BARUA


Pongezi CUF Kilwa Kivinje

Ndugu Mhariri

NAOMBA unipe fursa ili nitoe pongezi zangu za dhati kwa viongozi na wanachama wa CUF mjini Kilwa Kivinje.

Mji wa Kivinje ni mji mashuhuri saana katika historia ya Afrika Mashariki na Kati. Wakazi wake wana sifa za ukarimu, upole, na ucha Mungu. Pia hapo ndipo ilipo hospitali ya wilaya.

Jambo la kusikitisha ni hali ya barabara inayounganisha mji huu na sehemu nyngne za wilaya ni mbovu sana. Hali ya barabara hiyo ni kero kubwa kwa wananchi.

Linalotia uchungu zaidi ni suala la wagonjwa ambao inabidi wafikishwe hospitalini hapo kwa matibabu. Kama ni mama mjamzito si ajabu akajifUngua njiani kwa misukosuko ya barabara hiyo.

Wana CUF walipoona tatizo hili ni la muda mrefu na halipatiwi ufumbuzi, basi wameamua kuitengeneza barabara hiyo kwa mikono yao ili kuwaondolea adha kubwa wanaoipata. Wakati ambapo kuna kambi kubwa ya ujenzi ya serikali kilometa chache tu kutoka mji huo, lakini hakuna linalofanyika. Sijui hali hii mpaka lini?

Mwisho tunawapongeza wote walioshiriki katika kazi hiyo muhimu na tunaomba msiishie hapo yapo mengi ya kufanya ili kuondoa matatizo ambayo wenzetu bila kujali athari zinazotupata kwa makusudi tu hawataki kuyaondoa.

Daima tunasema Haki sawa kwa wote. Penye nia pana njia.

Bady Bashir,
Mtoni,
Dar es Salaam.


Waeleweni vizuri wanapokemea udini

Ndugu Mhariri

INAVYOELEKEA kwa tafsiri ya viongozi wa CCM na serikali yake, kuendesha mambo bila kujali dini ni pale viongozi wote wanapokuwa Wakristo.

Kiongozi anapoteua watendaji Wakristo watupu hapo Ukristo hakuna.

Udini unakuja hali hiyo inapolalamikiwa. Kila anayelalamika kwanini upo ubaguzi kwa misingi ya dini huyo ndiye huitwa mdini na anashutumiwa kwa kuleta udini.

Ni muhimu kwanza Waislamu waielewe nukta hii. Pili wasichoke kusema japo watu wenyewe wanaonekana kutokuwa na haya.

Juma Jackson,
Kibaha.


Shinikizo la Kanisa litaendelea hadi lini?

Ndugu Mhariri

NINAOMBA kwa heshima unipe fursa katika gazeti lako ili niwape nasaha zangu Waislamu.

Imekuwa ni kawaida kusikia au kuona Kanisa likitoa maelekezo linayoyataka na serikali ya CCM inatii haraka kwa ushahidi ufuatao:

Mosi, Tanzania kujiunga na OIC hapana. Pili, kutaka kuitukuza siku tukufu ya Ijumaa hapana. Tatu, kutaka kuwepo uwiano mzuri wa ajira serikalini hapana. Nne, kutaka kuwepo uwiano mzuri wa kuchagua wanafunzi kwenda sekondari hapana. Tano, kuchanganya mfumo wa maisha (dini) na siasa hapa. Sita, kuwa na ubalozi wa Vatican ndiyo. Saba, kuzitukuza siku za Jumamosi na Jumapili ndiyo. Nane, kuteua wasimamizi wa uchaguzi Wakristu watupu ndiyo. Tisa, kuchanganya dini na siasa ndiyo. Kumi, kufanya wimbo wa Kanisa kuwa wa Taifa ndiyo. Kumi na moja, kufanya dua ya Kanisa kuwa ndiyo dua ya Bunge ndiyo.

Ushahidi gani tena tunataka zaidi ya huu?

Mwisho ninamuomba Allah (s.w.) atuzindue ifikapo mwezi Oktoba na tukumbuke maneno matukufu ya Allah (s.w).

Id Hamad,
Box 4,
Bukoli, Geita


Dawa ni kuungana

Ndugu Mhariri

NIMEKUWA nikisoma gazeti la AN-NUUR kwa muda sasa. Nimegundua kwamba mnachojaribu kufanya kwa kiwango kikubwa ni kuutokomeza Ukristo kwa propaganda na kupandikiza chuki kwa Waislamu.

Tatizo ni kwamba mnachofanya ni kukata matawi badala ya shina. Bw. Muhammad (s.a.w.) alisema: "...walio wabaya zaidi kwa Waislamu ni Mayahudi na Mushirikina..."

Dawa ya kuutokomeza Ukristo ni Waislamu ambao kwa ukweli Mola amewajaalia utajiri mkubwa kuungana nyote; kama walivyofanya marehemu Nasser, Assad na Waislamu wengineo ili kumng'oa Myahudi pale Yerusalemu.

Hapo Ukristo hautasimama maana ndio nguzo vinginevyo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Hamtaweza. Ila kama mpo kujipatia riziki kwa 'kuuza' gazeti endeleeni Inshaallah na Ukristo utashamiri.

Collins Thewe,
S.L.P. 14,
Ifakara.


CCM sherehe ya nini?

Ndugu Mhariri

KAMA ni zama za uwazi na ukweli kwanini CCM hawasemi madeni makubwa yanayotukabili yametokana na nini? Na yametusaidia vipi kimaendeleo?

Kinyume chake hali duni za kiuchumi zinaendelea kutuandama katika sekta mbalimbali za kijamii, katika afya hali ni ya kutisha, hakuna madawa, vitanda, vitendea kazi na kadhalika. Barabara zimekuwa mahandaki yasiyopitika, shule ndiyo zimebaki nembo tu zikikabiliwa na upungufu wa vitabu, madawati, walimu, majengo na kadhalika.

Tatizo la maji salama ni adha kubwa isiyosemeka. Cha kusikitisha na kushangaza ni kufanyika sherehe hewa ya kusamehewa madeni, ilhali za wananchi ni mbaya kiuchumi na kijamii.

Hii inatuonesha kwamba madeni haya yamewafaidisha wakubwa tu na ili kuulaghai umma zinafanyika sherehe ya kujipongeza.

Abdul R. Bashir,
Box 159,
Hai-Moshi.

--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org

 
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook