Vitabu vya Mungu si vya kuapia Ikulu
 

KUONGOZA kwa dhana potofu badala ya mwongozo wa Allah ndio tatizo kuu linalowakabili walimwengu.

Vitabu vya Mwenyezi Mungu vimefanywa vya kuapia tu watu wakipewa madaraka lakini mafundisho yake hayafuatwi.

kuvidhalilisha vitabu vya Mwenyezi Mungu.

Amesema viongozi huvikejli kwa kuripia, kisha wakaviweka kando wakaongoza kwa kufuata matamanio yao.

Matokeo yake, amesema ni kupatikana 'utwaghuti' aliye adui mkuu.

Amesema, dini zote zinapinga mauaji, ulevi, zinaa, wizi, rushwa na dhulma. Hivyo wananchi waisaidie jamii kuwachagua viongozi watakaopambana na maovu hayo.

Viongozi wanaoona pombe ni burudani na uzinzi si tatizo maadam mtu hapati ukimwi, hao watatuangamiza, ametahadharisha.

Kwa mtizamo huo, Sheikh Mbukuzi amewataka wananchi, kuipa jamii uongozi unaojua matatizo yake.

Amesema kuwa Hayati Mwalimu Nyerere aliwahi kutamka kuwa moja ya matatizo ya nchi hii ni rushwa. Akawataka wananchi wasaidie kupata viongozi watakaopambana nayo.

Lakini rushwa ni matokeo tu ya tatizo la kuporomoka kwa maadili, amesema Sheikh Mbukuzi.

Ndio maana mpaka leo hakuna dalili ya rushwa kuondoka.

Sheikh Mbukuzi amesema kuwa mtu muadilifu hawezi kudhulumu haki ya mtu kwa kutoa au kupokea rushwa.

Amesema ili kuisaidia jamii, watu watafute viongozi wanaojua kuwa tatizo ni kuporomoka kwa maadili ya jamii. Viongozi wenye maadili mema na wanaoweza kupambana na yale yanayozaa maovu.

Wakati huo huo, Amir wa Waislamu, Sheikh Mbukuzi amewataka vijana wa Kiislamu, 'kuvaa' Uislamu wao popote walipo.

Amesema akina mama na mabinti wameonesha mfano, kwa kuvaa hijabu zao hata wakienda makazini.

Huwezi kusema hakuna udini iwapo baadhi ya watu wanatupa utamaduni wao na taratibu zao, kuwafuata wengine.

"Ni lazima watukubali na ndevu zetu, kanzu zetu, kofia zetu na lugha yetu", alisema Sheikh Mbukuzi.

Amewataka vijana popote walipo wakumbatie utamaduni na mavazi ya Kiislamu na sio kuukumbatia, umagharibi.

"Vaeni Kiislamu popote, ustahimilivu wao ndio utaonesha kuwa hakuna udini", alisisitiza Sheikh Mbukuzi.

Amir Sheikh Juma Mbukuzi, ameeleza hayo na kuwataka wananchi waitoe dini Misikitini ikaongoze maisha yao mitaani.

"Hatuwezi kuinusuru jamii kama tutaruhusu utwaghuti uimarike huku tikidhania maadui wetu ni umasikini, ujinga na maradhi", alisema.
--
Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook