Saudi Arabia-3


Sekta ya Usafiri na Mawasiliano

UFALME umeendeleza ipasavyo miundombinu (visaidia uchumi) vya kisasa ikiwemo mfumo bora kabisa wa reli iunganishayo eneo la mashariki ya nchi hadi Jiji la Riyadh ambalo ndiyo mji mkuu wa Saudia. Kwa nyongeza tu, serikali inamtandao imara wa usafiri wa anga na imejenga bandari za kisasa kabisa kwa ajili ya usafiri wa bahari huko Pwani ya mashariki na ya magharibi ya nchi. Mwandishi MUSSA ALLY anaelezea zaidi katika sehemu ya tatu...

UREFU wa jumlawa njia za usafiri wa ardhini katika ufalme huo umepungua toka kilometa 41,615 zisizojengwa mwaka 1970 hadi kilometa 8,000 zisizojengwa mwaka 1993.

Aidha, urefu wa barabara za mashamba umeongezeka toka 35,000 kwa kipindi hicho hicho ambapo zaidi ya Riali bilioni 120 za Kisaudia zilitumika kujengea barabara nchi nzima. Tofauti na hapa kwetu reli iliyojengwa wakati wa Mdachi (Mjerumani) inaendelea 'kutamba' hadi karne ya sayansi na teknolojia.

Kwa upande wa reli iunganishayo mashariki ya nchi na mji mkuu Riadh, ufalme umeweka njia mpya na ya kisasa kabisa ya reli kwa kuing'oa ya zamani.

Njia ambayo inawezesha kupitisha garimoshi nne za mwendo kasi kila siku kwa kutumia masaa manne tu kumaliza kilometa 450 za safari toka Riyadh hadi Damman (Kwa kasi hii ingechukua takriban mwendo wa massaa 10 kufika Kigoma hapa kwetu ambapo wasafiri huwachukua siku tatu kufika kwa gari moshi yetu na reli zetu zilizopitwa na wakati)

Na kwa upande wa usafiri wa majini idadi ya maeneo ya kina kirefu kwa ajili ya meli kuzipiga nanga yameongezwa toka 27 mwaka 1975 hadi 179 mwaka 1992/93 ikiwa ni pamoja na maeneo 23 katika Bandari ya mji wa viwanda wa Jubail wa King Fahd na ile ya mji mwingine wa Yanbu wenye maeneo 22.

Idadi ya kampuni ya meli za Kisaudi ni 114 ambapo ufalme pekee unamiliki meli kubwa kabisa 11 huku ukiwa na lengo la kununua nyingine 48 haraka iwezekanavyo!

Na kwa usafiri wa anga, Saudia ina viwanja 25 vya kibiashara, kati ya hivyo 14 ni viwanja vya kiwilaya, vinane vya kimkoa na vitatu vya kimataifa.

King Khaled International Airport, Riyadh ni moja ya viwanja vikubwa na vya kisasa kabisa vya ndege si tu Saudia, bali duniani. Kina ukubwa wa eneo la kilometa 225 za mraba, ambacho kipo umbali wa kilometa 35 toka katikati ya jiji la Riyadh. Kilifunguliwa mwaka 1983 na kimesanifiwa kuhudumia abiria milioni saba laki tano kwa mwaka.

King Abdulaziz International Airport, Jeddah, ni kiwanja kingine mashuhuri cha kimataifa nchini humo kilifunguliwa mwaka 1981, kikiwa na ukubwa wa eneo la kilometa 105 za mraba na kuchukua nafasi muhimu mno katika kipindi cha Hijja.

Dhahran International Airport kilichoko mkoa wa mashariki kina ukubwa wa eneo la kilometa za mraba 780! Kiwanja hiki kinafanana kwa ukubwa na ubora zaidi na kile cha King Fahd International Airport ambacho kinaendelea kujengwa katika eneo hilo.

Serikali ya Saudia pia inautajiri wa ndege 111 za abiria na mizigo ikiwa ni pamoja na "Lockheed, Tristas, Airbus na hata dege kubwa aina ya Boeing 747-4000. Ndege hizi zinamilikiwa na shirika la ndege la serikali liitwalo Saudi Arabia Airline ambalo lina jumla ya wafanyakazi 10,000 wakiwemo marubani 1,000 wa Kisaudi wakifanya safari za ndani (Local routes) na za nje (International routes) ya nchi hiyo.

Idadi ya abiria waliosafiri na shirika hilo imepanda hadi kufikia milioni 18.5 kwa mwaka 1992/93!

Mawasiliano

Moja ya maendeleo muhimu ambayo Wasaudia wanapaswa kupigiwa mfano na nchi zinazoendelea ni yale ya miradi ya maendeleo.

Mtandao wa mawasiliano mbali na yale ya kisasa ya kompyuta (Internet) ambapo Saudia inajivunia kuyatumia huku ikiwa imejizatiti kwa tadhadhari zote za kimaadili, Saudia imo katika orodha ya nchi zenye mitandao ya hali ya juu kabisa ya mawasiliano duniani.

Saudia ina vituo vya simu 273 ambayo pia hutumika kutuma telegramu.

Eneo la mtandao wa simu za umma (za serikali) za kisasa kabisa umekuwa mara mbili zaidi katika miaka saba iliyopita, ikiwa na njia milioni 1,535,992, huku mpango mkubwa wa kupanua mfumo wa kisasa wa simu nchini humo kuwafikia watu wengi zaidi.

Historia mpya ya Saudia inafahamisha kwamba hivi sasa kuna njia zaidi ya milioni tatu za simu nchini humo huku upanuzi ukiendelea kwa kasi ya ajabu!

Mtandao wa simu za kisasa nchini humo unajumuisha miji na vijiji 6,000, huku serikali ikidhamiria kufikisha njia milioni saba kwa raia milioni 15 wa nchi hiyo.

Na huduma za Posta (barua na vifurushi) nazo zinatandawaa kwenye miji na vijiji 4,664 nchini humo huku kukiwa na makasha 220,079 na ofisi ndogo za Posta 175 nchini kote.

Huduma za haraka za Posta zimepanuka katika Taifa hilo la Kiarabu, ambapo kumeanzishwa ofisi zinazohudumia miji 37 ya Saudia na 46 ya mataifa ya nje.

Huduma za 'E-Mail' (Electronic Mail) zinahudumia nchi ishirini za nje kupitia vituo vikubwa kabisa 16 vya Kisaudia.

Na mtandao wa Tarakilishi (Telex) hivi sasa umechukua njia 30,000 katika Saudia nzima.

jarida, vitabu na matoleo mengineyo.

Idara ya maadili na utamaduni pia ina jukumu muhimu katika eneo hilo, ambapo sharti kuu la vyombo vya habari vya nchi hiyo ni kutoruka mipaka ya sheria za Kiislamu katika utendaji kazi wake.

Idara pia inadhibiti habari za nje ziendazo kinyume na maadili ya Kisaudia na kupambana na kampeni au propaganda kupitia vyombo vyake vya habari hususan magazeti, TV na Radio.

Redio ya Saudia ilianzishwa mwaka 1948 mjini Jeddah. Hivi sasa kuna vituo 22 vya Redio vinavyorusha matangazo yake kupitia mitambo mitano mikubwa na ya kisasa kabisa, karibu katika mabara yote ya ulimwengu kwa lugha 10 tofauti.

Saudi Radio hurusha matangazo yake kwa Kiarabu katika Chaneli (Channel) tatu ambazo ni General Programme, the second programme na The Call of Islam.

Kituo cha Qur'an (Qur'an Station) hurusha matangazo yake kwa Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kituruki, Kipeshia, Kiurdu, Kibengali, Kiindonesia na Kibambarba.

Katika nyakati za hija huwa na kituo cha muda kiitwachoRadio ya kukuza maarifa am rikali ina shirika lake kubwa la habari liitwalo Saud Press Agency (SPA).

SPA lina ofisi sita kubwa nje ya nchi hiyo na waandishi wa ziada (Correspondents) katika miji na majiji muhimu duniani kote.

Aidha, ina ofisi kubwa nne ndani ya nchi na waandishi wake katika miji yote ya Saudia.

Huduma za Afya

Kupitia hospitali zake baadhi ya operesheni kubwa na ngumu kabisa kama vile za moyo, figo na upandikizaji ini hufanywa bila matatizo yoyote na madaktari bingwa wa nchi hiyo.

Serikali inatoa huduma za kiwango cha juu sana za afya kwa wananchi wake chini ya madaktari wenye sifa. Na huduma hizo za afya ni bure kwa raia na wageni.

Zifuatazo ni takwimu zilizowekwa bayana na idara ya utafiti ya Dar Al Ufuq Riyadh juu ya huduma za afya nchini Saudi Arabia. Wizara ya afya ina hospitali 170, vitanda 26,878, vituo 1,702 vya afaya na madaktari 13,000, kuna wauguzi 32,229 waume kwa wake na wataalam wengine 17,195 wote wakipata malipo mazuri, marupurupu na vitendea kazi vya kisasa.

Mbali na wizara ya afya, taasisi nyingine za serikali zina jumla ya hospitali 32, vitanda 7,285, madaktari 4,721 na wataalam wengine 6,806.

Pia zipo hospitali 72 za watu binafsi,vituo 3,640 vya afya, vitanda 6,988, maduka 2,492 ya dawa, madaktari 7,580.

Aidha, kuna kliniki binafsi 685, manesi 10,216 na wataalam wengine 4,319.

Saudia yenye utaratibu wa vituo vya afya ya msingi, hospitali za umma na zile za rufaa, pia ina utaalam wa kisasa wa kupandikiza viungo.

Takwimu za karibuni za kituo cha Taifa cha matatibabu cya kupandikiza viungo zinaonesha kwamba ufalme huo umepata mafanikio makubwa katika uwanja huo.

Rekodi zinaonesha kuwa kulikuwa na operesheni tatu za kupandikiza mapafu, 49 za moyo na 23 za ini na kadhalika zikiwa zimefaulu kwa zaidi ya asilimia 80.

Aidha, Taifa hilo limeasisi mradi mkubwa kabisa wa afya uitwao King Fahd Medical City ambao ungali ukiendelea na ujenzi huko Riyadh. Lengo ni kuwa moja ya hospitali kubwa kabisa duniani kitakachotoa huduma kwa kina mama 254 kwa wakati mmoja, watoto 280 na wengineo 810. Wagonjwa wanawake hasa wenye magonjwa ya kike na wajawazito huhudumiwa na madaktari na wahudumu wenzao wanawake.Hakuna shaghalabaghala kama ya huku kwetu, madaktari wa kiume kushughulika na magonjwa ya siri ya wanawake!

Huduma nyingine za jamii

Kwa upande wa huduma nyingine muhimu za jamii nchi hiyo imejitahidi kujenga vituo kadhaa vya wasiojiweza, wazee, mayatima, watoto wadogo na kusaidia vyama 114 visivyo vya kiserikali (NGOs) vya misaada ya kibinadamu vikiwemo 20 vya kina mama.

Vyama hivyo mbali na kutoa misaada mbalimbali ya kibinadamu kwa wanajamii husika, pia vina majukumu ya kutoa taaluma chini ya usimamizi wa karibu wa Wizara ya Kazi na masuala ya kijamii.

Mwaka 1992/93 kwa mfano, zaidi ya mayatima 1,002, watoto 875, walemavu 217 na wazee 973 wamenufaika na misaada hiyo.

Aidha, serikali imetoa milioni 21 za Riali kwa familia zinazokaa na wasiojiweza ambapo watu 1,919 wamefaidika na msaada huo.

Jumla ya misaada ya kibinadamu inayopewa NGOs na serikali kuwafikishia walengwa imeongezeka toka Riali milioni nne mwaka 1976 hadi milioni 61 mwaka 1992/93.

Kwa upande wa Bima, wizara ya kazi na masuala ya jamii inajitahidi kutoa changamoto kwa NGOs hizo, kuchukua nafasi muhimu kuwasaidia wasiojiweza.

Kiwango walicholipwa walengwa kimeongezeka toka Riali milioni mbili nukta tatu mwaka 1969/70 hadi Riali milioni 108.7 mwaka 1992/93. Hilo ni sawa na ongezeko la asilimia 71.5 kwa mwaka kwa kipindi hicho chote.

Wizara hiyo pia imetoa 'pensheni' na mafao mengine kwa wasiojiweza ili kuwawezesha kupata mahitaji ya msingi na kukuza uwezo wao kiuchumi hivyo kuibadili sura ya jamii.

Kupitia Bima ya jamii, mamilioni ya Riali hutolewa kwa wahusika kumudu hali ya maisha.

Kwa upande wa bima ya Taifa (National Insurance) idadi ya pesa walizolipwa wafanyakazi waliosajiliwa imeongezeka toka 145,000 mwaka 1973 hadi milioni tatu nukta moja mwaka 1992, asilimia 90 wakiwa wafanyakazi wa sekta binafsi.

Na jumla ya taasisi zilizosajili wafanyakazi wake katika bima hiyo imeongezeka toka 1,062 mwaka 1973 hadi 15,576 mwaka 1992.

Michezo na vijana

Kwa kuzingatia nafasi ya vijana wadogo katika uongozi wa taifa la usoni, serikali ya Saudia inajitahidi kuwalea kwa kuzingatia utamaduni halisi wa nchi hiyo.

Ufalme umejitahidi kuongeza idadi ya vilabu vya michezo yote toka 53 mwaka 1975 hadi 154 mwaka 1993.

Aidha, idadi ya vyama vya michezo na kamati zake kitaifa sasa ni 21 na maofisa wakuu kabisa 13 na matawi yaliyotandawaa nchi nzima.

Ufalme umetoa zaidi ya Riali bilioni tatu kwa vyama hivyo kama ruzuku kati ya mwaka 1974 na 1993 kwa minajili ya kuendeleza michezo.

Saudia imejenga nyumba 19 kwa ajili ya jumuiya ya vijana wake ambayo ina wanachama hai 57,000.

Imeasisi kambi mbili za vijana huko Taif and Hail, hadi mwisho wa 1993 mradi ifuatayo imetekelezwa:

Vituo 15 vya kitaifa vya michezo, kumbi sita za ndani na mabwawa ya ndani ya kuogelea, vilabu 154 vya michezo, viwanja vitano vya kitaifa vya wazi, taasisi ya uongozi kwa vijana, kitengo cha tiba za asili kwa vijana, jengo kubwa la kamati ya taifa ya Olympic, majengo matatu makubwa ya huduma za ustawi kwa vijana huko Jeddah, Damman na Riyadh, vituo viwili vya michezo vya pwani (ufukweni), kiwanja cha kimataifa cha michezo cha Riyadh kikiwa na uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 80,000 na kituo cha utamaduni cha kitaifa (King Fahd Cultural Centre).

Mbali na hayo yote niliyoyaeleza kama mafanikio Saudia ina kijiji kikubwa cha sayansi na teknolojia, mabenki makubwa, mashirika ya misaada ya kimataifa na kadhalika, lakini bado haijawa makini na sera zake za mambo ya nje, hususan kuelekea Magharibi. Jambo ambalo wakosoaji wake wanapasha kwamba hiyo ni dosari itakayopelekea taifa hilo kuporomoka kimaadili na kiutamaduni.
--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org

 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook