JUMUIYA ya vijana wa Kiislamu wa Vyuo na Sekondari hapa Songea imefanya uchaguzi wa kuwapata viongozi baada ya uongozi uliokuwepo kumaliza muda wake.
Viongozi hao ni Mwenyekiti Mohammed Ramadhani kutoka Songea Boys', Makamu Mwenyekiti Kondo Ngosa kutoka Ruhuwiko Sekondari.
Nafasi ya Katibu Mkuu imechukuliwa na Shaweji Maliki kutoka Songea Boys', Katibu wake msaidizi anakuwa Mustafa Juma kutoka Ruvuma Sekondari Muhazina alichaguliwa Rahia Mohammed kutoka Songea Girls'.
Jumuiya hiyo inaunganisha wanafunzi wa Kiislamu kutoka katika taasisi saba za elimu hapa mjini Songea zikiwa ni Songea Boys, Songea Girls sekondari na Ruvuma sekondari ya kutwa pamoja na shule ya sekondari ya Ruhuwiko inayomilikiwa na JWTZ pamoja na sekondari ya Kiislamu Msamala Muslim Seminary ya hapa mjini Songea.
Aidha, vyuo vinavyounda RUMUSA ni pamoja na Chuo cha Ualimu Matogoro T.T.C. na Chuo cha Wauguzi C.O.T.C. hapa Songea.
Mkutano huo wa uchaguzi ulifanyika Septemba 19, mwaka huu kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Ualimu Matogoro. Wanajumuia zaidi ya 200 walihudhuria mkutano huo pamoja na walimu walezi.
Kabla ya uchaguzi, Katibu Juma Nchia alitoa mada ya uamsho mbele ya wanajumuia na kutoa ufafanuzi juu ya Waraka wa serikali kuhusu masuala ya hijabu na sala ya Ijumaa, ambapo Katibu alitoa ufafaunzi wa mapungufu ya waraka huo na kusema safari ya mapambano dhidi ya dhuluma bado mpaka haki ipatikane na siyo nusu nusu, hivyo basi katibu huyo aliwataka Waislamu kutoridhika na waraka huo, bali kusonga mbele zaidi na kuwa na msimamo na kile wanachokidai.
Baada ya ufafanuzi, wanajuiya kwa pamoja walitoa kauli ya kutounga mkono waraka huo na kusema hiyo ni geresha ya serikali ya CCM dhidi ya Waislamu kwa sababu mwaka wa uchaguzi umefikia nao wanataka kupata kauli ya kusema serikali ya CCM inajali maslahi ya Waislamu kitu ambacho walidai sio kweli.
Katibu huyo aliwataka wanafunzi kutoa taarifa ya mapema kwa viongozi wao wanapoona walimu wanaendelea kufundisha wengine Waislamu wanapokuwa Msikitini, pamoja na walimu watakaotoa kauli za masimango kwa wanaovaa hijabu na kuwabeza.
Akielezea matatizo yanayoikabili RAMUSA kwa kipindi chote cha uongozi wao, Katibu huyo alisema tatizo ni walimu walezi kutokuwa tayari kushirikiana na viongozi kwani walimu wanataka wanayoyasema wao ndiyo yawe kauli ya mwisho jambo ambalo viongozi wa RAMUSA walilipinga na kuendelea kusema kauli ya mwisho ni ya Qur'an na Suna za Mtume (s.a.w.).
Katibu huyo alimalizia mada
yake kwa kusisitiza wanajumuia na wanafunzi wote Tanzania kumuunga mkono
Amir Sheikh Juma Mbukuzi.
--
|
|