Wachechen waapa kupambana nao
UINGIAPO mji wa Grozny jirani na kilichokuwa kituo cha mabasi, unakutana na maandishi makubwa yaliyoandikwa ukutani kwa wino mzito mweupe yenye ujumbe ufuatao:
"Ee Mwenyezi Mungu waweke miongoni mwa Mujahidiin wale wote waliokufa katika nyumba hii ya huzuni".
Wanajeshi wa Russia kwa aibu ya kushindwa na wapiganaji wa Chechnya walihamishia hasira kwa raia.
Waliendesha mateso na mauaji dhidi ya raia wa jimbo hilo.
Likiripoti mateso hayo mabaya, jarida la The Muslim linalochapishwa nchini Marekani, limeandika kwamba watu walikuwa wakitumbukizwa kwenye mashimo ya kuhifadhia mafuta kisha mashimo hayo kugeuzwa vyoo.
"Askari wa Russia walikuwa wakiwaendea haja ndogo watu hao waliotumbukiza mashimoni, kutoka hapo wakiwachukua hadi kwenye selo za mateso", limeandika jarida hilo.
Likiendelea limeeleza kuwa selo hizo za mateso zilizungushwa nyaya za umeme ukutani, askari wa Russia waliwashtua raia hao kwa umeme kisha huwaleta mbwa wa njaa wakawatafuna wakiwa hai.
Baadaye majeruhi hao huchomwa moto hadi kuwa majivu kuficha ushahidi wa jinai ya vita kujulikana na vyombo vya haki za binadamu duniani".
Aina nyingine ya mateso limeandika gazeti hilo kuwa ni ile ya kupigilia misumali ndimi za wahanga hao. Baadaye ndimi hizo hukatwa kisha hulazimishwa kunywa maji ya moto. Hatimaye hutumbukizwa kwenye mapipa ya moto kuwakaanga hadi wakamalizika kabisa.
Pamoja na unyama huo, Wachechen wameendelea na msimamo wa kutetea na kulinda itikadi yao dhidi ya serikali ya Russia.
Wanasema silaha yao kuu ni kumcha Mwenyezi Mungu ili wastahiki msaada wake pamoja na maguvu na uwingi wa askari wa adui InshaAlah waibuke washindi katika vita hivyo.
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |