|