Bismillahir Rahmaanir Rahiim
ISLAMIC
PROPAGATION CENTRE
TAMASHA LA AWAMU YA PILI YA UJENZI WA KIRINJIKO
ISLAMIC SECONDARY SCHOOL
30 June - 14 July, 2000
Tunachukua fursa hii kuwatangazia Waislamu wote nchini kuwa tamasha la awamu ya pili ya ujenzi wa "Kirinjiko Islamic Secondary School" litaanza tarehe 30 Juni hadi 14 Julai 2000.
Awamu hii ya pili itahusika na kuinua majengo yafuatayo:-
(1) Mabweni 4
(2) Nyumba 5 za walimu
(3) Mabwalo 2 ya chakula
(4) Madarasa 4
(5) Msikiti
Waumini wote mnaombwa kushiriki katika tamasha hili kwa kuhudhuria au kwa kutoa mchango wa kuligharimia.
Watakao shiriki katika tamasha hili tunaomba wathibitishe kushiriki kwao na idadi ya siku watakazo shiriki kabla ya tarehe 25/6/2000.
Pia tunaomba washiriki waje na mchango wa chakula Tsh. 500/- kwa siku. Ambao hawatakuwa na uwezo wa kujigharimia chakula watuarifu kabla ya tarehe 25/6/2000.
Shime Waislamu! Tuimarishe mshikamano wetu na tuhudhurie kwa wingi.
Wabillahi Taufiiq
MKURUGENZI
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |