Sera ya CCM ahadi hewa - Lipumba


Na Bakari Mwakangwale

TATIZO la nchi hii ni sera za 'ahadi hewa' za chama Tawala.

Zimekuwa zikitolewa ahadi za kuwaondolea kero wananchi na kuboresha maisha yao, zote zimeishia kuwa propaganda za majukwaani.

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, ameeleza hayo na kusisitiza kuwa CCM haina ubunifu na uwezo wa kusimamia shughuli za maendeleo.

Akiongea na wakazi wa mikoa ya kusini hivi karibuni Prof. Lipumba amesema hivi sasa CCM wanang'ang'ania tu madaraka kwa manufaa ya watu binafsi.

Mwenyekiti huyo alieleza kuwa ikiwa wananchi wa mikoa ya kusini wataendelea kusema kuwa CCM ndio mama ndio baba, umasikini utandelea kuwapo mikoa hiyo miaka nenda rudi.

"Tunahitaji mwamko wa kisiasa wa kusema kwamba sasa CCM imetuchosha", alisisitiza Mwenyekiti huyo.

Aidha, alieleza kuwa umaskini wa mikoa ya kusini ni kukosa sera ya mawasiliano, sera ya kilimo na huduma bora kwa wakulima.

Akizungumzia ujenzi wa barabara ya Kusini amesema, hivi sasa kuna watu (wafadhili, mashirika, serikali) ambao wanahitaji kusaidia nchi masikini, lakini kwa masharti kuwa misaada hiyo iwasaidie wananchi walio masikini, na isitumiwe na watu wachache kujenga mahekalu badala ya mabarabara.

"Ikiwa kama serikali ya Tanzania itawahakikishia wanaotoa misaada , kama fedha za misaada zitatumika kujenga barabara na hazitayeyuka, basi barabara ya Kibiti-Lindi itajengwa", alisema.

"Tunaloshindwa kufanya Tanzania hivi sasa ni kuwahakikishia watoa misaada kwamba kweli wakitoa misaada wa kujenga barabara, barabara hiyo itajengwa", alisisitiza.

Prof. Lipumba aliwaeleza wananchi wa kusini waishio jijini kuwa barabara ya Kibiti-Lindi inaweza kujengwa kama serikali ina nia ya kujenga barabara hiyo.

Prof. Lipumba alieleza kuwa watu wengi ni masikini, japo wanautajiri wa maliasili, lakini hamna barabara na huwezi ukawa na maendeleo bila mawasiliano ya uhakika.

Amesema hali hiyo imemstaajabisha balozi wa Norway aliyetembelea mikoa hiyo hivi karibuni, na kuona utajiri wake.

Mwenyekiti huyo wa CUF alitoa wito kwa wananchi wa kusini kusaidiana kuimarisha chama kwa mikoa ya kusini: "Tusaidiane kuhamasisha wananchi wa mikoa ya kusini", alisisitiza. nia ya kujenga barabara hiyo.

Prof. Lipumba alieleza kuwa watu wengi ni masikini, japo wanautajiri wa maliasili, lakini hamna barabara na huwezi ukawa na maendeleo bila mawasiliano ya uhakika.

Amesema hali hiyo imemstaajabisha balozi wa Norway aliyetembelea mikoa hiyo hivi karibuni, na kuona utajiri wake.

Mwenyekiti huyo wa CUF alitoa wito kwa wananchi wa kusini kusaidiana kuimarisha chama kwa mikoa ya kusini: "Tusaidiane kuhamasisha wananchi wa mikoa ya kusini", alisisitiza.

--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org

 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook