Wahukumiwe walioua kwanza
BAADHI ya vyama vya siasa viliwahi kuwaambia wafuasi wao na wananchi kwa ujumla kuwa uonevu sasa basi.
Hakuna tena kupigwa shavu la kulia ukageuza na la kushoto. Sera za "hewala bwana baada ya kukung'utwa bakora" si zama zake.
"Sasa ni jino kwa jino, jicho kwa jicho na pua kwa pua". Kwa sera hiyo vyama hivyo vimekuwa vikishutumiwa kwa dai la kutishia amani ya nchi na kuchochea umwagaji wa damu.
Inapokuja suala la amani ya nchi ni haki kabisa watu wote, vyama vya siasa na vyombo vya habari vihusike kuisemea.
Haiyumkini mtu atishie amani ya nchi atizamwe tu. Lakini mtu anaposema amechoka kuonewa sasa ni jino kwa jino, hapana sababu ya mtu muungwana asiyewaonea wenzake kuwa na wasiwasi.
Maana kwa kanuni ya kisasi, hatang'olewa jino asiyeng'oa la mwenzake. Ataingia kiwewe tu yule iliyo ada yake kuwapofua wenzake macho yao na kuwanyofoa pua zao.
Akifanya hivyo huku akitaraji wahusika waridhike na wasifurukute.
Inatupa wasiwasi tunaposikia makelele yanayopigwa dhidi ya sera hiyo ya jino kwa jino.
Je, hiyo ni ishara kuwa wapo wanaowaonea na kuwadhulumu wenzao na wangependa tu waendelee na udhalimu wao?
Kama huui nafsi ila kwa haki kwanini uhofie na uogope haki ya kisasi!
Ni katika muktadha huu tunasema kabla ya kuipigia kelele 'sera' hii ya jino kwa jino tuwakemee kwanza na tuwahukumu waliokwisha ua.
Hawa ni pamoja na viongozi wa serikali na CCM walioridhia mauaji ya Waislamu Mwembechai.
Pamoja nao ni viongozi wa Makanisa waliochochea mauaji hayo.
Huwezi kukemea wanaotoa wito wa jino kwa jino huku wewe mwenyewe ni muuaji!
Na makelele haya yanatutia wasiwasi. Inaonesha bado wapo watu wanaotaka waendelee kuwatwanga wenzao risasi na ummah ukae kimya.
Tukemee na kuwashughulikia wanaotoa amri
wenzao watwangwe risasi za moto, sio wanaowataka wajihami wakionewa.
--
![]()
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |