NASIKITISHWA sana na baadhi ya Masheikh wanaouza imani yao kwa maslahi ya muda mfupi ya dunia. Badala ya kukemea ufisadi kama alivyoagiza Allah, wao wanawaunga mkono mafisadi.
Kitendo cha Masheikh maarufu wa Dar es Salaam kutoa matamshi dhidi ya Waislamu kuwa wanawachukia waumini wa dini nyingine kinathibitisha kuwa Masheikh wetu hao wamo katika mtandao wa propaganda dhidi ya haki za Waislamu.
Hakuna ushahidi wa kihistoria wala wa kisayansi unaoonesha kuwa Waislamu wamekuwa na matatizo na waumini wa dini nyingine nchini. Hata mazingira ya jamii yetu yanathibitisha ukweli huo.
Sasa Sheikh anapokwenda kinyume na maneno ya Mwenyezi Mungu "Wala-takfu-maa-laisalakabihi ilmu-inna sania wal-baswara walfuadaa-kul-ulaaika kana 'anhu-mas-u-la". Sijui anatarajia nini mbele ya Mola wake.
Naamini hata hao viongozi ambao Masheikh wetu wanajaribu kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa, pia wanashuhudia nyoyoni kuwa Masheikh wananena kauli isiyothabiti. Wanafarijika kuwa kumbe wataingia bega kwa bega na "wacha Mungu hao" mahali pasipostahili kukaliwa na kiumbe.
Kuwa na aya au Hadith nyingi kichwani sio kigezo cha kuingia peponi. Mwenyezi Mungu anasema:
"Inna-l-ladhina-hummilu taaurata-thumma-lam-yahmiluuhaa kamathali-l-himari.
Ni hasara iliyoje Masheikh wetu. Kwa hakika aya za Qur'an hazipitwi na wakati maadamu wanadamu wanaendelea kuishi.
Ipo kanuni moja kuwa mtu asipomtumikia Allah, basi atamtukimia shetani. Asipotenda haki, ataenda dhulma. Asipotenda wema, atatenda uovu. Asipokuwa upande wa haki atakuwa upande wa dhulma.
Masheikh wetu hao hawakufungua vinywa kutetea waliodhulumiwa Mwembechai, ssa kanuni hiyo inawarudi kwa kuwatetea madhalimu.
Waislamu tunawatenge Masheikh wa aina hiyo.
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |