Mtoto anatakiwa kuwatii wazazi wake kwa yote yasiyopingana na hukumu za Mwenyezi Mungu. Mtoto wa Kiislamu anatakiwa awe:
1. Msafi na mwenye nidhamu - popote alipo, nyumbani, shuleni, madrasa mwili, nguo na matendo.
2. Awaheshimu wazazi au wanaomlea wakubwa, wadogo na rika zote;
3. Achunge adabu na kuchunga kanuni zake;
4. achunge adabu za kuzuru watu na kwenda njiani'
5. Achunge adabu za kuingia nyumba za watu.
Haki za Wazazi
Watoto wanatakiwa wawaheshimu wazazi wao na kuwafanyia wema mkubwa:
Na tumemuusia mwanaadamu (kuwafanyia ihasani) wazazi wake wake - mama yake ameichukuwa mimba yake kwa udhaifu juu ya udhaifu, na (kumnyonyesha na kuja) kumwachisha kunyenya katika nyaka mwili - ya kwamba unishukuru Mimi na wazazi wako; marejeo yenu ni kwangu. (31:14).
Na Mola wako amehukumu kuwa msimuabudu yoyote ila Yeye tu. Na (ameagiza) kuwafanyia wema (mkubwa) wazazi. Kama mmoja wao akifikia uzee, (naye hayuko) pamoja nawe, au wote wawili, basi usiwaambie hata Ah! Wala usiwakemee. Na useme nao kwa msemo wa hishima (kabisa). (17:23).
Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa (njia ya kuwaonea) huruma (kwa kuwaona wamekuwa wazee). Na useme: "Mola wangu! Warehemu (wazee wangu) kama walivyonilea katika utoto". (17:24).
Ili kuonesha nafasi muhimu waliyo nayo wazazi, Mwenyezi Mungu (s.w.) ameagiza kuwa wafanyiwe ihsani. Na katika aya nyingi agizo hilo limekuja mara tu baada ya agizo la kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake. Baadhi ya aya hizo ni hizi zifuatazo:
Mwabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni ihsani wazazi wawili. (4:36).
Sema: Njooni nikusomeeni alivyokuharimishieni Mola wenu: ya kwamba msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wenu. (6:151).
Na tulipochukua ahadi ya kizazi cha Israili kuwa: Hamtamwabudu yoyote ila Mwenyezi Mungu; na muwafanyie wema wazazi. (2:83).
Na miongoni mwa aya zilizotia msisitizo mkubwa ni hizi zifuatazo:
Na Mola wako amehukumu kuwa msimuabudu yoyote ila Yeye tu. Na (ameagiza) kuwafanyia wema (wakubwa) wazazi. Kama mmoja wao akifikia uzee, (naye yuko) pamoja nawe, au wote wawili, basi usimwambie hata Ah! Waala usiwakemee. Na usema nao kwa msemo wa hishima (kabisa). Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa (kuwaonea) huruma. Na usome: Mola wangu; Warehemu (wazee wangu) kama walivyonilea katika utoto. (17:23- 24).
Miongoni mwa mambo ya kuzingatia katika aya hizi ni haya:
1. Kuwatendea wema wazazi ni amri itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Si hiari ya mtu, bali wajibu.
2. Wazazi watendwe wema na kuhishimiwa kiasi ambacho hata kuguna kidogo tu kama kusema "Ah!" pia ni makosa, seuze kuwakemea.
3. Wema anaotakiwa mtu kuuonesha kwa wazazi wake umefanishwa na ndege wanavyowafunika makindawao kwa kuwateremshia mbawa zao ili kuonesha wema, huruma na mapenzi.
4. Watu wanakumbushwa wakumbuke wema, huruma na mapenzi waliyopewa na wazazi wao walipokuwa bado wachanga.
Kutokana na umuhimu wa jambo hili ndio maana tunajifunza katika Qur'an kuwa mitume wa Mwenyezi Mungu walikuwa siku zote wakijitahidi kuwafanyia wema wazazi wao (Taz: Qur'a 19:14, 19:32).
Qur'an pia (46:15) imemtaja mama kuwa alipata usumbufu mkubwa katika uja uzito, uzazi na ulezi wa mtoto. Hivyo anastahili heshima maalum.
Nini maana ya kuwafanyia wema Wazazi?
Tumeona kuwa Qur'an na hadithi vimesisitiza sana kuwafanyia ihsani wazazi. Ihsani au wema katika hali halisi ya maisha ya kila siku maana yake nini? Neno lililotumika katika hadithi nyingi ni "birr" - ambalo lina maana ya Ucha-Mungu, wema, huruma,. heshima, utii, subira nakadhalika. Hivyo kuwafanyia wema wazazi maana yake ni kuyatimiza yote hayo.
Kwanza kuwahurumia wazazi. Katika hadithi iliyosimuliwa na Baihaq, Mtume (s.a.w.) amesema: Ukiwahurumia wazazi utapata malipo (sawa na) ya Hija. Na usipowahurumia utakuwa unakwenda kinyume na birr.
Pili, awahishimu wazee wake. Mtu asiinue sauti
yake anapozungumza na mzazi wake. Katika Ibn Majah Mtume (s.a.w.) amesema:
Usiinue sauti mbele yao (wazazi). Tatu, mtu awapende wazazi wake. Katika
kuelezea mwenendo wa Mtume (s.a.w.) tunafahamishwa kuwa ilikuwa Fatma akienda
kwa Mtume (s.a.w.), Mtume alikuwa akisimama, akimbusu na kumpisha akae
mahali pake. Na Mtume (s.a.w.) akienda kwa Fatma, Fatma alikuwa akisimama,
akimbusu na kumpisha mahali pake. Na pia ni wajibu wa mtu kuwahudumia wazazi
wake wakiwa na shida.
Kuwakimu wazazi ni wajibu:
Masharti yanayotosha kumlazimisha mtu kuwahudumia wazazi wake ni matatu:
1. Ikiwa hawana uwezo wa kupata mahitaji yao ya lazima.
2. Ikiwa hawawezi kufanya kazi ili kuchuma mali au kutafuta riziki zao kwa sababu ya uzee au ulemavu.
3. Ikiwa mtoto anao huo uwezo wa kuwahudumia.
Na uwezo siyo ziada baada yakuwa ametosheleza
mahitaji yake yote na halafu ndio awafikirie wazazi, la. Baadhi ya wanazuoni
wanasema kama mtu anamejipatia mahitaji yake ya lazima kwa mchana mmoja
na usiku wake, na kubaki basi anahesabiwa kuwa anao uwezo, na hivyo ampatie
mzazi wake kila katika kile kilichozidi.
--
![]()
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |