MAKALA
 
Mirathi katika Uislamu - 5
 

KATIKA baadhi ya matoleo ya AN-NUUR miaka iliyopita tulieleza kwa kina falsafa ya mirathi katika Uislamu. Lakini suala al mirathi kwa mujibu wa sheria za Kiislamu limekuwa likiwakera sana wasioutakia mema Uislamu na miongoni mwao wamo wanaojiita Waislamu. Huenda ikawa suala hilo limekuwa likiibuka mwaka hata mwaka kwa sababu halijapatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa Waislamu kuelimishwa juu ya haki zao katika Uislamu za kutaka sheria ya mirathi ya Kiislamu ibadilishwe kwa kuwa inambagua mwanamke. Kelele zinasikika kila mara jamii inapojadili sheria mbalimbali za mirathi na wanapoichambua sheria ya mirathi ya Kiislamu hufanya hivyo bila kufahamu msingi wa sheria yenyewe. Katika sehemu ya tano ya makala haya BI. HAWRA SHAMTE anaeleza mantiki ya sheria ya mirathi katika Uislamu.

Iwapo warithi ni mchanganyiko wa wenye mafungu maalum na asaba, itabidi kutafuta kigawe kidogo cha shirika (lowest common multiple (LCM) ili kupata mafungu yatakayhogawiwa kwa kila mrithi kwa kadri ya haki yake anayoistahiki. Hebu tuangalie mifano kadhaa ya mgawanyo wa mirathi.

Kwa mfano 1:

Amekufa mke na kuacha:

i) mume

ii) mtoto mwanamume

iii) baba

Wenye mafungu maalum kati ya hawa ni:

i) mume - ana robi (1/4) madhali yupo mtoto

ii) baba ana sudusi (1/6) madhali yupo mtoto.

Asaba Mtoto mwanamume na atachukua kitakacho bakia.

Ugawaji

Mafungu yatakayotolewa ni 1.4 na 1.6. Hesabu ndogo ambayo inaweza kutolewa mafungu ya urithi ni 12 yaani LCM ya 4 na 6. Kwa hiyo mali ya uryhtii itagawanywa kwenye mafungu 12 yaliyo sawa sawa na ugawaji utakuwa kama ifuatavyo:

i) Mume atapata 1/4 ya 12 (1/4 x 12) = 3

Yaani atachukua mafungu 3 katika mafungu 12 = (3/12 - 1/4)

ii) Baba atapata 1/3 ya 12 (1/6 x 12) = 2 yaani atachukua mafungu 2 kati ya mafungu 12 - (2/12 = 1/6).

iii) Mtoto atachukua mafungu yaliyobakia 12 - (3 + 2) = 7, yaani atachukua mafungu 7 kati ya mafungu 12 - (7/12)

Mfano wa 2:

Amekufa mume na kuacha wafuatao:

- mke mmoja

- mama

- mjukuu mmoja wa kike (binti wa mtoto mwanamume)

- mtoto mwanamume

- watoto watatu wanawake.

Kama mali iliyoachwa na marehemu ni Shs. 1,200/-, utarthisha wahusika kama ifuatavyo:

Ugawaji:

Wenye mafungu maalum kati ya hawa ni:

- Mke ambaye atapata thumuni (1/8) kwa sababu wapo watoto

- Mama atapata sudusi (1/6) ya mali kwa sababu wapo watoto.

Mjukuu hapati kitu kwa sababu wapo watoto ambao humzuilia

- Mtoto mwanamume na watoto wanawake watagawana mali iliyho bakia, wakiwa hao Asaba mwanamume achukue sawa na wanawake wawili (2:1).

Njia mbili zifuatazo zinaweza kutumika katika kurithisha wahusika:

(a) Hisabu ndogo inayoweza kutolewa mafungu ni 24. Yaani LCM ya 8 na 6. Kila fungu litakuwa na thamani ya Shs. 50 - (1,200 + 24). Kwa hiyo:

- Mke atapata 1/8 ya 24 (1/3 x 24) = 3 yaani atapata 3 x 50 = 150/=.

- Mama atapata 1.6 ya 24 (1/6 x 24) = yaani atapata mafungu 3 ambayo ni sawa na shs. (4 x 50) = 200/=.

- Asaba watarithi mali iliyobakia ambayo ni 1,200 - (150 + 200) = 850/-.

Mali hii itagawanywa katika mafungu 5 (kumbuka: mwanamume atapata sawa na wanawake wawili). Hivyo, kila mtoto wa kike, atapata Shs.1 x 850/- = 170/- na mtoto wa kiume, atapata Shs. 2 x 850 = 340/- .

(b) Njia ya pili ni kutafuta sehemu ya mali atakayoipata kila mwenye fungu maalum. Kama mali inayorithiwa ni Shs. 1,200/-.

- Mke atapata 1/8 ya 1,200/- = 1/8 x 1200 = 150/=

- Mama atapata 1/6 ya 1,200 = 1/6 x 1200 = 200/-.

Asaba watagawana mali iliyobakia ambayo ni 1200 - 350 = 850/-.

Kuna binti 3 na kijana mmoja ambaye ni sawa na binti 2. Hivyo mali iliyo bakia itagawanywa katika mafungu 5 ambapo kila binti atapata = Shs. 1 x 850 = 170/-.

na kila mama watapata sawa na binti 2 Shs. 2 x 850 = 340/-.

Kuongeza Mafungu (Awl)

Iwapo idadi ya mafungu yatakayogaiwa kwa warithi wenye mafungu maalum ni kubwa kuliko mafungu yaliyopatikana kwa njia ya LCM, idadi ya mafungu itabidi iongezeke ili kila mmoja apate haki yake.
 
--
Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook