IMEELEZWA kuwa iliyokuwa shule ya Muslim Moshi wamepewa dhehebu la Kilokole wafanye shule binafsi ya msingi.
Dhehebu hilo imedaiwa limepatiwa misaada toka mashirika ya Kikristo ya Sweden.
Mwenyekiti wa Kamati inayofuatilia mgogoro wa shule hiyo, Bw. Ansaar, amesema wasemaji wa shule wamekuwa wakikwepa kusema lolote juu ya kuporwa shule ya Mwenge.
Shule hiyo ilijengwa na Waislamu miaka ya 1950, chini ya Chama chao Muslim Association of Moshi and Pare Districts.
Bw, Ansaar amesema kamati yake inakusudia kumuona Mkuu wa Mkoa baada ya Mkuu wa shule hiyo Mama Miriam Urio na Afisa Elimu kukataa kabisa kujibu lolote.
Imeelezwa kwamba, barua zinazotolewa na Wizara kuhalalisha shule hiyo kuwa "English Medium School" ni za hila.
"Barua ya Bwana Ndeki ni kama tu ule Waraka wa Tabitha Siwale. Wana agenda yao ya siri , sisi wanatufanya wajinga", amesema Bw. Khalifah Mushi alipoongea na AN-NUUR mjini Moshi juzi.
Akifafanua alisema "Tabitha alitoa Waraka wa kutozitambua seminari kuwa ni shule ili akwamishe seminari za Kiislamu na hii barua ya Kamishna wa Elimu Bw. Ndeki imeficha uporaji kwa kisingizio cha ridhaa na maombi ya wananchi. Serikali inaongopa ili kuwadhulumu Waislamu", amesema.
"Kama hakuna agenda ya siri mbona jambo hili lifanywe kwa usiri huku wananchi wakisingiziwa kuamua, na wakuu wa elimu mkoani hapa wadai ni maagizo toka ngazi za juu, kila wanapotakiwa watoe ufafanuzi", amehoji.
Katika hatua nyingine ya mgogoro huo, Waislamu walikutana kujadili hatma ya shule hiyo.
Wazazi na walezi wa Mtaa wa Bondeni walikanusha kuwepo kikao chochote cha wananchi kujadili suala la shule hiyo kuwa "English Medium School".
Hoja hiyo ilitolewa baada ya kusomwa barua ya Kamishna wa Elimu inayodai kuwepo kwa kikao hicho.
Baadhi ya wazungumzaji katika mkutano huo, walieleza masikitiko yao jinsi Waislamu wanavyoburuzwa na serikali.
Wamesema, inasikitisha wakati Wakristo wanarejeshewa baadhi ya majengo ya shule zilizokuwa zimetaifishwa, za Waislamu wanapewa watu wengine bila hata wao wenyewe kupewa taarifa.
Akitoa nasaha zake katika kikao hicho, Ustaadh Issa Omar Malecela alisema, amani haiwezi kuwepo iwapo uhai, heshima na mali za watu hazitalindwa.
Amesema migongano na mapambano katika jamii hayawezi kuondoka iwapo dhulma itaendelea kuwepo.
Akielezea historia ya shule hiyo, mkongwe wa EAMWS Mzee Ali Omar amesema harakati za ujenzi wa shule za Muslim zilianza mwaka 1946.
Amesema shule za awali kujengwa chini ya Muslim Association of Moshi and Pare Districts zilikuwa Machame, Kirongwe, Msangeni na Moshi (Mwenge).
Amesema awali walikuwa wamekatazwa na serikali ya kikoloni kuanzisha shule mpaka walipotishia kutolipa kodi.
Mzee Ali amesema, maadhali shule ya Moshi Muslim imejengwa kwa michango na nguvu za Waislamu wa Mkoa wa Kilimanjaro ni lazima wote waarifiwe na wasimame imara kuidai shule yao.
Katika mkutano huo, akinamama walitoa mchango wa shilingi laki mbili kuendeleza mapambano ya kudai haki ya Waislamu.
Aidha, lilipitishwa azimio kuwa kuanzia sasa sherehe na hafla zote za Kiislamu zitakuwa zikifanyika katika viwanja vya shule ya Mwenge.
Maazimio mengine muhimu yalikuwa kufungua kesi mahakamani, kulipeleka suala hili kwa Waislamu na kuanza taratibu za kudai kurejeshewa shule hiyo.
Mkutano wa Jumapili pamoja na kuhudhuriwa
na wawakilishi kutoka wilaya za mkoa, walihudhuria wajumbe toka Mombasa
ambao waliwakilisha stakabadhi za michango ya Waislamu wa Mombasa wakati
wa ujenzi wa shule hiyo.

Mkutano wa Jumapili pamoja na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka wilaya za mkoa, walihudhuria wajumbe toka Mombasa ambao waliwakilisha stakabadhi za michango ya Waislamu wa Mombasa wakati wa ujenzi wa shule hiyo.
WANAFUNZI wa darasa la saba shule ya msingi Mlandege, Iringa wamelazimika kuhudhuria masomo siku ya Idd kutokana na kile walimu walichodai kuwa kutoitambua sikukuu hiyo.
Baadhi ya wazazi waliofika shuleni hapo machi 20, mwaka huu kuulizia suala hilo waliambiwa kuwa walimu wahusika wamefanya hivyo ili kuwaandaa vyema vijana wao na mitihani ya mwisho
Hata hivyo, ilifahamika kuwa wanafunzi katika shule hiyo walipewa ruhusa siku ya ibada ya Kikristo ambayo hutambulika kwa jina la "Siku ya Majivu".
Akitetea msimamo wa shule yake, Mwalimu mkuu wa shule hiyo alisema iweje wazazi waifuate shule hiyo pekee ilhali shule nyingine zinafanya hivyo pia.
Aliitaja shule ya Mlangali kuwa mojawapo ya shule zenye utaratibu huo wa kusomesha wanafunzi siku za Idd.
Taarifa ambazo gazeti hili halikuweza kuzithibitisha zimefahamisha kuwa karibu wanafunzi wa shule saba walihudhuria masomo siku ya Idd.
Hata hivyo baadhi ya walimu wakuu walikanusha kuwepo kwa hali hiyo katika shule zao.
IMEELEZWA kuwa chanzo cha vurugu kati ya wafanyabiashara na polisi Manzese ni baadhi ya viongozi wa CCM na wa serikali ya mtaa wa Midizini.
Wakiongea na mwandishi wa habari hizi muda mfupi baada ya vurugu hizo, walisema viongozi hao wanataka kuwahamisha ili waweke watu wao.
"Viongozi hao hawafai utendaji wao wa kazi wanafanya kinjaa kuna watu wanahitaji maeneo haya", alisema Mzee Omari.
Aidha, walieleza kuwa wanashangazwa na viongozi wa serikali kujifanya wanawajali wakati wanapohitaji kura zao. Wamesema, kipindi cha uchaguzi wa mitaa ulipokaribia walifika viongozi wa juu maeneno hayo ya Manzese na kuwaeleza kuwa hawatabomolewa vibanda vyao waendelee na biashara.
"Alikuja Mkuu wa Mkoa hapa akasema tusibomolewe, pia walifungulia tawi lao hapa wakatuambia tusihame hapa. Pia Makamu wa Rais Dk. Omar alieleza hivyo hivyo, leo tunashangaa tunabomolewa. Kumbe hizo zilikuwa ni kampeni tu", alisema Bw. Bakari Abeid.
Wafanyabiashara hao wameeleza kuwa, wao wameamua kujituma kujitafutia riziki halali, lakini wanabughudhiwa. "Kama serikali inaona kuna njia ya kutupatia ajira itupatie. Sisi biashara tuliyobuni ndio hii ambayo inatusaidia", alisema Eddy John, mfanyabiashara wa Mitumba.
Wameeleza kuwa hasara waliyoipata hapo ni kubwa ambayo haiwezi kufidika. "Leo vitu vingi vimepotea, pesa zetu, nguo za biashara na mbao kuvunjwavunjwa kama sio dhuluma ni nini?" alisema kwa masikitiko Bw. Ramadhani Kambangwa.
Mapema wiki hii askari polisi wa Tume ya Jiji wakiwa na silaha walipambana na wananchi maeneo ya Manzese kwa lengo la kubomoa vibanda vyao vya biashara, jambo ambalo wafanyabiashara hao hawakuafiki, hivyo kusababisha mashambulizi kwa kutumia mawe.
Wafanyabiashara waliwasha moto barabarani, jambo lililosababisha barabara ya Morogoro hapo Manzese kufungwa kwa muda wa saa mbili hivi na kusababisha msururu wa magari.
Katika vurugu hizo polisi walitumia mabomu ya machozi kutuliza ghasia hizo na kupiga risasi hewani. Jambo ambalo halikuwastua Wamachinga hao.
Vurugu hizo zilitulizwa na Kamanda mmoja wa
ngazi ya juu wa polisi mkoa ambaye alisitisha uvunjaji wa mabanda na kuwaruhusu
wafanyabiashara hao waendelee na shughuli zao.
--
![]()
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |