BARUA

Tupambane na Abujahal

Ndugu Mhariri

KATIKA miaka ya hivi karibuni hasa kuanzia mwaka 1993 matukio ya kukamatwa na polisi Masheikh, Maimamu na waumini wao yamekuwa jambo la kawaida.

Viongozi wa Waislamu wanafanywa kama vibaka.

Utasikia wametishia kuua, wamefanya fujo, wanahatarisha amani na tuhuma nyingine.

Ni imani yangu kuwa hayupo Muislamu leo asiyeelewa propaganda na uonevu unaofanywa dhidi ya Waislamu.

Inatia moyo pia kuona kuwa kila Muislamu anajua kuwa wanaoyafanya haya ni kina Umayya na Abujahal wa zama hizi.

Abujahal wa zama zile walizalishwa na mfumo wa dini ya kishirikiana. Leo wanazalishwa na mfumo huo huo.

Kina Bilal walitekeleza wajibu wao. Wakaondoa dhulma kwa kupambana na akina Abujahal katika Badri.

Basi tujue kila tuonavyo Maimamu wetu na waumini wenzetu wakikamatwa na polisi ovyo, tujue Allah anatukumbusha kuwa hatujatekeleza wajibu wetu wa kupambana na akina Umayyah na vyama vyao vinavyowapa nguvu.

Badri yetu twaijua? Akina Ubei bin Sahil twamjua?

Basi tuwaoneshe kwamba hata leo yupo Hamza, Khalid bin Walid na Bilal.

Abu Hashim Masoud,
Bagamoyo.



 


Ni vyombo vya habari vya CCM au vya Taifa?


 






Ndugu Mhariri

NAOMBA nafasi ili niweze kutoa dukuduku langu kutokana na picha na mwenendo mbaya unaoendeshwa na vyombo vya habari vya Taifa.

Vilitazamiwa kuwa vyombo hivi vitatenda kazi vizuri kwa wananchi. Kwa kutenda kazi zake vizuri bila ya upendeleo wala ushabiki wowote wa chama fulani cha siasa. Lakini matokeo yake vyombo hivyo vinaonesha ukereketwa na ushabiki wa chama kimoja cha siasa ambacho ni CCM. Bali tunaviona vyombo vya habari vya kujitegemea ndivyo vinavyotekeleza azimio au wito wa kutopendelea au kubagua au kupendelea upande mmoja.

Tunashangazwa na vyombo hivi vya Taifa jinsi vinavyopendelea Chama Cha Mapinduzi, kwani ni hivi majuzi tu imefanyika mikutano mikuu ya vyama vya CUF na CCM, vyama vyote hivi vilifanya mikutano hiyo ya kuwapitisha wagombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano na Zanzibar.

Jambo la kushangaza na kusikitisha ni kuwa wakati mkutano wa CCM unafanyika ulitangazwa na kuoneshwa kupitia katika vyombo hivyo moja kwa moja kutoka kule ulikofanyika, lakini mkutano wa Chama cha CUF licha ya kuoneshwa au kutangazwa na vyombo hivyo bali hata kuripotiwa kwa sentensi moja.

Badala yake vyombo vya habari vya nje ndivyo tulivyovisikia kutangaza mkutano huo. Hivi ni kweli habari nyingine tupewe na nyingine tusipewe mpaka tusikilize vyombo vya habari vya nje ya nchi wakati vyombo vya habari tena vya Taifa tunavyo? Hivi ndivyo sawa kwa wote?

Sasa mimi nawauliza hawa watu wanaoongoza vyombo hivi vya habari, hivi vyombo vya habari ni vya Taifa au ni vya CCM? Na kama ni vya CCM basi tuambieni, ili tuweze kuweka vyombo vya habari vya Taifa ambavyo vitatoa habari za vyama mbalimbali bila upendeleo au ubaguzi wa aina yoyote ile.

Hassan AbdulQaadiri Muya,
S.L.P. 45772,
Dar es Salaam.


Nini siri ya wasomi kujiunga na CCM?

Ndugu Mhariri

HIVI karibuni wasomi wa Vyuo Vikuu vya Mlimani - Dar es Salaam na Sokoine - Morogoro wameripotiwa kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Je, kujiunga kwao kuna lengo la kutaka kuboresha hali ya maisha ya Watanzania au ni kiini macho?

Hisia yangu ni kuwa wasomi hawa wanajiunga na chama husika si kwa wito au mapenzi juu ya uzuri wa sera za chama au uhodari wa watendaji katika chama hicho. Mazingira yamewalazimisha wahitimu kucheza karata hii hasa katiak kipindi hiki kuelekea uchaguzi.

Kutokana na uwezo wa wasomi kuona mbali nionavyo mimi yafuatayo ndiyo chachu ya wasomi wahitimu kujiunga na CCM.

Kwanza, nafasi nyingi za kiutendaji katika chama husika ama zinashikwa na watu ambao umri wao ni mkubwa au wenye elimu isiyowiana na nafasi zao.

Pili, wengi wa wahitimu hawana ajira, hivyo kujiunga kwao na chama tawala kunabashiri kupata nafasi za uongozi kilaini katika nyanja mbalimabli katika chama au serikali iwapo chama hicho kitafanikiwa kuunda serikali..

Hii inatokana na ukweli kuwa kumekuwa na juhudi za makusudi za wahusika kuhakikisha kuwa kadi za kujiunga na chama zinatolewa na kiongozi au viongozi wa juu kabisa katika chama. Kwa mfano mwaka jana Morogoro kadi zilitolewa na Makamu Mwenyekiti, mwaka huu Mwenyekiti alikabidhi huko Dodoma na hatimaye Makamu Mwenyekiti alifanya hivyo kwa wana Mlimani.

Je, wahitimu wasomi hawa 80 wana-Mlimani na wengine kadhaa wana-SUA wamejiunga na chama tawala kwa madhumuni ya kulinda AMANI kama walivyodai au wanaingia katika uwanja huu kwa lengo la kutoa msukumo katika juhudi za kumwondolea Mtanzania wa leo matatizo aliyonayo kimaisha au ni katika kutafuta kazi?

Luwongo S. Hassan,
Morogoro.



Serikali ifute Kf. 19(2) katika Katiba

Ndugu Mhariri

VIONGOZI kadhaa wa Misikiti wako ndani. Kwa sababu yoyote itakayotolewa na polisi, lakini viongozi hao walikamatwa baada ya kufanyika uchaguzi wa viongozi.

Inavyoelekea kuna aina ya watu ambao ndio polisi au serikali inataka waongoze Misikiti.

Nashauri, ili kuzuia migongano serikali ifute Kf. 19(2) badala yake iweke kinachosema kuwa viongozi wa Misikiti wateuliwe na serikali.

Mwanaidi Mohamed Athumani
S.L.P 9240,
Dar es Salaam.


Fundi huyu hatufai


 


Ndugu Mhariri

SERIKALI awamu ya tatu tunaambiwa imefanikiwa kuweka misingi imara ya uchumi. Kwa hiyo inatakiwa ipewe muda inyanyue nguzo.

Lakini awamu hii ni muendelezo wa awamu iliyoanza 1961. Kama kwa miaka arobaini fundi (CCM) anajenga tu msingi. Fundi huyu hatufai.

Bora tutafute fundi mwingine.

Ramla Mwita,
Kibaha.

--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji


   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org
An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook