Habari za Kimataifa
 

'Kuanzisha harakati ni rahisi, kuzidumisha ni kugumu'

Kabul

MAWAKALA wa makafiri wakiwa katika mavazi ya Kiislamu wamesababisha madhara makubwa kwa Uislamu na Waislamu. Wamefanya iwe rahisi kuanzisha harakati za Uislamu lakini iwe kuna ugumu kuzidumisha.

Maelezo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa serikali ya Kiislamu ya Afghanistan, Maulana AbdulHakeem Muneeb wakati akiongea na timu ya maulamaa (wasoma) kutoka Pakistan.

Alisema Afghanistan imekuwa ikikabiliwa na magumu mbalimbali yakiwemo majanga ya njaa, mashinikizo toka nje na mitihani ya mara kwa mara.

"Hayo ni kwa sababu ya kulinda na kutetea itikadi na udugu wa Kiisamu", AbdulHakeem aliuambia ujumbe huo.

Aidha, aliwataka Waislamu duniani kote wakumbuke wajibu wa kuwasaidia ndugu zao wa Afghanistan katika kulikarabati taifa hilo jipya la Kiislamu.



Maelfu ya cassette chafu yachomwa moto Pak-Afghan

Tarkham

KATIKA kuelekea kusimamisha jamii yenye kuzingatia maadili ya Kiislamu nchini Afghanistan, Idara ya kuamrisha mema na kukataza maovu, imechoma moto maelfu ya kanda za radio na video, mapicha ya uchi, majarida na machapisho mbalimbali yanayokiuka maadili.

Uchomaji moto huo ulifanyika eneo la mpaka wa Afghanistan na Pakistan (Pak-Afghan) na kushuhudiwa na umati mkubwa wa wananchi wa nchi zote mbili waishio eneo hilo.

Hatua hiyo ilichukuliwa chini ya usimamizi wa askari wa kujitolea wa idara hiyo ambayo pia iliunguza madawa ya kulevya iliyoyakamata kwa watu waliokatiza mpaka huo hivi karibuni.



Magereza Afghanistan yazingatia haki za binadamu

Kabul

MAGEREZA nchini Afghanistan yameripotiwa kuwatendea wema na ubinadamu wafungwa wa makosa mbalimbali.

Magereza hayo huwapa wafungwa chakula safi na matibabu bora.

Kwa mujibu wa gazeti la Dharbi Muumin linalochapishwa nchini Pakistan, magereza hayo hivi sasa yamefungua maktaba ili kuwawezesha wafungwa kujipatia maarifa mbalimbali wawapo magerezani.

Taarifa iliyotolewa hivi karibuni kuhusu hali ya magereza nchini humo zimeeleza hivi sasa umeandaliwa mpango kamambe kuhakikisha kuwepo kwa mazingira safi na lishe bora kwa wafungwa katika magereza.

Aidha, umeandaliwa mkakati maalum kwa ajili ya kubadili tabia za wafungwa kwa kuwapa malezi ya kidini muda wote wa vifungo vyao.

Afghanistan hivi sasa inaongozwa na serikali yenye uelekeo wa Kiislamu iliyoundwa na wapiganaji wa Talaban baaa ya kuikomboa nchi ho kutoka kwa mabeberu na vibaraka wao.


Barua ya aliyekuwa kamanda wa wapiganaji wa Kashmir Shahiid Sajjad kwenda kwa mama yake
 
 

Mama yangu mpendwa,

Assalaam Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh!

MWENYEZI Mungu (s.w.) akuzidishie imani, mwenendo mwema na afya njema. Akupe heri na fanaka duniani na akhera. Rehma zake zilizomo ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ziendelee kukushukia tena na tena - Aamin.

Ni matumaini yangu kuwa uko salama kwa uwezo wa Allah (s.w.). Mpaka sasa niko salama na naendelea na funga ya Ramadhani katika mazingira haya magumu.

Mama! Usiwe na wasiwasi juu yangu. Wewe ni miongoni mwa wazazi waliobahatika kuwa na watoto waliotoa mali, muda na nafsi zao kwa ajili ya kusimamisha dini ya Allah (s.w.).

Mama yangu mpendwa, kumbuka maisha haya si lolote ila ni mapito, kwa hiyo kama si leo basi kesho utakuwa miongoni mwa wakazi wa makaburini kusubiri siku ya mwisho. Kwa hiyo ukiyapokea machungu na misiba ya muda mfupi ya ulimwengu huu kwa subira na kumtukuza Allah (s.w.) kwa hakika utakuwa miongoni mwa watakaozawadiwa siku ya kuogopesha ambayo hapatakuwa na wa kumsaidia mwingine kila mmoja atashughulika na lake. Ni matendo mema aliyoyatenda katika maisha haya ndiyo yatakayomsaidia.

Kwa hiyo mama yangu mpendwa, najua una huzuni na uchungu mkubwa kwa kunikosa, lakini ni huzuni ya muda mfupi ya kutenganishwa baina ya mama na mtoto, ambayo ukiipokea kwa subira, dua na ahadi ya kumcha Allah (s.w.) katika hali yoyote ile, kwa hakika Allah (s.w.) atatusaidia siku ambayo wote watahukumiwa kwa matendo yao.

Ni ipi subira hiyo? Ni subira isiyo na malalamiko, tuhuma wala maombolezo. Subira ya kuulazimisha moyo kufuata maamrisho ya Allah kinyume na matashi yake.

Nakusalimu sana wewe, baba na wengine wote. Nasikitika kuwa sikupata kukuandikia barua kabla ya hii.

Kwa waumini, ulimwengu huu ni wa mapambano, harakati, mitihani na huzuni. Na kadri muumini atakavyokabiliana na mtihani au magumu ajue Mwenyezi Mungu atamfidia kwa malipo mema katika maisha ya kudumu ya Akhera ambako hatakuwa mwenye khofu wala huzuni.

Kwa kuwa lengo letu la maisha katika ulimwengu huu ni kumtii na kumnyenyekea Allah (s.w.), tuwe tayari kupokea rehma zake tukiwa majumbani mwetu, vitani au katika selo za magereza. Mcha Mungu sehemu zote hizi hanabudi kuzipa hadhi inayofanana.

Aina yoyote ya maisha atakayojaaliwa mcha Mungu huyu itambakisha kuwa mwenye furaha na kuridhika.

Nasubiri kwa furaha kufa shahidi mikononi mwa maadui wa Uislamu.

Mwisho, nakuomba ujichunge na uchunge amali zako huku ukikumbuka siku ya hisabu.

Pamoja na dua.

Ni mimi mwanao,

Sajjad Khan
10 Ramadhan 15, 1996
Februari 5, 1996.

Shahid Sajjad Khan ni muasisi wa jihadi nchini Kashmir aliuawa na majasusiwa India hivi karibuni.


Mfuko kwa ajili ya Waislamu Chechnya
 

Hivi sasa kuna maelfu ya wajane na mayatima wanaohitaji misaada ya hali na mali kutoka kwa ndugu zao katika imani duniani kote.

Al-Rasheed inakusanya misaada na zaka za waumini ili:

Kuipeleka moja kwa moja kwa familia zilizoathirika, wajane na mayatima walioachwa na mashahidi waliokufa vitani.

Kununua madawa na vifaa kwa ajili ya kuwatibia waliojeruhiwa.

Kuwasaidia wote wenye kuhitaji misaada.

Kupambana na njama za maadui wa Uislamu katika uwanja wa habari na mawasiliano.

Waislamu kote duniani wanawajibika kuwasaidia ndugu zao wa Chechnya na Afghanistan.

Tuma msaada wako kupitia:

Al-Rashiid Trust
Opposite Darul-Iftawal Irshad
Nazimabad No. 4, Karachi
Post Code 74600
Pakistan

Simu: 6683301

Fax: 6623814

Al Rasheed Account No. 4245774
Dollar Account No. 0550 17-41
Pound Account No. 065001-38

Habib Bank Ltd Foreign Exchange,
Habib Square, Karachi, Pakistan.
 

--
Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook