Mkapa adhibiti uchapaji fedha
 

UDHIBITI wa uchapaji na usambazaji wa fedha unaofanywa na Benki Kuu, umetajwa kuwa miongoni mwa mafanikio makubwa ya Rais Mkapa.

Aidha, imeelezwa kuwa Rais amefaulu kwa kiwango kikubwa kutekeleza masharti ya IMF na Benki ya Dunia.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni, Mwenyekiti wa CUF, Prof. Lipumba amesema uchapaji wa fedha umedhibitiwa na hivyo kupunguza ongezeko kubwa la bei za vitu.

Hata hivyo, Prof. Lipumba amesema, kwa miaka minne ya uongozi wa Rais Mkapa, kipaumbele katika matumizi ya serikali imekuwa kulipa madeni ya nje na matumizi ya kila siku ya kuendesha serikali.

Katika hali hiyo, amesema, miradi ya maendeleo haipati fedha na huduma za jamii kuzorota kabisa.

Ameeleza kuwa, katika kipindi hiki uchumi umekuwa kwa asilimia 3.5. Hata hivyo akasema kuwa, ikilinganishwa na kasi ya kukua idadi ya watu ambayo ni 2.8 asilimia; uchumi kwa wastani haujaongezeka kiwango chochote cha maana.

Amesema, awali ilani ya uchaguzi ya CCM (1995) iliweka lengo la kukuza uchumi kwa kiwango cha chini cha asilimia 6.

Profesa Lipumba amesema kuwa takriban nusu ya wananchi huishi chini ya wastani wa umaskini.

Kwa upande mwingine amesema kuwa pengo kati ya maskini walio wengi na matajiri wachache, limekuwa likiongezeka kwa kasi ya kutisha.

"Vijana walio wengi wanakata tamaa kwa shida na kiwango cha ukosefu wa kazi kinakua kila leo", amesema.

--
Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook