Tanzania kumezwa na Kenya

IPO hofu kuwa huenda kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kukaifanya Tanzania soko la bidhaa za Kenya na Uganda.

Kutokea kwa hali hiyo, kutaifanya Tanzania imezwe kiuchumi na kuwa ngazi kwa nchi shirika kusonga mbele.

Habari za vyombo vya habari zimeeleza kuwa, wafanya biashara nchini wamekuwa wakitizama kuanza kwa Jumuiya hiyo kwa wasiwasi.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Jakaya Kikwete amethibitisha kuwepo kwa hofu hiyo.

Mhe. Kikwete amesema, hofu hiyo inatokana na ukweli kwamba Tanania ni maskini zaidi kuliko Kenya na Uganda.

Kwa hali hiyo upo uwezekano wa nchi hizo kuua juhudi za Tanzania katika uzalishaji.

Waziri Kikwete amesema, kutokana na wasiwasi huo, hatua kadhaa zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wafanyabiashara katika mazungumzo.

Amesema, hatua nyingine ni kuweka kanuni itakayohakikisha kuwa mwenye uwezo anabeba mzigo mkubwa zaidi na mdogo anasaidiwa akue sio kumezwa.

Mhe. Kikwete alikuwa akiongea juzi na mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC juzi ambaye alitaka kujua ukweli kuhusu kuwepo kwa hofu hiyo.

Juzi, Bunge liliridhia mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, mkataba huo tayari umesharidhiwa nchini Kenya na Uganda.

Mkataba huo utapelekea kuwa na sarafu moja na hatimaye kuundwa kwa Shirikisho la kisiasa.

Jumuiya hii ilikuwepo awali ambapo nchi hizi zilishirikiana na kuwa na mashirika makubwa ya huduma za kiuchumi na jamii.

Miongoni mwa mashirika hayo yalikuwa shirika la Reli, shirika la Ndege (East African Airways), Bandari na Posta na Simu.

Jumuiya hiyo ilivunjika mwaka 1977 kutokana na tofauti za kisiasa.

Waliokuwa wafanyakazi wa mashirika hayo kwa upande wa Kenya na Uganda walilipwa haki na mafao yao mara moja. Lakini kwa Tanzania bado wanadai.

Baada ya mvutano na serikali kwa muda mrefu, wafanyakazi wengine wamepewa hundi za sh. 10/-. Hali hiyo imepelekea wafanyakazi hao wastaafu kujikusanya kuipeleka serikali mahakamani.

--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org


An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook