Ulimwengu wa Kiarabu uangalie upya mwenendo wake


SEHEMU fulani ya ulimwengu wa Kiislamu imejengwa na jumuiya ya Kiarabu ambayo kwa asilimia tatu toka watu milioni 235 miaka kumi iliyopita hadi milioni 300 hivi leo. Je, wingi wao na utajiri wao una tija gani miongoni mwao pamoja na ulimwengu wa Kiislamu? Makala hii inalichambua swali hilo kwa kifupi.

UMOJA wa Waarabu umechafuliwa kwa kiwango kikubwa Umwagaji wa damu, propaganda za chuki, uhasama na tuhuma miongoni mwao vimekuwa ni vitu vya kawaida katika ulimwengu wa Kiarabu ambao miaka kadhaa iliyopita ulikuwa unaongozwa na Misri kwa idadi ya watu.

Misri ilikuwa na watu milioni 52 ikifuatiwa na Sudan ambayo ni nchi kubwa kabisa kwa eneo barani Afrika iliyokuwa na watu milioni 26 mbele ya Moroco na Algeria zilizokusanya watu 27.7 milioni kila moja.

Shirikisho la Ghuba (Gulf Co-operation Council) lililoasisiwa mwaka 1981 likikusanya nchi sita ambazo ni ni Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates), Kuwait, Oman, Qatar na Bahrain, lilimeza watu 22 milioni, Saudia peke yake ikikusanya Waarabu 15.5 milioni kati ya hao.

Iraq nayo ambayo ni moja ya nchi chache za Kiarabu zenye nguvu thabiti za kijeshi barani Asia ilikuwa na watu milioni 20 ikifuatiwa na Yemen iliyokuwa na watu milioni 12.5.

Nchi hizi na nyinginezo za Kiarabu ni miongoni mwa nchi tajiri kabisa duniani, lakini hazina sauti yoyote kubwa katika muelekeo wa siasa za ulimwengu.

Hii inatokana na sera zake ambazo kwa kiasi kikubwa zinategemea ulimwengu wa magharibi katika utekelezaji wake.

Wataalam wengi wa fani kadha wa kadha ndio wanaotoa ushauri wa mipango ya maendeleo katika sehemu kubwa ya 'bara Arabu' na hata kuitekeleza. Swali la msingi kujiuliza je, Wazungu hawa wataweza kweli kuukweza ulimwengu wa Kiarabu na 'kuzifunga tela' nchi zao za magharibi katika maendeleo ya nyanja mbalimbali muhimu hususan elimu (upande wa mitalaa) na siasa za kimataifa, utamaduni na maadili mema ulinzi pamoja na maendeleo ya kweli ya sayansi na teknolojia?

Kinachozitisha nchi za magharibi zikiongozwa na Marekani ni wimbi kubwa la wakazi wake linalomiminika katika Uislamu kwa kasi ya ajabu.

Ustaarabu wa Kiarabu umeaRIthiwa mno na utamaduni wa Kiislamu hali ambayo mara kadhaa inawapa ugumu Wazungu hawa jinsi ya kutofautisha Uarabu na Uislamu.

Wanachofanya ni kuupiga vita Uarabu kwa njia zisizo za moja kwa moja kwa upande mmoja na kuushambulia Uislamu uso kwa uso kwa upande mwingine chini ya mwavuli wa siasa kali, imani kali, ugaidi na kadhalika. Hata hivyo takwimu za Waislamu za kila mwaka katika nchi zao zingali zikiwasuta.

Italia pekee ambapo ndio makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani kwa mfano, tangu mwaka 1994 si chini ya Wataliano 10,000, husilimu kila mwaka kuingia Uislamu.

Kwa mujibu wa Kasisi Mourice Bourmance, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya mitaala ya "Uarabu na Uislamu" huko Vatican (katika ofisi ya Papa) Waislamu wageni waishio nchini humo ni zaidi ya 350,000 ukilinganisha na Mayahudi 20,000 wanaoishi Italia.

Miongoni mwao ni Wamoroko wasiopungua 95,000, Watunisia 50,000, Wasenegal 27,500 na Wamisri zaidi ya 23,500 pamoja na taasisi zao madhubuti za Kiislamu.

Kinyume chake, baadhi ya mataifa ya Kiarabu yanatekwa kidogo kidogo kuelekea magharibi kiutamaduni kwa mbalimbali kuanzia zile za kitaaluma, kisanii, michezo na hata kisayansi na teknolojia yake.

Licha ya kuwepo mataasisi makubwa ya Kiarabu kama vile Arab League lililoasisiwa mwaka 1945 linaloshughulikia masuala mbalimbali ikiwemo uchumi na maendeleo ya jamii, The Arab Authority for Investment and Development in Agriculture lililoanzishwa mwaka 1976 likiwa na makao makuu yake mjini Khartoum likishughulika na vitega uchumi na maendeleo ya kilimo, fuko la uchumi na maendeleo ya jamii (Arab Fund for Economic and Social Development) lililozinduliwa mwaka 1968, makao yake yakiwa nchini Kuwait, shirikisho la michezo la Kiarabu (Arab Sports Conferation) lililoanzishwa mwaka 1976 makao yake yakiwa Riyadh Saudia, Arab Gulf Programme of the UN Development Organization, inayoshughulikia mipango ya maendeleo ya umoja wa mataifa katika nchi za ghuba za Kiarabu iliyoanzishwa mwaka 1981, makao yake yakiwa huko Riyadh. Lakini bado ulimwengu wa Kiarabu unaburuzwa na nchi za magharibi katika masuala mbalimbali ya kimataifa!

Mataasisi mengine makubwa ya Kiarabu na Kiislamu yaliyoasisiwa na kuangozwa na nchi za Kiarabu ni pamoja na Arab Bureua for Education for Gulf States lenye makao yake makuu huko Riyadh likishughulika na masuala ya elimu katika nchi za Ghuba za Kiarabu.

Pia kuna Arab Towns Organization lililoanzishwa mwaka 1967 kushughulikia masuala mbalimbali yanayoihusu miji ya ulimwengu wa Kiarabu. Umoja huo una makao yake makuu nchini Kuwait.

Ipo Ecomic and Social Council for West Asia yenye makao yake makuu mjini Baghdad, Irag iliyoanzishwa mwaka 1974.

Aidha, kuna Gulf Organization for Industrial Consulting yenye makao yake nchini Qatar.

Halikadhalika kuna International Association of Islamic Banks yenye amkao yake makuu Jeddah Saudia iliyoanzishwa mwaka 1977. Na The Islamic Institute for Defence Technology iliyoanzishwa mwaka 1978 ikishughulikia teknolojia ya ulinzi katia ulimwengu wa Kiislamu ikiwa na makao yake makuu huko London, Uingereza.

Mengine ni World Muslim Congress na the Muslim World League iliyoanzishwa mwaka 1962 ikiwa na makao yake makuu Jijini Makkah Al Mukarama pamoja na Africa Muslim Agency lenye makao yake makuu nchini Kuwait na kadhalika.

Mbali na mashirika hayo na mengine nisiyoyataja bado Waislamu wa nchi mbalimbali wanateseka juu ya kadhia kadha wa kadha ama bila ya msaada wenye kufaa au wakisaidiwa na nchi chache au mashirika machache tu ya ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu.

Tuangalie Kossovo, Kashmir, Chechnya, Philipines, Misri, Algeria, Sudan, Somalia, Sahara Magharibi, Kisiwa cha Komoro, Afghanistan na kadhalika. Ni hatua gani za dhati na za msingi kabisa ambazo jumuiya ya Kiarabu na ulimwengu wa Kiislamu kwa pamoja umechukua kumaliza matatizo ya maeneo hayo?

Kuhusu masuala ya kiuchumi, ulimwengu wa Kiarabu wenye nguvu kubwa za kiuchumi kwa sehemu kubwa umeangalia vipi sura ya uchumi katika ulimwengu wa Kiislamu? Je, zina uhusiano gani wa kiuchumi na Waislamu wa nchi zisizokuwa za Kiislamu kama Tanzania?

Tukiitupia jicho Saudia kwa mfano, imeanzisha kile kiitwacho Saudi-American ambapo makampuni makubwa ya kimagharibi (Amerika) kama vile "Standard Oil of Calfonia" yamepewa nafasi katika eneo la mashariki ya Ufalme huo kuchimba mafuta kwa mapana na marefu yake!

Mwaka 1945, mfalme wa Saudia wakati huo Abdulaziz katika ziara yake ya kwanza nje ya nchi alikutana na Rais wa Amerika zama hizo Franklin D. Roosevelt huko Suez ambapo suala la mahusiano ya kidiplomasia lilijadiliwa pamoja na mahusiano na ushirikiano wa kibiashara.

Ni katika msingi huo kukaasisiwa kamati ya Kisaudi na Kiamerika inayoshughulikia ushirikiano wa kiuchumi (American-Saudi Common Committee for Economic Co-operation) mwaka 1974; pamoja na hayo kamati hiyo ilishughulikia mpango wa 'kuipa teknolojia' Saud Arabia toka Marekani!

Uhusiano huo pia ulikubaliana kupambana vilivyo na mianya yote ya kisiasa, kimawazo na kidini itakayohatarisha 'utulivu' wa mashariki ya kati!

Hali ambao imeifanya Marekani kuiona Saudia kama jiwe lake la pembeni katika ujenzi wa himaya yake ndani ya ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu kwa ujumla.

Uhusiano wa kijeshi na kiuchumi pia unathibitisha ukweli huu kiuchumi kwa mfano, hadi mwaka 1982, Saudia ilikuwa nchi ya sita duniani kuwa 'soko kuu' la bidhaa za Marekani, hali ambayo imezidi maradufu hivi sasa.

Bidhaa za Amerika huko Saudia zinabeba zaidi ya asilimia 44 ya bidhaa zote zitokazo nje.

Mwaka 1982 pekee Amerika ilijikusanyia dola bilioni tisa ukilinganisha na dola milioni 442 mwaka 1977 kutokana na bidhaa zake katika soko la Saudia.

Wakati yote hayo yakifanywa na taifa hilo la Kiarabu na la Waislamu, uongozi wake (Ufalme) umesahau kabisa nafasi yake muhimu katika ulimwengu wa Kiarabu na hata wa Kiislamu.

Umesahau kuwa Marekani ni Uyahudi na Uyahudi ni Marekani. Na kusahau au kutoangalia jinsi Mayahudi wanavyowakandamiza Wapalestina na Walebanon kwa miongo kadhaa sasa na hata kukalia ardhi ya Syria, Lebanon na Palestina.

Wamesahau ukina na 'ukiriri' wa Amerika katika kuupiga vita Uislamu kwa hali na mali.

Hali hiyo haishii kwa Saudia tu, bali nchi kadhaa za Kiarabu ambazo zinazikumbatia nchi za magharibi bila kuangalia athari za mahusiano hayo kwa utamaduni, maadili, uchumi, ulinzi na usalama na maendeleo yake kwa nyanja zote kiujumla.

Hivyo, wingi wao na utajiri wao wa maliasili umegeuzwa mafuta ya kuwakaangia wenyewe na nchi hizi za magharibi, halikadhalika wakiwadumaza na kuwapumbaza kwa kuwatengenezea anasa kadha wa kadha na agenda chungu nzima za kuwashughulisha.

Umefika wakati ulimwengu wa Kiarabu kuangalia upya mwenendo wake na mahusiano yake na ulimwengu wa Kiislamu ili kukusanya nguvu za pamoja kupambana na mfumo wowote wa maisha unaomfanya mwanadamu kuwa mnyama zaidi hapa duniani, badala ya kuwa mtu bora zaidi.
--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org

 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook