Putin alitoa tahadhari hiyo katika mkutano
wake na waandishi wa habari wa Uingereza uliofanyika mwishoni mwa mwezi
uliopita ambao ulihudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Bwana Tony
Blair.
Wakati Putin akitoa kauli hiyo Waislamu zaidi ya 400 walikuwa wakiandamana katika mitaa ya jiji la London kupinga ziara yake nchini Uingereza kufuatia mashambulizi ya kinyama yanayofanywa na majeshi ya Russia nchini Chechnya.
Waislamu nchini humo wamemlaumu Bwana Tony Blair kwa kumualika mtu waliyedai kuwa mikono yake ina damu za raia wasio na hatia na mwenye maradhi ya kuuchukia Uislamu.
"Namna alivyoonekana katika mkutano na waandishi wa habari, Putin anaashiria kuwa dhalimu na dikteta siku za usoni. Badala ya kukiri jinai anayotenda Chechnya, analaumu Waislamu", ameeleza Tanzeem Wasti Mwenyekiti wa kamati ya masuala ya Kimataifa iliyochini ya Baraza la Waislamu nchini humo.
Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari, Bwana Putin aliwashambulia Waislamu wa nchi za magharibi kwa kile alichodai ushawishi wao kuyataka mataifa ya ulaya yaiunge mkono Chechnya.
"Baadhi ya viongozi wa nchi za Ulaya hawako tayari kuiunga mkono Russia kwa kuchelea upinzani kutoka kwa wakazi Waislamu wa Ulaya, alidai Rais huyo aliyepata kuwa mkuu wa shirika la ujasusi la Russia (KGB).
Aliendelea kusema kuwa inachokifanya Russia Chechnya ni kuwastaarabisha Wachechen.
"Hatua za Russia Chechnya ni urejeshaji wa ustaarabu katika eneo hilo", alisema kwa majivuno Bwana Putin.
Akihalalisha unyama inaofanya Russia Chechnya, Putin alilaumu vikali kile alichokiita magaidi wa Kiislamu. "Lengo letu, alisema fedhuli Putin, lilikuwa "kuikomboa Chechnya kutoka kwa magaidi Waislamu wa Kimataifa, na alionya kwamba tishio hilo la Uislamu huenda likazikumba nchi nyingine za bara hilo.
Waislamu nchini Uingereza wameichukua kwa uzito kauli ya Bwana Putin dhidi ya Waislamu wa Ulaya na wameahidi kulifikisha suala la Chechnya katika mahakama ya dunia.
"Hatuwezi kuvumilia mauaji ya ndugu zetu katika bara hili na tutatumia njia zote kuhakikisha haki inatendeka kuhusiana na maangamizi ya Chechnya", alisema Mwenyekiti wa kamati ya Waislamu nchini humo.
Baadhi ya mabango yaliyobebwa na waanadamanaji waliokuwa wakizunguka mitaa ya Jiji la London yalikuwa na ujumbe usemao "mikono ya Putin ina damu za Wachechen 100,000".
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu nchini Uingereza, Iqbal Sacramie, amemwandikia barua Waziri mkuu wa nchi hiyo kuelezea masitiko ya Waislamu kufuatia ziara ya bwana Putin nchini humo.
Barua hiyo imehoji ni kwa namna gani serikali ya Uingereza inakuwa na mashusiano na muuaji.
Aidha, imewataka Waingereza waunge mkono wito
wa kufanyika uchunguzi juu ya kukiukwa kwa haki za binadamu kulikofanywa
na askari wa Russia nchini Chechnya.
Taasisi na makundi mbali mbali ya Waislamu yameungana na aliyekuwa Spika wa Bunge la Sudan, Dk. Hassan al Turab kumshutumu kiongozi wa nchi hiyo Generali Omar al Bashir.
Wamesema mtafaruku uliozushwa na Rais huyo hautalijenga Taifa hilo badala yake utatoa nafasi kwa mataifa adui kulisambaratisha.
Mtaalamu mmoja wa kiislamu wa masuala ya siasa amesema Rais huyo amejiangusha kisiasa katika mgogoro wake na Dk. Turabi kwa kuwa inaeleweka wazi umadhubuti wa Sudan katika siasa za kimataifa umetokana na jitihada za Turab.
Aidha mwamko wa kisiasa na kidini walionao wasomi na vijana wa nchi hiyo umetokana na mtaalamu huyo wa masuala ya sheria Duniani.
Hali nyingine iliyoelezwa kumuangusha Generali AlBashir ni jitihada ya hivi karibuni ya kujaribu kurejesha uhusiano na mataifa ya kigaidi ambayo imeelezwa ni kujipendekeza kwa watu ambao hawana nia nzuri kwa Taifa la Sudan.
Mataifa hayo ni pamoja na Marekani ambayo kufuatia mgogoro huo imefungua ubalozi wake mdogo ikidai kuanzisha upya uhusiano na Sudan.
Mwanzoni mwa mwaka juzi Marekani ilikipiga mabomu kiwanda cha madawa cha Sudan ikidai kinahusika na utengenezaji wa silaha za sumu.
Upigaji huo wa mabomu ulikuja siku chache
baada ya kutokea milipuko ya mabomu katika balozi za Marekani miji ya Nairobi
na Dar es Salaam.
--
![]()
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |