Sherehe za Mei Mosi:
Lipumba kuhutubia wafanyakazi Starlight


SERA za chama cha CUF juu ya wafanyakazi zinatarajiwa kuelezwa Mei Mosi katika ukumbi wa Starlight.

Mwenyekiti wa Chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba, siku hiyo ataongea na wafanyakazi na wananchi kwa ujumla.

Taarifa ya chama hicho imesema, mkutano huo utaanza saa 9 mchana.

Wakati huo huo, chama cha CUF kimesema, CCM imekataa kutekeleza kipengele muhimu katika muafaka.

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya IPC, Bw. Muhunzi amesema, kiini cha mgogoro wa Zanzibar ni matokeo ya uchaguzi 1995.

Amesema, CUF iliituhumu Tume ya Uchaguzi kutokutenda haki. Ndio maana katika muafaka kikawepo kipengele cha kuirekebisha Tume.

Bwana Muhunzi amesema, CCM imezingatia tu idadi ya wajumbe, ikaacha suala la msingi. Suala hilo amesema, ni namna ya kuwapata wajumbe hao.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi mjini Tanga hivi karibuni, Bw. Muhunzi amesema, kwa msimamo huo wa CCM wa kuwa na Tume wanayoidhibiti ndio maana wamesema mwaka huu hakuna sra ya "hewala Bwana".

Katika tukio jingne, serikali ya Muungano na ile ya Zanzibar zimetakiwa zifanye hima kutatua mgogoro wa kisiasa Zanzibar.

Ujumbe wa Wabunge kutoka Ujerumani wameeleza kutoridhishwa kwao na kuwekwa ndani kwa muda mrefu watuhumiwa wa kesi ya uhaini.

Wametaka watuhumiwa hao waachiliwe.
--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org

 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook