Sira ya Muhammad: Kipindi cha utume Makka
WAISLAMU nchini wataanza kuadhimisha kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume(s.a.w) kuamnzia tarehe 12 ya Rabiul Awwal. Kuanzia toleo hili tutakuwa na mfululizo wa makala zinazoelezea wasifu wake akiwa kigezo cha waumini. Tunaanza na maisha yake Makka.
Tabia ya Muhammad (s.a.w.) katika Ujana
Tunajifunza katika vitabu vya historia kuwa hata alipokuwa mtoto hakuwahi kufanya vitendo vya kipuuzi vya kitoto na alikuwa ni mwenye haya sana. Wakati fulani kuta za Ka'bah zilifanyiwa ukarabati, wavulana wadogo wadogo nao walishiriki.
Wavulana hawa walizitoa nguo zao za kiunoni na kuziweka mabegani ili kubebea mawe. Abu Talib alimshauri Mtume (s.a.w.) naye ajiunge na watoto wenzie. Mtume (s.a.w.) alikubaliana na ushauri wa Ami yake, lakini alipojaribu naye kuvua nguo yake kubaki uchi, alishikwa na bumbuazi (butwaa) na kuanguka chini.
Mtume (s.a.w.) tangu utotoni mwake aliepukana na tabia zote chafu zenye kuchukiza watu kwa ujumla. Pia aliepushwa na matendo yote maovu yenye kuchukiza Allah (s.w.) ambayo yalionekana mazuri mbele za watu wa jamii yake.
Tangu utotoni mwake, Muhammad (s.a.w.) alisifika kwa kila sifa nzuri zilizobainishwa katika Qur'an. Bibi Aisha (r.a.) alipoulizwa juu ya tabia ya Mtume (s.a.w.) alijibu kuwa tabia yake ni Qur'an yaani amejipamba na vipengele vyote vya tabia njema vilivyobainishwa katika Qur'an tangu utotoni mwake. Qur'an yenyewe miongoni mwa aya zake za mwanzo mwanzo kushuka, inamsifu Mtume (s.a.w.) kwa tabia yake tukufu:
"Na bila shaka unatabia njema kabisa"
Aya hii haielezi kuwa tabia yake ilikuwa njema tu pale alipopata utume bali inaashiria kuwa tabia yake njema anayo tangu utotoni mwake. Muhammad (s.a.w.) tangu utotoni mwake tumeona kuwa alikuwa mpole mtulivu, mwenye huruma, mwenye haya na mwenye sifa zote nzuri nzuri zilizowapendeza watu na kuwavutia. Alikuwa mashuhuri Bara Arabu nzima kwa ukweli na uaminifu wake. Alikuwa mwaminifu mno mpaka akapewa jina la Al-Amin. Muhammad alikuwa hatajikani ila kwa jina la Al-Amin.Wakubwa na wadogo walimuheshimu na walimpa amana zao kuwawekea hata baada ya kupewa Utume.
Kujiunga na chama cha kuwatetea Wananchi Wanyonge
Tumeona kuwa baada ya Abd al-Muttalib kufariki mtoto wake Abu Talib aliyeshika nafasi yake katika kuwaongoza Maquraysh na baadhi ya koo za Kiquraysh zilimheshimu. Lakini kutokana na umasikini aliokuwa nao hakuweza kupata nguvu na hadhi aliyoifikia baba yake.
Baadhi ya koo zilizokuwa na watu wengi matajiri na wenye nguvu zilifanya jeuri kubwa katika mji wa Makkah. Zilizokuwa jeuri kupita kiasi ni koo za Bann Umayyah na Banu Makhzum. Mwenye chake hakuwa na chake mbele yao. Mwenye nguvu na uwezo wa kujitetea kwa silaha ndiye tu aliyeweza kuishi kwa amani na furaha.
Jeuri yao ilipopindukia mipaka na watu wakachoshwa na udhalimu wao, Bwana Zubayr bin Abd al-Muttalib (Ami yake Mtume aliwaita wakubwa wa kila ukoo wa Kiquraysh na akawapa shauri ya kuanzisha chama cha kuwakinga au kuwalinda wanyonge na kila namna ya udhalimu waliokuwa wakifanyiwa na wale wenye nguvu.
Ni koo tano tu kati ya koo kumi na mbili za Kiquraysh zilizokubaliana na shauri hili. Koo zilizokubaliana ni Banu Hashim (ukoo wa baba yake Mtume) Banu Zuhra (ukoo wa mama yake Mtume), Banu Tamym (ukoo wa Abu Bakr) Banu Asad (ukoo wa Bibi Khadija mke wakwanza wa Mtume) na Banu Muttalib. Madhumuni ya chama hiki yalikuwa kama ifuatavyo:
1). Kuwasaidia wasiojiweza bila ya kujali ukoo wao au kabila lao.
2). Kumsaidia kila mwenye kudhulumiwa na kufanya kila inavyowezekana kurejesha haki yake.
Muhammad (s.a.w.) akiwa na umri wa miaka ishirini alishiriki kikamilifu na kutoa ushauri wake katika kuunda chama hiki. Hata baada ya kupewa Utume, Mtume (s.a.w.) alikuwa akifurahi sana kila alipokumbuka kuwa yeye alikuwa miongoni mwa wanachama katika chama hicho na alikuwa akisema.
"Niliyapenda makubaliano ya chama hicho kuliko ngamia mwekundu na mpaka sasa hivi nakubaliana na madhumuni hayo", amekariri Ibn Al-Athir katika "Al-Kamil fil Tarikh Beirut 1965, Vol. II uk. 41)
Kujiunga Muhammad (s.a.w.) katika chama hiki ni kielelezo cha tabia yake, tangu utotoni mwake alikuwa na tabia ya kuwahurumia wanyonge. Hakupata usingizi kwa ajili ya matatizo ya wengine. Alifurahi sana kwa kuwepo chama hiki ambacho alikitegemea kuwa huenda kikawa ndio utatuzi wa tatizo sugu la dhulma katika jamii.
Muhammad (s.a.w.) katika misafara ya Biashara
Mtume (s.a.w.) alianza kujitegemea tangu udogoni mwake. Tumeshaona kuwa kazi aliyojishughulisha nayo katika kipindi chake cha uvulana ni uchungaji wa mbuzi na kondoo. Umri wake ulipoinukia kidogo alijiingiza katika shughuli ya biashara ambayo ilikuwa ni kazi ya heshima mno katika nyakati hizo. Kazi hii hakuianza ghafla bali alianza kwa kujifunza kidogo kidogo akiwa anaandamana na ami zake. Alipokuwa na umri wa miaka tisa aliongozana na amri yake mdogo, Bwana Zubayr, kwenye msafara wa biashara kwenda Yemen na walikaa huko kwa muda wa siku tatu. Alipokuwa na umri wa miaka kumi na mbili, alisafiri tena na amri yake, Abu Talib, kwenda Shamu (Syria). Walipofika katika mji wa Busra walikutana na padri mkubwa wa Kikristo, jina lake Bahyra alimtambua Muhammad (s.a.w.) kuwa ni Mtume wa Allah kwa dalili mbali mbali alizoziona kama zilivyotabiriwa katika Injili.Bahyra alimsihi Abu Talib na kumwambia "Mtoto huyu namuona ana alama zote za Mtume aliyetabiriwa kuwa atakuja. Basi naona ni hatari kubwa kama atakwenda Sham; asije akauawa na Mayahudi huko. Nakusihi sana urejee naye au umpe mtu mwaminifu arejee naye, nawe uendelee na biashara zako.1 Abu Talib alimpa mtu arejee naye Makkah naye aliendelea na safari yake. Padri Bahyra pamoja na kuwa alikuwa na uhakika kuwa Muhammad (s.a.w.) ndiye yule Mtume aliyetabiriwa katika Taurati na Injili, bado hakusilimu, mtume alipopewa utume. Bali mwanafunzi wake Bwana Salman Al-Farsy, Mwajemi, alisilimu mara alipopata habari ya utume wake.
Baadhi ya makafiri walidai kuwa Salman al-Farsy, Mwanafunzi wa Bahira, ndiye aliyemfundisha Mtume Qur'an. Qur'an yenyewe imeonyesha udhaifu wa dai hili kama ifuatavyo:
"Na bila shaka tunajua kwamba wanasema:"Yuko mtu anayemfundisha" lakini lugha ya yule wanaemuelekezea (kuwa anamfundisha Mtume) ni ya kigeni na hii (lugha iliyotumika katika Qur'an) ni lugha ya Kiarabu fasihi (Bulbul)" (16:103).
Ni jambo lisiloingia akilini kuamini kuwa mtoto wa miaka kumi na mbili atajifunza falsafa ya dini kwa muda mfupi kiasi cha kukutana njiani na aweze kutoa mafundisho hayo baada ya miaka 28 katika mfumo wa dini tofauti na dini ya mwalimu wake!
Alipokuwa na umri wa miaka 15, Muhammad (s.a.w.) alianza kufanya biashara ndogo ndogo katika miji iliyokuwa karibu na Makkah. Tofauti kabisa na wafanya biashara wengine wa nyakati hizo, Mtume (s.a.w.) alikuwa mwaminifu mno katika mahusiano yake yote na watu. Alikuwa mfanyabiashara mkweli na muaminifu ambaye hakuwahi kutoa hata mara moja kauli ya uongo. Wakati mmoja Muhammad (s.a.w.) aliwahi kumuuzia mtu ngamia. Baada ya muda alikumbuka likumbuka kuwa ngamia mmoja katika wale aliowauza alikuwa kilema (ana kasoro). Mara moja alipiga shoti juu ya farasi kumkimbilia yule mnunuzi. Alipompata alimfahamisha juu ya ngamia yule, kisha akamrudishia yule mununuzi fedha alizolipa kwa ajili ya yule ngamia wake.
Muhammad (s.a.w.) alikuwa ni mwenye kuchunga ahadi kweli kweli.Kutokana na msimamo wake katika kuchunga ahadi, aliwahi kumsubiri mtu njiani kwa muda wa siku tatu. 'Abdullah bin Abi al-Hinsa, aliyemuahidi Mtume kuwa amsubiri na atarudi pale kwa muda mfupi. Mtume hakutoka pale mpaka siku ya nne. 'Abdullah alipopita siku ya nne alimkuta Mtume (s.a.w.) pale bila ya kuonyesha hali ya kuchukia. Mtume alimfahamisha 'Abdullah: "Niko hapa kwa siku tatu kutekeleza ahadi yangu" 'Abdullah aligundua kosa lake na kumuonea huruma Mtume.1
Muhammad: Mkweli na Muaminifu
Tabia yake njema iliyoshehenezwa na ukweli, uaminifu, uchungaji ahadi na mahusiano mema na watu wote ilimfanya Muhammad (s.a.w.) kujulikana na kupewa heshima na hadhi na watu wa jamii yake. Hapakutokea kijana mwenye tabia ya mfano wake katika Bara Arabu nzima. Umaarufu na hadhi yake katika jamii, ulidhihirishwa na majina ya heshima aliyoitwa kwayo. Ni wakati huu wa ujana wake aliitwa kwa majina ya Muhammad As-Sadiq na Muhammad Al-Amini.
Kumuoa Bibi Khadija
Umaarufu wa Muhammad (s.a.w.) kutokana na tabia yake tukufu ulienea Bara Arabu nzima. Bibi Khadija, mwanamke mjane miongoni mwa matajiri wakubwa Makkah, alivutiwa na tabia ya Muhammad (s.a.w.) Bibi Khadijah alimtaka Muhammad ampelekee bidhaa zake Yemen kwa ujira wa ngamia wawili.
Muhammad (s.a.w.) alikubali na alirejea na faida kubwa zaidi kuliko matarajio ya Bibi Khadijah. Bibi Khadijah alivutika kwa faida hiyo kubwa na ikambidi tena amuombe Muhammad (s.a.w.) ampelekee bidhaa zake Shamu kwa malipo baada ya ile safari ya kwanza alipokuwa na umti wa miaka 12. Katika msafara huu, Muhammad (s.a.w.) alimletea Bibi Khadija faida kubwa zaidi ya mategemeo yake. Khadija alikuwa hawahi kupata faida kubwa kiasi kile tangu aanze kufanya biashara katika misafara ya Shamu.
Pamoja na furaha ya kupata faida kubwa kiasi hicho, Bibi Khadijah alizidi kufurahi na kuvutiwa na Muhammad aliposikia sifa zake za ajabu kutokana na taarifa ya Maisarah waliyeongozana naye. Kutokana na alivyovutika, Bibi Khadija hakuweza kustahamili kukaa mbali na Muhammad.
Hivyo alimtaka radhi Muhammad na kuomba amuoe. Bibi Khadija wakati huo alikuwa mjane mwenye umri wa miaka 40 aliyewahi kuolewa mara mbili na kujaaliwa kupata watoto watatu wawili wanaume na mmoja mwanamke.
Kabla ya hapo Matajiri na wakuu wengi wa Makkah
walipeleka posa zao kwa Bibi Khadija lakini aliwakatalia. Muhammad (s.a.w.)
akiwa na umri wa miaka 25, alikubali ombi la Bibi Khadijah baada ya kushauriana
na Ami yake, bila ya kujali tofauti ku
--
![]()
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |