Pengo awaonya viongozi wanaotaka dini ziende wanavyotaka



KARDINALI Policarp Pengo amewatahadharisha viongozi wa serikali wanaotaka dini ziende kwa matashi yao.

Pengo alikemea tabia hiyo wakati akihutubia Wakristo waliohudhuria misa ya kumuombea hayati Mwalimu Nyerere.

Alisema dini haiwezi kutumikia dola na kwamba Kanisa Katoliki litaendelea kuwa na msimamo huo bila ya kutetereka.

"Viongozi wakijifanya waungu lao liwe juu ya dini hatutokuwa tayari kuwafuata", alisema Kardinali Pengo huku waumini waliofurika Kanisani akiwemo Rais Benjamin Mkapa na viongozi wengine wa serikali wakimsikiliza kwa makini.

Katika hotuba hiyo Kardinali Pengo pia aliwashutumu wanaomlaumu Mwalimu Nyerere kuwa aliwapendelea Wakatoliki wenzake.

"Mimi ni mmoja wa wale waliofuata kwa karibu maisha ya Mwalimu", alidai Kardinali huyo na kuongeza kuwa; "sijapata kusikia akisema anampendelea mtu kwa sababu ni Mkatoliki pamoja na kwamba yeye alikuwa Mkatoliki".

Matamshi makali ya Kardinali Pengo yamekuja wakati kukiwa na malalamiko kadhaa yanayotolewa na Waislamu dhidi ya serikali.

--
JuuRUDI



 


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji


   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org


An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook