Upandaji bei ya petroli:
Serikali 'Mumiani'

SERIKALI imekuwa ikiwaumiza wananchi kutokana na kodi kubwa inayotoza bidhaa mbalimbali za petroli.

Hali hiyo imefananishwa na 'umumiani' dhidi ya raia. "Hii haina tofauti na vitendo vya IMF kuzikamua nchi changa. Serikali imekuwa kama mumiani anayetunyonya damu bila kutupa lishe", amesema mfanya biashara mmoja mwenye daladala.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa, kodi inayotozwa petroli [super] na dizeli ni zaidi ya asilimia mia moja ya bei ya mafuta hayo yanapoingia nchini.

Kwa mafuta yaliyopo kwenye soko sasa hivi, uchunguzi umebaini kuwa bei yake ilikuwa kiasi cha Sh.230 [super] na Sh.210 dizeli kwa lita yalipoingizwa nchini.

Hiyo ni bei ya kuyanunua na kuyasafirisha hadi Dar es Salaam.

Mafuta hayo ndiyo mlaji leo anauziwa kwa wastani wa Sh.560 'super' na 510 kwa dizeli.

Uchunguzi unaonyesha kuwa mafuta hayo hutozwa kodi za aina saba.

'Import duty' asilimia tano,ushuru wa shirika la mafuta [TPDC margin) takriban Sh.16 kwa lita na kodi ya Tipper Sh.11.40. Gharama na kodi nyingine ni mfuko wa nishati [Energy Fund] Sh. 20 kwa lita, ushuru wa barabara [road tall] Sh.70 kwa lita na 'Excise duty' Sh.64.30 kwa super na 16.90 kwa dizeli.

Kodi nyingine ni ile ijulikanayo kama 'Wind fall profit/ tax' ambayo ni Sh.98.50 kwa super na 120.20 kwa dizeli.

Kodi na michango yote hiyo hufanya mafuta yaliyoingizwa kwa Sh.230 na 210 yauzwe kwa Sh. 510 [super] na 464 [Dizeli] kwa bei ya jumla kwa makampuni ya Total, BP, Oilcom,Gapco na mengineyo.

Awali 'wind fall profit' ni faida ambayo serikali ilikuwa inachukua ili kudhibiti mfumuko wa bei ya mafuta.

Kwa hiyo faida hii ilikuwa ikiongezeka na kupungua kulingana na bei ya mafuta katika soko la dunia.

Faida hii ndiyo iliyokuwa inaiwezesha serikali kudhibiti mafuta yasipande wakati ilipokuwa inadhibiti uagizaji wa mafuta.

Linalowashangaza wengi ni kuwa leo wakati mafuta ni biashara huria, na serikali haihusiki tena na upangaji wa bei bado inachukua "wind fall profit". Na imeiwekea kiwango maalum. [soma makala uk.12]
--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org

 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook