Wanusurika kufa baada ya kula matunda yenye sumu
 

WANAFUNZI 18 wanaosoma darasa la tatu katika shule ya msingi Mwere mjini hapa wamenusurika kufa baada ya kula matunda ya mti unadhaniwa kuwa na sumu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mwishoni mwa wiki iliyopita, Kaimu Mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw. Philimon Kibuya alisema kwamba tukio hilo lilitokea majira ya saa 4.00 asubuhi wakati wanafunzi hao walipokuwa mapumziko.

Alisema wanafunzi hao wakiwa pembeni ya shule walishawishiwa na mwenzao mmoja ambaye aliwaambia kuwa mbegu za mti ambao upo shuleni hapo tangu mwaka 1952 zinaliwa, hivyo wote wakabandua maganda na kuanza kula.

Aliendelea kusema kuwa mara baada ya mapumziko ambayo waliingia darasani na kuanza kufanya mtihani wa hesabu, ndipo wanafunzi hao wakaanza kuhema na wengine kutapika hali ambayo ilimchanganya mwalimu aliyekuwa anasimamia mtihani huo, mwalimu Grace Malya na kulazimika kwenda kumtaarifu Mwalimu Mkuu.

Mwalimu Kibuya alieleza kwamba ikabidi wawatafutie maziwa na kuwanywesha na hatimaye kuwakimbiza hospitali ya mkoa na kuwekewa chupa za maji, ambapo baada ya saa moja wanafunzi tisa kati ya 18 wakapata nafuu muda wa saa sita mchana na kuruhusiwa huku wengine hali zao zikiendelea kuwa mbaya zaidi.

Aliongeza kusema kwamba ilipofika saa mbili usiku wanafunzi waliobaki wakaruhusiwa kutoka baada ya hali zao kuendelea vizuri.

Aliwataja wanafunzi walionusurika kufa ambao wote ni wa darasa la tatu kuwa ni Zainab Abdallah (11), Asha Said (11), Mariamu Magiri (12), Mbarakati Swalehe (10), Arafa Musa (12), Farida Faridi (12) na Neema Abdulrahman (12).

Wengine ni Doris Ngogo (12), Matilda John (11), Jenifa Mbaka (11), Batul Hassan (11), Amina Abdallah (10), Zena Salehe (11), Madalu Sangweni (10), Maria Constantine (10), Zena Mohammed (9) pamoja na Faterian Josephat ambaye ndiye aliyedaiwa kuvumbua tunda hilo na kuwashawishi wenzie kula.

Alipoulizwa ni hatua gani uongozi huo utachukua ili kukabiliana na janga kama hilo lisitokee tena ambapo miti hiyo ipo mitatu shuleni hapo, Mwalimu Mkuu msaidizi alisema: "Sasa hivi tumeshauriana Afisa Mtendaji wa kata na tunafanya mipango ya kukata ili isije kuzua balaa lingine".

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umegundua kuwa tukio hilo kutokea katika eneo la shule siyo la kwanza, ambapo miaka ya nyuma liliwahi kuwatokea watoto wa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mchikichini ambaye alikuwa anaishi kwenye nyumba zilizopo pembeni mwa shule hiyo.

Vile vile uchunguzi umeendelea kuonesha kuwa mti kama huo vile vile upo katika shule ya msingi Kilakala ya jijini Manispaa Moro kufanya ukarabati.
--
Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook