Ijue nchi ya Yemen

YEMEN ni miongoni mwa nchi za Kiarabu ambazo zina mahusiano ya karibu na nchi yetu.Uhusiano huu una historia ndefu kabla hata kuingia kwa wakoloni wa Kireno na Kijerumani.Zama hizo Waayemeni waliingia Pwani ya Afrika ya Mashariki kufanya biashara.Miji mingi ya pwani ikiwemo Malindi, Mombasa,Tanga,Dar es Salaam na Kilwa ilijengwa na wageni wa kiarabu wakiwamo wale wa kutoka Yemen.

LAKINI ukiacha uhusiano wa kibishara,Yemen ina mchango mkubwa katika kuingia uislam Afrika ya Mashariki.Wafanya biashara waliotoka Yemen kila walipo weka makazi kwa ajili ya shughuli zao za kibiashara walijenga misikiti wakawasilimisha wenyeji na kuwafudisha uislam. Historia inaonyesha kuwa awali waarabu wa Yemen wengi walishukia Mombasa na wa Oman walishukia Unguja.

Hata hivyo ukizungumzia Waarabu katika Afrika ya Mashariki,basi waliowengi ni waarabu kutoka Yemen.

Katika historia ya uislamu,Hadharamout inatajwa kama moja ya miji mashuhuri iliyotoa masheikh na masharifu wengi ambao walitoa mchango mkubwa katika kueneza uislamu Afrika ya Mashariki.

Yemen ya leo sio Yemen ya jana.Awali zilikuwepo Yemen mbili,ile ya Kaskazini na Kusini.Ni miaka kumi tu iliyopita ambapo Yemen zote mbili ziliungana kufanya Wah'da chini ya Rais A'lly A'bdallah Swaleh,ambaye anaendelea kuiongoza nchi hiyo mpaka leo

Upande wa kaskazini Yemen inapakana na Saudia Arabia,wakati kusini inapakana na Bahahari ya Arabia.Mashariki inapakana na Oman,Magharibi ikiwemo Red Sea .

Ikiwa na kilometa za eneo 555,000, Yemen ina watu wapatao millioni 15.Pamoja na shughuli za uchimbaji wa mafuta,wananchi wa Yemen ni wafanya biashara,wavuvi,wafugaji na wakulima. Eneo lifaalo kwa kilimo ni kiasi cha hekta 1,052,783.

Kwa mujibu wa takwimu za 1994,Yemen huzalisha zaidi ya tani 39,837 za nyama kwa mwaka,maziwa tani 150,498 ,nyama ya kuku tani 28116 na mayai milioni 315.

Wanyama wanaofugwa kwa wingi ni ngamia,mbuzi,kondoo na ng'ombe kwa uchache.

Kilimo si sekta ya kutegemewa sana kwa vile ardhi imejaa majabali na eneo kubwa likiwa ni jangwa.Mitende ndio zao maarufu zaidi.Hata hivyo yapo mazao mengine kama ngano, mtama ,uwele, viazi,vitunguu, ndizi, pamba na baadhi ya matunda.

Kwa upande wa viwanda,uchimbaji na usafishaji wa mafuta ndio shughuli kubwa zaidi.Aidha vipo viwanda vya nguo,saruji na vya bidhaa za madini kama bati.

Yemen ina Vyuo Vikuu vikubwa viwili ambavyo ni Sanaa na Aden.

Chuo kikuu cha Aden kina vitivyo 6 vikiwa na wanafunzi zaidi ya 9063 wakati kile cha Sanaa kina vitivyo 8 na wanafunzi zaidi ya 70913.


Maendeleo ya Elimu Saudi Arabia

TAKWIMU za serikali zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 1970 na 1995 idadi ya mashule imeongezeka toka 3283 hadi 22,000 huku idadi ya wanafunzi ikiongezeka toka 600,000 hadi milioni 4.

Katika kiwango cha elimu ya Chuo Kikuu, idadi ya wanafunzi imeongezeka toka 8000 hadi 185,000. Hiyo ni mbali na ongezeko la wanafunzi katika vyuo vya ufundi ambalo ni 29,000 toka 840.

Kufikia mwaka 1985, shule zilikuwa zikifunguliwa kwa wastani wa shule moja kila siku. Hivi sasa ongezeko ni wastani wa vyuo/shule tatu kila baada ya siku mbili.

Kutokana na upanuzi huo, bajeti ya elimu katika Saudia ni takriban asilimia thelathini (30%) ya bajeti ya mwaka.

Elimu katika viwango vyote ni bure ambapo serikali hutoa pia posho ya kujikimu kwa wanafunzi walio vyuoni.

Kutokana na juhudi hizi, kufikia mwaka 1996 Saudia ulitunukiwa tunzo na UNESCO kwa juhudi zake za kufuta ujinga wa kutojua kusoma na kuandika.

Saudi Arabia ilifungua Chuo Kikuu chake cha kwanza mwaka 1957 - The King Saud University kilichopo Riyadh. Hivi sasa Chuo hicho kimepanuliwa na kuwa kama mji mdogo wa wasomi. Idadi ya wanafunzi katika chuo hicho ni zaidi ya wanafunzi 40,000 kikiwa na vitivyo (Fuculties) 17.

Vitivyo hivyo ni Sayansi za jamii, sayansi, uongozi, kilimo, uganga/udaktari (medicine), ualimu, utaalamu wa meno (Dentisty) na Support Medical Science.

Vitivo vingine ni Uhandisi (Engineering), Computer Science and Data, Architecture and Planning, Uchumi, Pharmacology, lugha na kadhalika.

Vyuo vikuu vingine ni Chuo kikuu cha Mfalme Abdul Aziz Jeddah chenye vitivo tisa; Chuo Kikuu cha King Fahd Petroleum and Minerals kilichopo Dhahrran chenye vitivyo 6; Chuo Kikuu cha Imam Mohammed Ibn Saud chenye vitivo 10 na Chuo Kikuu cha Mfalme Faisal chenye vitivo 6.

Vingine ni Chuo Kikuu cha Madinnah al Munawwarah, Umm Al-Qura (Makkah) na Chuo Kikuu cha Mfalme Khalid (Abha).

Pamoja na elimu ya Chuo Kikuu, vipo vyuo vinavyotoa mafunzo ya ufundi katika kiwango cha kawaida. Viko vyuo 7 muhimu zaidi ambavyo vipo katika miji ya Riyadh, Jeddah, Dammam, Al-Madinnah, Al Munawwarah, Taif, Hofuf na Abha.

Mafunzo yanayotolewa katika vyuo hivyo ni ufundi mashine wa ujumla (general mechanics), umeme, ufundi magari, uhandisi ujenzi na electronics.

Wanafunzi pamoja na kusomeshwa bure, hupewa chakula, malazi, vifaa vyote, hupewa pia mishahara muda wote wanaosoma.
--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org

 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook