TAHADHARI imetolewa na baadhi ya Masheikh wa Tanga kuhusiana na mikutano isiyo rasmi ya kujadili amani ya nchi.
Hii imekuja baada ya kikao cha tarehe 16 mwezi huu kilichoitishwa na mmiliki wa hoteli moja maarufu mjini hapa.
Katika barua yake ya muda mfupi kwa Masheikh tisa, Bwana huyo alisema watafiti wameona amani ya Tanzania iko hatarini kutokana na tofauti za kiimani.
Wakati wa kikao hicho, mwenyeji huyo alisema yeye alitakiwa aitishe kikao hicho na mmoja wa marafiki zake ambaye ni afisa wa usalama wa taifa ili kusikiliza maoni ya Waislamu wa Tanga.
Wawili kati ya Masheikh tisa, ambao hawakupenda kujitambulisha gazetini majina yao walisema wanashangaa kwanini mwaliko uje kwao peke yao badala ya taasisi, na kwanini uitishwe na mtu mmoja mmoja.
Vile vile walihoji kwanini amani ya nchi iwashughulishe watu wa nje zaidi, kama ambavyo watafiti wametajwa kuwa ni wa kutoka nje.
Katika kuzidi kuhoji Masheikh hao wamesema
mambo yenye kuweza kuhatarisha amani tayari yamejadiliwa kwa kina kwenye
nyaraka kadhaa zilizowahi kutolewa.
--
|
|