Aliwataka watakaoipigia CCM kura wanyooshe mikono. Wakanyoosha wenye sare za kijani. Akahoji, nani atavipigia hivi vyama vyenye majina ya ajabu ajabu, wakaonyoosha woote, mikono miwili miwili.
Mhe. Rais Mkapa akabaki kucheka.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa Mhe. Rais alipofungua Tawi la CCM Shinyanga Guest House.
Katika nyumba hiyo iliyopo mtaa wa Lumumba, ipo ofisi ya mfanyabiashara maarufu mjini hapa.
Mfanyabiashara huyo alikuwa akifungua tawi la CCM mbele ya ofisi yake.
Ilikuwa ni mchana wa Jumamosi Machi 25, Rais akiwa mgeni rasmi.
Mhe. Rais alifungua tawi lingine la CCM kule Ilemela.
Katika kipindi cha wiki mbili sasa, mji wa Mwanza umekuwa na harakati nyingi za kisiasa.
Mawaziri na Wabunge wote wa kanda ya ziwa pamoja na wakuu wa mikoa na wilaya za kanda hiyo wapo hapa wakijadili mambo ya ushirika.
Hata hivyo, wachunguzi wa mambo ya kisiasa wamedai kuwa fursa hiyo inatumika kupiga siasa za CCM, na kuandaa mazingira ya kupata kura.
Pamoja na ufunguzi wa matawi ya CCM, hali
ya hewa imekuwa ikisafishwa kuonesha serikali inawajali wakulima.
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |