Kesi ya mabomu:

Utetezi Februari 27


IKIWA inaingia mwaka wa nane kesi Na. 431 inayowahusisha Bwana Mohammed Saleh na wenzake ilisikilizwa Jumatatu wiki hii katika Mahakama ya Kisutu.

Katika kesi hiyo Mabwana Mohammed Saleh na Mzee AbdulRahman Kileo na wenzao wengine wanadaiwa kukutwa na mabomu "yaliyodhamiriwa" kulipua Makanisa na viwanda vya pombe.

Shahidi wa mwisho upande wa serikali ambaye ni "mlinzi wa amani" aliieleza mahakama kuwa maelezo yaliyotolewa na mshitakiwa wa kwanza yanathibitisha kuwepo kwa mpango.

Maelezo hayo shahidi huyo alidai mahakamani hapo kuwa yalitolewa na mshitakiwa mwenyewe katika mahojiano maalumu akiwa mahabusu.

Hata hivyo, ilidaiwa kuwa makovu na alama za mateso alizokutwa nazo mshitakiwa ziliashiria kuwa alilazimishwa kusaini nyaraka husika kinyume na ridhaa yake.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 27, mwaka huu ambapo upande wa washitakiwa utaanza kutoa utetezi wake.

Kesi ya mabomu ni miongoni mwa kesi kadhaa zilizofunguliwa mwaka 1993 dhidi ya Waislamu kufuatia kuvunjwa kwa mabucha ya nguruwe.

Kabla ya kuanza kusikilizwa kesi hiyo washitakiwa waliwekwa rumande zaidi ya miezi sita hadi pale mahakama kuu chini ya Jaji Anthony Bahati ilipoingilia kati na kuamuru wapewe dhamana.

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani mwaka huo Bwana Augustine Lyatonga Mrema ni miongoni mwa mashahidi wa upande wa serikali waliokwishatoa ushahidi dhidi ya Waislamu hao.

Katika moja ya madai yake dhidi ya Waislamu wakati ule Bwana Merma alipata kusema kulikuwa na majambia yaliyoingizwa nchini ili kuanzisha vita vya jihadi dhidi ya Wakristo.

Bwana Mrema hivi sasa ni Mwenyekiti wa Chama cha upinzani cha Tanzania Labour Party (TLP).

--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org

 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook