Uchambuzi wa Kisayansi
 
Serikali inapoandaa njama kuwahujumu wananchi
 
Na Abu Luqman

"IT may be necessary to ask.. Why the establishment of just two Muslim Seminaries created panic and so much intense opposition from a number of quaters? If it is arqued that the government wanted to uphold a principle of equality of educational opportunity to all which had been violated, this does not square off with the fact that there existed ten times as many Christian seminaries, as Muslim ones and yet Christians were not called to account or justify the exclusive nature of their schools".

Tafsiri:

"Pengine ni muhimu kujiuliza, kwanini kuanzishwa kwa seminari mbili za Waislamu kumeibua hofu kubwa ya ghafla na upinzani mkali kutoka kila upande? Kama ni hoja kuwa serikali ilitaka kudumisha kanuni iliyokiukwa ya usawa katika fursa za elimu, hii haiendi sambamba na ukweli kwamba zimekuwepo seminari za Wakristo nyingi zaidi ya mara kumi ya hizi za Waislamu na haijawahi wahusika kuhojiwa juu ya uhalali wa shule hizo".

Hii ni hoja iliyopo katika Tasnifu (thesis) (1992) ya PhD ya mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu kimoja huko Canada.

Utafiti katika tasnifu hiyo ya Dk. Abidin Chande ulikuwa unaangalia pamoja na mambo mengine ubaguzi uliopo katika elimu Tanzania.

Hoja iliyonukuliwa ilikuwa ina hoji kwanini serikali ilikuja juu na kuamuru shule za seminari za Kinondoni na Jumuiya zifungwe mwaka 1982.

Utafiti katika tasnifu hiyo unaonesha kuwa baada ya shule za Kinondoni na Jumuiya kugeuzwa kuwa seminari (1981), upinzani ulinzia kwa Wakristo wakidai kuanzishwa kwa shule hizo ni kuleta ubaguzi katika elimu.

Kilichofuatia, mtafiti anasema ni serikali kutoa Waraka No. EDC6/50/151 wa Aprili 4, 1981, uliosainiwa na Tabitha Siwale, Waziri wa Elimu wakati huo.

Waraka huo ulidai kuwa kutokana na sheria ya Elimu Na. 25 ya 1978, seminari sio shule.

Kwa hiyo wanafunzi wake hawatafanya mitihani ya kidato cha nne kama wanafunzi wengine, hawatachaguliwa kwenda kidato cha tano wala kupewa ajira.

Wakati huo kulikuwa na seminari zaidi ya ishirini za Wakristo na ziliendelea kutambuliwa kama shule na wanafunzi wake kuchaguliwa kwenda kidato cha tano, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Vyuo vingine.

Pamoja na Waraka huo Waislamu walihiari kuendelea na seminari zao japo wafanye mitihani kama wanafunzi wa kujitegemea.

Kwa vile kilichokuwa kimekusudiwa ni kuwa Waislamu wasiwe na shule zao pekee, Mwalimu Nyerere aliingilia kati na kuamuru zifungwe.

Sheikh Adam Nasibu ambaye alitumika sana katika kuzivunja shule hizo alitoa hoja kuwa zinavunjwa kwa kuzingatia Waraka wa serikali. Kwamba wanafunzi wa shule hizo hawatachaguliwa kwenda kidato cha tano wala kupewa ajira.

Maelezo ya Sheikh Adam Nasib yalichapishwa katika gazeti la Mfanyakazi la Novemba 6, 1982.

Kufuatia maelezo hayo ya Adam Nasibu, TASNIFU tuliyoinukuu hapo juu inahoji "... Never the less he (A. Nasib) forgot to mention that in 1982, the year which the new regulations were supposed to come into effect Christian private secondary school leavers from Christian seminaries completed as usual on an equal footing with public school students for admission to form V in government schools.

This information is available in the Ministry of National Education Booklet which contains the names of students who have been admitted to technical institutes and form V in government schools.

This raised suspecious among some Muslims that the guideline was really intended to function as a pressure tactic to induce them to accept the suggestion to break up seminaries".

Tafsiri:

"Hata hiyo (A. Naibu) alisahau kutaja kuwa mwaka 1982 ambapo ndio ilikuwa Waraka huo uanze kufanya kazi bado watoto kutoka seminari za Kikristo walichaguliwa kuingia kidato cha tano katika shule za serikali. Ushahidi ni vitabu vyenye orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kuingia shule za serikali za ufundi na kidato cha tano".

"Hali hii iliibua wasiwasi kuwa Waraka ule ulitolewa kama njama kuwashinikiza Waislamu wavunje seminari zao".

Baada ya seminari za Waislamu kuvunjwa Waraka wa serikali haukufanya kazi. Seminari za Kikristo zikaendelea kutambuliwa kuwa shule.

Na juhudi zozote za Waislamu kusajili shule nyingine zikakwamishwa mpaka njama hizo zilipofichuliwa na Prof. Kighoma Malima.

Haya ndiyo tuliyovuna baada ya uhuru. Kuwa na serikali inayoandaa njama ili kuwapora baadhi ya wananchi haki yao ya kuelimika!

Huu ndio urithi wetu, wa kuambiwa "Seminari za Kikristo zaendelea kutesa", lakini hatuelezwi kumbe nyuma ya pazia yapo mengi. Tumelijua hili la Waraka wa Tabitha Siwale, mangapi hayajulikani?

Hii ndiyo serikali inayodaiwa kutokuwa na dini. Hii ndiyo serikali iliyodaiwa kutaifisha mashule ili watu wote wasome!

Ndiyo pia inayodai kutokuwa na ubaguzi wala unyanyasaji kwa misingi ya dini!

Ni ndiyo hiyo inayowasuta Waislamu leo kuwa (eti) huko nyuma walipuuza elimu na haiwezi kuwapa vyeo kwa mgawo, wakasome kwanza kama wenzao Wakristo!

Wakati wa msiba wa Mwalimu Nyerere ziliimbwa ngonjera nyingi sana kuwa, Mwalimu alikuwa mzalendo na Mtanzania namba moja.

Asiyependelea na asiyebagua watu kwa misingi ya dini.

Na kwa sifa hizo, inadaiwa alifanikiwa kuondoa udini.

Hili ni pumbao la kisiasa na 'bangi' la kuwatia uzezeta Waislamu.

Isemwe tu wazi kuwa Mwalimu alifanikiwa kuwadhibiti Waislamu wasihoji dhulma iliyokuwa ikiendelea.

Baada ya Waraka wa hadaa wa Wizara ya Elimu (1982) ili kuwadhulumu Waislamu, ni serikali hiyo hiyo leo inajipa kazi ya kukusanya ushahidi wa kisayansi (na tekinolojia ?) kujua kuwa ipo dhulma dhidi ya Waislamu au la.

Wanaulizwa walioko Bandarini, Reli, ATC, Posta na kadhalika watoe ushahidi wa dhulma.

Huko ni kuwafanya watu wengine katika jamii ni 'majnuni'.

Mwalimu alianzisha UPE baada ya kutaifisha mashule. Lakini elimu ya juu bado ilifanywa ya watu maalum.

Tanga ambapo Waislamu ndio wengi, wanafunzi kutoka Bara wasio Waislamu ndio waliojaza mashule ya sekondari ya Tanga, Usagara na Popatlal.

David Court katika kitabu chake "The Education system as a Response to Inequality in Politics and Public Policy in Kenya and Tanzania (New York, 1979) anaeleza kuwa, sera ya kutaifisha mshule na UPE haikusaidia Waislamu.

Amesema Elimu kwa wote (UPE) iliyotolewa ilimuandaa mtu kuishi katika jamii ambayo haikuwepo. Jamii ya kijamaa.

Hivyo mfumo wa elimu ulikuwa na faida kwa wale wachache tu waliopewa fursa kuendelea na elimu ya juu.

Lakini penye upendeleo hakuna upendo wala umoja wa kweli.

Ripoti ya Tume ya Baraza la Makanisa (Christian Council of Churches) ya 1978, juu ya hali ya elimu ilihadharisha juu ya kuendelea kuimarika kwa matabaka katika jamii (Waislamu na Wakristo) (Taz: A.E. Baalawi; Nyerere and Muslim Tanzania).

Kutokana na kuimarika kwa mfumo wa kidhalimu na onevu dhidi ya Waislamu; Ali A. Mazrui na Michael Tidy katika kitabu chao, Nationalism and New States in Africa (London: Heineman 1984), wanahadharisha juu ya malalamiko ya Waislamu na matokeo yake katika masiku yajayo.
 
--
Juu RUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania 
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook