Na Ahmed Hussein
NIMEKUWA nikifuatilia kwa makini makala za maendeleo ya Saud Arabia. Kwa kweli nimevutiwa na hatua za maendeleo zinazopigwa na nchi hiyo katika nyanja za elimu na uchumi.
Hapokabla, Waarabu wa Saudia walikuwa wakidharauliwa sana kwa 'kutothamini elimu", walishutumiwa kwa kuendekeza mali na "elimu ya dini".
Hata hapa nchini zilivurumishwa propaganda miaka ya nyuma kuwa hali duni ya Waislamu kielimu ilisababishwa na Waarabu ambao, ilidaiwa, walifundisha "elimu akhera" badala ya "elimu dunia". Na kwamba Waislamu wakaendekeza madrasa badala ya kwenda shule. Na kwamba nchi za Kiarabu badala ya kuwaletea Waislamu misaada ya kitaalamu ziliwaletea tende.
Propaganda zote hizi zililenga kuhalalisha dhuluma zilizofanywa na serikali ya kikoloni na ile ya kizalendo dhidi ya Waislamu ikiwa ni pamoja na kuvunjiwa jumuiya yao ya EAMWS.
Lakini tokea washike madaraka wenzetu "waliothamini elimu dunia" hatuoni wanachofanya zaidi ya kuiporomosha nchi kielimu, kiuchumi na kimaadili.
Walioshika usukani awali waliifkisha nchi mahala pa kukosa hata dawa ya mbu na mswaki duniani. Alipoingia "Mwalimu wa Madrasa" kama alivyoitwa na "wasomi" nchi ikang'ara kwa miaka kumi tu.
Kuingia tena "wanadiplomasia" nchi imefika mahala ambapo ukisema inaongozwa na wasomi basi wazi unaitukana elimu. Jinsi mambo yanavyoendeshwa shaghalabagala hata tuliokaa madrasa tunaona basi kama ni hivyo hata sisi tunaweza. Japo wenzetu wanasema wanatuchagua kwa kufumba macho! Kipi kitamshawishi mtu wa kawaida aamini kuwa nchi inaendeshwa na "wasomi".
Sasa wakati "waliopelekwa kwenye shule za elimu dunia" wanahangaika kupambana na umaskini uliokithiri, "wale wasiothamini elimu dunia" wako Saudi Arabia wanapiga kasi ya ajabu katika maeneo yote muhimu.
Miaka arobaini ya uhuru wa Taifa la Tanzania lina vyuo vikuu viwili tu, Kweli hapa elimu inathaminiwa? Takwimu za taasisi za elimu Saudi Arabia kwa kipindi kifupi sana zinaonesha ni kiasi gani Waarabu hao wanavyothamini elimu.
Ukiangalia uchumi wao halafu uulinganishe na wa kwetu, kwa kweli utawadhalilisha "waliosoma", ukiambwa mafuta ni uti wa mgongo wa Saudi Arabia unakubali kwa asilimia mia moja lakini ukiambiwa kilimo ni uti wa mgongo wa Tanzania unakataa kwa asilimia mia moja!
Juzi tu hapa, watalaamu wa nje, baada ya kukifanyia tathmini kilimo chetu, wametamka bayana kuwa hakuna Mtanzania anayestahiki kuitwa mkulima.
Leo hii "wakubwa" wetu ndio wanakwenda nje kujifunza utafiti wa kilimo!
Saudi Arabia haina rasilimali nyingi kama sisi, ila wameitumia vema rasilimali yao ya mafuta. Eti wengine wanasema wenzetu wameendelea kwa sababu ya visima vya mafuta.
Hicho ni kisingizio tu. Kama sisi Watanzania tungetokea kuishi Saudi Arabia na Wasaudia kuishi Tanzania, basi sisi tungekuwa maskini mara ishirini zaidi kuliko tulivyo sasa na Wasaudia wangelikuwa matajiri mara hamsini zaidi kuliko walivyo sasa.
Hiyo ni kwa sababu, kama sisi tumeshindwa kuendelea licha ya rasilimali chungu nzima tulizonazo, tungewezaje kuendelea kwa rasilimali ya aina moja?
Kama tumekuwa masikini hata kufa njaa katika ardhi yenye rutuba, mabonde na madini "bwerere", tungewezaje kuwa matajiri na kusalimika na njaa jangwani penye rasilimali chache? Tumshukuru Mungu kwa hekima zake. Ametuweka huku walau kuna chunga, kisamvu, mlenda na matembele yanayotunusuru na njaa ambayo imekwishagharimu roho za wana Kilwa na Wanaifakara.
Kwa upande mwingine, kama wenzetu wamekuwa matajiri jangwani, wangekuwa huku sijui tungewaitaje. Mwarabu mmoja alipoitembelea Tanzania alishindwa kuamini kuwa Tanzania ni moja ya nchi masikini kabisa duniani. Kilichomfanya astaajabu ni baadhi tu ya rasilimali alizoziona. Bwana huyo akakataa kuwa Tanzania ni masikini.
Nakubaliana na mgeni huyo kuwa Tanzania sio masikini kijiografia bali watu wake ndio masikini, na labda hasara tuliyoipata ni ile ya kukosa siasa bora kama waliyonao wenzetu ambayo imeweza kuzipatia nchi zao maendeleo kwa rasilimali chache tu.
Kama Saudia ingepata siasa kama za CCM, basi jangwa lingejaa makaburi ya wahanga wa njaa na Maka na Madina zingefurika ombaomba wenye vibakuli na vikopo vya kuomba msaada kwa Mahujaji.
Na kama Tanzania ingepata siasa kama ile ya Saudia basi Morogoro pekee ingetosha kufuta umaskini wa nchi nzima. Kila mkoa ungepata maendeleo kwa rasilimali zake.
Kwa jinsi makala ya uchumi wa Saudi Arabia inavyosomeka sambamba na makala ya ufukara wa mojawapo ya mikoa ya Tanzania, wananchi tunapata uchungu mkubwa sana. Saudia haipo angani, vipi wenzetu wawe na maendeleo makubwa kupindukia na sisi tuwe na umasikini mkubwa kupindukia.
Wakati umefika kwa wananchi kuwaondoa madarakani
"wachawi" wetu ambao sasa wanakamatana wizi wa mapesa ya wakulima katika
vyama vya ushirika
--
![]()
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |