"KUHATARISHA amani ya nchi", imeelezwa kuwa ni usemi umekuwa ukitumika kuzuia juhudi za kuleta haki na usawa nchini.
Hiyo imeelezwa kuwa mbinu iliyorithiwa toka zama za Firauni alipowatia utumwani Wayahudi.
Akitoa waadhi baada ya swala ya Ijumaa Msikiti wa Kibo Jjijini, Ustadh mmoja alisema, Firauni alipokabiliwa na Mussa aache uovu, alimsingizia uchawi, akasema:
"Hakika huyu ni mchawi ajuaye (uchawi vyema). Anataka kukutoeni katika ardhi yenu". [7:109-110]
Alinukuu aya hiyo na kusema, leo watu wakidai usawa na haki wataitwa siasa kali na kudaiwa kuwa wanahatarisha amani.
"Amani gani inahatarishwa kwa mtu kudai haki, jamani hata tukionewa tusiseme?" alihoji Ustadh huyo ambaye mwandishi hakuweza kupata jina lake.
Ni siasa zile zile za zama za Firauni, kuzuia haki katika jamii, alisema Ustadh na kuwataka Waislamu zisiwashughulishe.
Amesema, mtu akishatamka shahada amechukua ahadi ya kusimamisha haki.
Wakati huo huo, Waislamu wametakiwa wajiulize wameridhika na nafasi yao katika jamii.
"Je, mmeridhika wengi wenu kuwa wapagazi na wakwezi? mmeridhika kuwa wengi wenu ni wapika chai maofisini? Je, mmeridhika kuwa madereva mnaotumwa na Wakurugenzi na Mameneja kwenda sokoni na kuwapeleka vilabuni kulewa"? amehoji Imamu wa Msikiti huo baada ya nasaha za Ustadh.
Alisema, walionufaishwa katika nchi hii (Wakatoliki), wanapiga kielele kuwa viongozi hawafai. Akahoji vipi wale waliofanywa wengi wao wawe wapagazi na wakwezi! Aliwataka wasome gazeti moja la kila wiki lililochapisha habari kuwa Maaskofu Katoliki wanasema viongozi waliopo hawafai.
Hata hivyo aliwataka waichukue kauli hiyo ya Maaskofu kwa tahadhari.
"Je, sasa wanataka haki na usawa, au wanaona fursa wanazopewa na serikali
hazitoshi", alihoji.
--
![]()
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |