Vijana watakiwa kuondoa maovu

AMIR wa Waislamu, Sheikh Juma Mbukuzi Salim amewataka vijana wafanye juhudi kuondoa dhulma na maovu yaliyotapakaa katika jamii kwa kutaraji radhi za Allah (s.w.).

Sheikh Mbukuzi ameyasema hayo Masjid Aqswa (Kwa Njani) Mburahati Jumapili Aprili 23, mwaka huu alipokuwa akizungumza na vijana na Waislamu kwa ujumla katika mkutano ulioandaliwa na vijana wa Masjid Aqswa kwa kushirikiana na Jumuiya ya Waislamu Masjid Hijaaz (Jamaatul Ikihitimanyl Islamiyya).

Sheikh Mbukuzi amesema, jukumu la Muislamu sio kuswali tu, bali kuondoa dhulma na maovu katika jamii ni jukumu kubwa kwa Muislamu.

"Kuingia Msikitini mara tano kwa siku maana yake ni kuwa kila unapoingia Msikitini unakusanya nguvu mpya ya kupambana na dhulma na maovu nje ya Msikiti. Kwa maana hiyo Uislamu uko nje ya Msikiti", amesema Sheikh Mbukuzi.

Kutokana na hali hiyo, Sheikh Mbukuzi amesema, vijana ni budi wafanye juhudi kubwa kuhakikisha wanaondoa dhulma na maovu katika jamii.

"Piganieni kuondoa dhulma na maovu ili mpate radhi za Allah (s.w.) na jamii iweze kuishi katika mazingira ya maadili mema, msipofanya hivyo mtakuwa hamkufanya kazi aliyowatuma Mwenyezi Mungu (s.w.), amesema.

Sheikh Mbukuzi amesema, jamii hivi sasa inaishi katika mazingira ya upotofu, dhulma, na maovu yamezunguka pembe zote kiasi kwamba kumlea mtoto katika maadili mema limekuwa ni jambo gumu sana.

"Mabaa, grocery, madisco, mazizi na mabucha ya nguruwe yamezunguka Misikiti yetu na majumba yetu, tutawalea vipi watoto wakaleleka vizuri bila kuondoa maovu haya?" alihoji Sheikh Mbukuzi.

Awali katika risala yao kwa Amir, vijana wamewataka Maimamu wa Misikiti wasiwaelewe vibaya vijana wanaoamua kuanzisha jumuiya mbalimbali za Kiislamu katika Misikiti kwa lengo la kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu.
--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org

 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook