Na Kamaludin Mustafa
NIMESOMA kwa makini maelezo ya Moses Nnauye katika gazeti moja litolewalo kila siki mara moja kwa lugha la Februari 3, 2000, hadi sasa sijaelewa kwa nini aliamua kutoa maelezo kama yale hasa wakati huu ambapo Waislamu wengi nchini wameamua kuvunja kimya cha muda mrefu kuhusu dhulma ya serikali dhidi yao. Si kwamba Waislamu hatukujua udhalimu huo siku zote bali ni kwa sababu wakati muwafaqa ulikuwa haujafika.
MOSES anaanza kujitambulisha kuwa yeye ni mtoto wa Sheikh, Maalim na Imamu wa Msikiti na kwamba jina alilopewa na wazazi wkae ni MUSSA, lakini sasa anaitwa MOSES. Hajaeleza ilikuwaje akalitupa jina huru alilopewa na wazazi wake na badala yake kuwa na jina la ubatizo la Moses. Anatoa hoja kwa kueleza kuwa Moses na Musa ni sawa isipokuwa wakati Musa ni jina la Kiarabu, Moses ni la Tourati au Kilatini.
Muhammad Ali, bingwa wa zamani wa ngumi za uzito wa juu duniani alikuwa anaitwa Charles Clay likiwa ni jina la ubatizo, lakini akiwa tayari ni mtu maarufu na tajiri aliamua kwa khiyari yake bila kulazimishwa wala kushawishiwa kulikataa jina la Charles la ubatizo na akajiita Muhammad Ali baada ya kubaini kuwa dini yake ya asili ni Uislamu na kwamba Charles lilikuwa ni jina la kitumwa.
Kila aliyesoma historia anajua unyama uliofanywa na wakoloni wazungu wakisaidiana na kanisa, hadi leo unawakuta watu weusi Marekani. Udhalimu huu uliofanywa na wazungu wa kuwakamata na kuwapeleka Waafrika utumwani ambapo wengi pia walifia njiani athari zake ziko hadi leo.
Tunapozungumzia umaskini wa Afrika na utajiri wa Ulaya na Marekani hatukosi kujua kuwa wazungu walitajirika kwa gharama ya Waafrika, Waafrika hatukuumbwa maskini bali tumekuwa hivi baada ya mababu zetu waliokuwa na nguvu za kufanya kazi na akili nyingi za ugunduzi kupelekwa utumwani na wengine kuuawa kikatili.
Tunamtarajia kiongozi wa ngazi ya juu serikalini kusimama kidete na kudai kuwa lazima wazungu watoe fidia kwa unyama wao waliotufanyia kama wanavyofanya Waisraeli kwa kudai na hatimaye kufidiwa kwa unyama waliofanyiwa wakati wa utawala wa Manazi.
Kwa mafundisho ya Uislamu kila mtu anayezaliwa huzaliwa akiwa ni Muislamu ndio maana Waislamu hawawapeleki watoto wao Misikitini kuwabatiza, maana ukishambatiza tu tayari umeshamuondolea uhuru wake aliozaliwa nao ambo ni Uislamu. Kwa kuijua maana Muhammad Ali akaamua kurudi katika asili yake, ndio maana mtu yeyote asiye Muislamu akiamua kusilimu tunasema kuwa amerudi katika dini ya asili.
Mtu kujiita Muislamu safi lakini sio Mujahidina huu ni ufinyu wa kuelewa maana ya Jihadi. Jihadi katika Uislamu lina maana pana sana, tofauti na baadhi ya watu wanavyofikiri. Ukizungumzia jihadi vichwani mwa watu hao inawajia picha ya Muislamu aliyeshika panga tayari kwa kumchinja kafiri.
Kupigana vita katika Uislamu kunaitwa Qitaal, lakini jihadi ni pamoja na kuamrisha mema na kukataza maovu katika jamii bila kujali wadhifa, kwa mfano kupiga vita rushwa, kazi hii inaweza kuwa ni ima kwa kupigana vita (Qitaal), kuzungumza kwa mdomo, kuandika kwa kalamu au hata kuamua kuchukia tu nyoyoni unapoona maovu yakitendeka japokuwa hii ya kuchukia tu ni imani dhaifu. Kwa mnasaba huu ni vigumu kwa mtu mwenye dhamana ya uongozi katika jamii awe ni Muislamu bila ya kuwa Mujahidina.
Lakini hii inanikumbusha nyuma wakati wa utawala wa awamu ya kwanza tulipokuwa viongozi wa sasa waliokuwa hawana elimu nzuri ya kuwalinda na hiyo ili waweze kulinda nafasi zao za kisiasa iliwabidi wajipendekeze kwa Master wao kwa kukiri kuwa hawana dini.
Watu hawa ni wengi ni wale ambao wazazi wao walikuwa ni Waislamu na kwa vile Muislamu katika awamu hiyo ilikuwa ni vigumu kupata wadhifa wa juu serikalini au kwenye mashirika yake akadumu nao vizuri wakati huo akijinasibisha na Uislamu, watu hawa waliona kujiita Wakristo moja kwa moja ni vigumu na hivyo wakabaki kujiita kuwa hawana dini bali ni wajamaa/wakomunisti, kwa mujibu wa Uislamu huu ndio ukafiri halisi na hii ndio dini yao, rejea Qur'an sura ya 119.
Wahenga wanasema kuwa "aliyekwisha umwa na nyoka huogopa hata mjusi". Hivyo Waislamu wa zamani baada ya kujaribu njia nyingi za kupambana na ukoloni zikashindikana, kwa mfano vita ya Majimaji, waliamua kuuogopa hata mjusi kwa kukataa kuwapeleka watoto wao katika shule za wazungu wakoloni.
Elimu wakati wa ukoloni ilikuwa haimuandai Mwafrika kujikomboa kifikra wala kiuchumi bali ilikuwa ni ya kumuandaa ili aendelee kumtumikia mzungu, na Waislamu wasingekuwa tayari kwa hilo hawakuwa wajinga, maana kama wazee Waislamu wangekubali watoto wao wabatizwe katika shule za misheni pengine Waislamu tusingekuwepo, lakini sasa Alhamdulillah tupo, baadhi yetu tumesoma tunaielewa vema dini yetu na dunia yetu, na tunaheshimiwa. Ndio maana hata wengine leo wanajitokeza kifua mbele kama Waislamu tena safi jambo ambalo wasingediriki kulitamka katika utawala wa awamu ya kwanza.
Wapo Waislamu wengi ambao walikataa dhulma ya kubatizwa kwa nguvu lakini sasa wanayo maisha mazuri. Kuna Waislamu ambao wana biashara zao hawatarajii kustaafu.
Lakini tunapozungumzia dhulma katika elimu na madaraka serikalini tunashangaa kurudishwa nyuma wakati wa ukoloni, wakati ni miaka 40 sasa tangia tupate uhuru. Huu ni umri wa mtu mzima unaotosha mtu kusoma hadi shahada ya udaktari wa falsafa, hapa hatumaanishi kuwa wasomi Waislamu hawapo, wapo tena wengi lakini hawawiani na wenzao Wakristo, leo hata kama safu nzima ya viongozi katika ofisi ya Rais watakaa pembeni watapatikana Waislamu wenye elimu nzuri wa kujaza nafasi hizo.
Mchujo wa wanafunzi kutoka darasa la saba kujiunga na kidato cha kwanza uliokuwa unafanywa kwa dhulma dhidi ya wanafunzi Waislamu si wakati wa ukoloni bali ni baada ya uhuru, kama ungefanyika usawa tangia pale tulipopata uhuru leo tungekuwa hatuzungumzii uwiano mbaya kielimu.
Masheikh waliosoma vizuri dini wanajua kabisa kuwa (Al-Slamu Alddyn Waddawla) yaani Uislamu ni dini na dola, huwezi kuacha dola iendeshwe na watu wasiomjua Mungu halafu ujiite Muislamu kamili, na huwezi kuendesha dola bila ya elimu.
"Tafuteni elimu hata kama ni China". Mtume (s.a.w.) wakati anatoa Hadith hii alikuwa Uchina wakati huo Uislamu ulikuwa haujafika lakini alitaka kuwahimiza Waislamu umuhimu wa elimu kupatikana popote na kwa mtu yeyote.
Mtume (s.a.w.) anasema kuwa: Binadamu anapokufa amali zake/vitendo vyake vote hukatika isipokuwa vitatu tu, navyo ni Sadaka inayoendelea, kwa mfano alijenga barabara kwa jitolea hivyo kila watu wakipita malipo mema humuendea huko aliko.
Elimu yenye manufaa yaani kama aliwafundisha watu mambo ya kuwafaa kila wakiyafanya basi malipo mema humendea marehemu.
Mtoto mwema mwenye kumuombea dua njema.
Kama hatunayo haya uhai wetu umeruka matupu.
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |