Serikali kumaliza mgogoro wa Walutheri kwa njia ya amani!
SERIKALI inafuatilia kwa makini mgogoro wa Walutheri, Mwanga na itahakikisha unaisha kwa amani.
Hayo ni maelezo yaliyotolewa na Mwandishi wa Rais jana akiongea na waandishi wa habari.
Ni jambo jema kama serikali imeona umuhimu wa kuingilia kati mgogoro huo. Tena kuingilia kwenyewe kwa azma ya kuzuia machafuko na pengine mapambano.
Ni jambo jema kwani mpaka sasa watu washajeruhiwa na wanaendelea kufanya hivyo huku uharibifu wa mali ukifuatia.
Mgogoro wa Mwanga unayahusisha makundi mawili ya Dayosisi moja yanayopingana. Moja likidai kujitenga na kuunda Dayosisi yao mpya.
Hadi kutolewa kauli hii ya serikali, hakuna ushahidi wowote madhubuti wa kuituhumu serikali kuwa imechukua upande katika mgogoro huu.
Na kwa kauli hii hakuna ishara kuwa itatumia vyombo vya dola vya mabavu dhidi ya kundi moja kwa maslahi ya jingine.
Hawaelekei kufanya hivyo kwani, hiyo itachochea fujo zaidi na mapambano, wakati serikali inataka amani.
Lakini zaidi tunaamini inaangalia maelekezo ya katiba na sheria za nchi katika kuliangalia suala hilo.
Tunaamini busara hii ya serikali ingetumika, Paroko Lwambano alipowatuhumu Waislamu kumtukana Yesu, polisi wasingefikia hatua ya kuwaua Waislamu.
Tunachojiuliza, zile kauli za vitisho, shari na mapambano za serikali mbona hazisikiki katika mgogoro huu na mingine inayowahusu Wakristo.
Ubalakala katika kufuata sheria na kanuni
za utendaji kazi wa serikali ni moja ya mambo yanayoashiria kuwepo kwa
dhulma na ubaguzi katika nchi. Na mara zote ubaguzi na dhulma, havijengi
umoja, amani na mshikamano katika nchi.
--
![]()
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |