Ufugaji holela wa nguruwe:
 


Kossovo kali kuzuka Tabata


WINGU la hali ya hatari linasemekana kutanda katika maeneo ya Tabata wanapofugwa nguruwe kinyume na sheria za miji.

Taarifa kutoka maeneo mbalimbali jijini zimeeleza kuwa Waislamu wamekuwa wakitafakari namna ya kukabiliana na wafuga nguruwe katika maeneo ya makazi.

Huko Tabata Kimanga, vikao vimekuwa vikifanyika kujadili hatua ya mtu mmoja anayejenga banda la kufugia nguruwe katikati ya makazi ya Waislamu.

Waislamu hao waliitisha kikao Januari 2 ili kumuhoji muhusika wa banda hilo la nguruwe. Hata hivyo Bwana huyo aliyefahamika kwa jina moja la Bwana Nene hakutokea katika kikao hicho.

Mwenye banda hilo la nguruwe ametakiwa akafugie ufugaji wake huo mbali na makazi ya watu.

Mjumbe wa Tawi la CCM shina Na. 35 Kimanga alithibitisha kupokea malalamiko ya Waislamu na barua ya kumwita mwenye banda kwenye kikao.

Baadhi ya vijana waliohojiwa na gazeti hili wamesema, kero ya nguruwe itaondolewa na Waislamu wenyewe.

"Maadhali sheria hazifuatwi na wanasiasa hawataki kuwahukumu wafugaji nguruwe 'Wachechen' tutafanya kazi hiyo", alisema kijana mmoja bila ya kufafanua.

Akiongelea suala hili Bw. Hussein Vunja ametaka Waislamu wa Misikiti yote wafahamishwe ili waungane nao juu ya suala hili.

Bw. Abdillah Salim Mpate aliyeandika barua kwa tawi la CCM kwa niaba ya Waislamu ameeleza wasiwasi wake juu ya athari itakayowakumba Waislamu iwapo ufugaji wa nguruwe utaanza katikati ya makazi yao.

Kwa muda mrefu yamekuwepo malalamiko dhidi ya ufugaji na uuzaji wa nyama ya nguruwe bila kufuata sheria husika wala kujali hisia za Waislamu.

Inasemekana Mhe. Rais Mkapa ametoa msimamo wake kuwa hawezi kuwahukumu wala nguruwe kwani ni Rais wao pia.

--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org

 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook