MAONI YETU

Hii siasa au 'alinacha'


AKISOMA maazimio ya semina ya Baraza la Maimamu, Sheikh Zubeir Yahya, Imamu wa Msikiti wa Kwa Mtoro alisema:

"Tumeamua kushirikiana na waumini wa dini zote na hatutawafanyia uadui wafuasi wa dini yoyote na badala yake tutaendelea kuitumia dini yetu kuharakisha maendeleo ya wafuasi wa dini zote". (Taz. UHURU No. 17380, Machi 13, 2000).

Kauli hii imeibua maswali mengi ambayo, lau hayatapatiwa majibu sahihi yatawachanganya waumini.

Uadui gani Maimamu hao walikuwa nao dhidi ya wasio Waislamu? Lini waliuanza uadui huo na kwasababu gani? Lini na kipi kimewatanabahisha? Je, ni vilio na malalamiko ya hao watu wa dini nyingine?

Maendeleo gani wanayaharakisha kwa manufaa ya wafuasi wa dini zote. Je, wanajenga mashule! Wanajenga mahospitali! Wanamipango yoyote ya kueneza huduma bora za maji safi! Wanamipango ya kiuchumi kuboresha hali za maisha kwa vijana na akina mama?

Bila maswali haya kupatiwa majibu munasibu, itakuwa vigumu kuelewa mazingira ya semina hiyo ya Maimamu na maazimio yake.

Katika mazingira ya Tanzania, dini za Kikristo, Kihindu na Baniani ndizo zinazohodhi maendeleo ya kiuchumi, afya, elimu na huduma za jamii. Aidha, baadhi ya watu hao ndio wanaohodhi madaraka ya nchi.

Je, Maimamu hawa wa Baraza la Maimamu (sio Shura ya Amir Mbukuzi) waliwahi kushirikishwa kuleta maendeleo hayo? Wao na watoto wao, nini nafasi yao katika maendeleo hayo! Je, ni maendeleo gani watayaleta ya kuwamegea wafuasi wa dini hizo ambao tayari wanahodhi 'keki' ya uhuru wa nchi!

Ni jambo jema iwapo Maimamu wetu wameona wazitumie nafasi zao kuleta maendeleo ya Watanzania.

Lakini kama si 'alinacha' au siasa za mazingira ya 2000, tunarataji maendeleo hayo yaanze kuonekana kwa waliokaribu zaidi na Maimamu hao.

Tuone vijana wa Kiislamu wasio na ajira na akina mama Waislamu wasiokuwa na mitaji hata ya kuanzishia mama ntilie, wakionja matunda ya maazimio ya Maimamu hao.
--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org

 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook