Msihadaiwe mkaitupa dini yenu
 

WANAWAKE wa Kiislamu wameshauriwa kutokukubali vyeo na majukumu yatakayowasababisha waende kinyume na amri na makatazo ya Mwenyezi Mungu.

Wito huo umetolewa Jumamosi iliyopita Novemba 13, wakati wa semina iliyofanyika katika ukumbi wa kituo cha Utamaduni wa Iran jijini Dar es Salaam.

Bibi Zaynab Mwatawala, mwanafunzi wa sheria wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisema hakutarajia kumuona mke wa Rais wa Zanzibar Bibi Salma Salmini kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya urembo yaliyopita ambayo Bi Joyce Temu aliinuka kuwa mshindi.

Alihoji vipi mke wa Rais wa nchi ambayo ina Waislamu zaidi ya asilimia 90 akakubali kushiriki katika kukabidhi taji kwa waendao utupu?

Bibi huyo aliwaasa wanawake wa Kiislamu kutokubali kuwa chambo cha kushajiisha maovu katika jamii na hata kama mtu atafanya analolifanya kwa sababu ya wadhifa wake, ana haki ya kulikataa jukumu hilo kama linakwenda kinyume na itikadi yake.

--
Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook