IMEELEZWA Wasimamizi na Waratibu wa uchaguzi, hawana uwakilishi wa watu wote.
Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu liemeyaeleza hayo katika waraka wake kwenda kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Lewis Makame.
Waraka huo Na. BK/GC/B16/161/2000 umenakiliwa kwa Mhe. Rais,Waziri Mkuu na Maimamu wote nchini.
Imedaiwa kuwa, uteuzi huo unadhamiri za makusudi za kuendeleza ubaguzi.
"Hali hii haiwezi kujitokeza yenyewe hivi hivi bila ya kulazimishwa kuteuliwa kwa watendaji wa aina hii, kwa uwiano huu, nje ya maumbile asilia", umedai waraka huo.
Likinukuu maandiko ya Padri Paul Crane kutoka makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani , Baraza Kuu limetuhumu uteuzi huo kuwa huenda umezingatia maelekezo ya kanisa ya tangu nchi haijapata uhuru.
"Kufanya uteuzi wa aina hii inatudhihirikia zaidi tu kuwa Tume yako imo katika kuendeleza utekelezaji wa maagizo yale yale ya kanisa yaliyotolewa tangu hata kabla nchi yetu haijapata uhuru wake", limedai baraza kuu.
Katika maandiko yake aliyoyatoa mwaka 1959, Padri Crane amesema tatizo la Afrika ni kwamba watu wasiofaa wamekuwa katika nafasi za utawala.
Crane alihoji ni kwa vipi wangeweza kuweka watu wanaostahili katika nafasi hizo na akasema lazima wajitahidi kadri ya uwezo wao kupata wasomi wakatoliki ambao watashika nafasi muhimu kwenye ngazi zote za jamii.
Utekelezaji wa maagizo hayo Baraza kuu limedai katika waraka huo kuwa ni pamoja na kuanzishwa vikundi vidogo vidogo vya wakatoliki walei na vikundi vya wanawake wakatoliki.
Imedaiwa kuwa kupitia vikundi hivyo wakatoliki wamefanikiwa kushika nafasi zote za madaraka nchini, kisiasa na serikalini.
"Kanisa katoliki si kwamba linahakikisha kuwa wakatoliki wao 'wanashika nafasi muhimu kwenye ngazi zote za kijamii' na watu wasiofaa hawawi katika nafasi za utawala, bali pia, zaidi ya yote, na lililobaya, linauhesabu Uislamu kuwa ni adui", umesisitiza waraka huo.
Kutokana na tuhuma hizo, Baraza Kuu limesema linalaani kwa nguvu sana uteuzi wa wasimamizi wa uchaguzi mkuu 2000, ambao Tume imefanya.
"Tunalaani kwa sababu, ikiwa mmekusudia au hamkukusudia kufanya uteuzi wenu yatakuwa yale yale ya kuweka aina ya utendaji kwenye shughuli ya uchaguzi Mkuu 2000 utakaoendeleza maafa na madhara yale yale yanayotusibu Waislamu penye watendaji wanaoteuliwa kwa kulundika wakristo", Waraka huo umesema.
Baraza Kuu limeitaka Tume izingatie Katiba ya nchi ibara ya 13 ambayo inapiga marufuku raia wa nchi hii kubaguliwa kwa sababu ya dini, kabila, jinsia au rangi yake.
Aidha, imeitaka ifanye marekebisho kwa kutengua uteuzi huo kwa kuwa kinga siku zote ni bora kuliko kuponya na kwamba ishara zote za mwenendo mbaya zidhibitiwe mapema.
Mnamo mwezi Aprili mwaka huu, Tume ya uchaguzi ilifanya uteuzi wa wasimamizi wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba.
Katika uteuzi huo imejitokeza wasimamizi walio waumini wa dini ya kikiristo kuwa kiasi cha asilimia 90 na Waislamu asilimia 10.
Tangu wakati huo jumuiya mbali mbali za kiislamu zimekuwa zikitoa malalamiko yake kuhusiana na dosari hiyo ya kiutendaji.
Hata hivyo, wahusika kwa upande wao hawajachukua
hatua zozote muafaka hali inayoweza kutafsiriwa kuwa huenda kuna mkakati
maalum ulioandaliwa ndiyo maana sura ya wasimamizi ikalazimika kuwa hiyo.
ILI kuzuia kutokea machafuko ya kisiasa
imeelezwa ni muhimu Rais aache kutenda kazi zake kama mwana CCM awapo Ikulu.
Aidha, imeelezwa Rais hana budi kuwajibika na kiapo chake cha Urais kwa Watanzania wote na asiwabague kwa misingi ya itikadi zao za kisiasa.
Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati ya Usuluhishi wa mgogoro wa Zanzibar (IPC), Bw. Muhammad A. Dedesi.
Bw. Dedesi ametoa hoja hiyo alipokuwa akizungumzia namna ya kuikoa Zanzibar na kutokea machafuko ya kisiasa.
"Rais anahitaji awe anaonana na viongozi wa makundi yote ya Watanzania yawe ya kisiasa au ya namna nyingine ili aelewe matatizo yao katika kujenga Tanzania imara yenye mshikamano", amesema.
Bw. Dedesi alikuwa akiwasilisha mada "Utatuzi wa mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar kati ya CCM na CUF", jana katika mkutano wa nane juu ya hali ya kisiasa Tanzania.
Bw. Mohammed Dedesi amesema Rais wa Zanzibar naye anawajibika afanye hivyo hivyo. Awaheshimu na awatendee mema wapinzani.
Aidha, amesema, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar haina budi ijiuzulu.
"Uchaguzi Mkuu wa 1995 ulitosha kuthibitisha kama hawawezi kusimamia uchaguzi unaotakiwa katika karne hii", amesema Bw. Dedesi na kuongeza kuwa ana wasiwasi "wajumbe wa Tume watabeba jukumu la kuikwamsha nchi katika janga kubwa".
Katika kuijadili mada ya Bw. Dedesi, Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Mangula aliishutumu CUF kwa kauli zake alizodai zinaashiria kuleta fujo.
Akijibu shutuma hiyo Bw. Dedesi alieleza kuwa chama chake ndicho kilichofanya kazi kubwa kudumisha amani Zanzibar.
Alisema, walitoa ushahidi kwa maandishi kwa taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa juu ya madai yao ya kudhulumiwa katika uchaguzi.
Aidha, alisema, walifanya kazi kubwa kuwatuliza wananchi walioona dhahiri kudhulumiwa.
Hata hivyo akasema, Rais Mkapa amekuwa akitoa kauli zinazoashiria kutotaka muafaka.
Amesema pamoja na kujaribu kuwasiliana naye, Mhe. Rais hakuwahi kujibu barua zao.
"Rais Mkapa alibainisha kwamba yeye ni CCM na kuwataka wapinzani "wamkome" kuwasialiana naye. Hivyo, CUF ikakazana kutafuta msaada nje ya Tanzania katika kupata ufumbuzi wa amani wa mgogoro huo", amesema.
Akichangia katika mkutano huo, Bw. Samson Mzingo alitoa wito kwa waandaaji wa mada kuweka katika mada zao matukio ya kihistoria ya nchi mbalimbali kama mifano na vigezo.
Alitoa mfano wa historia ya mapambano ya tawala mbalimbali kuanzia zile za wafalme za Waingereza toka mwaka 1215 hadi mapinduzi ya ufalme wa Ufaransa.
Alisema kwamba chanzo na sababu za uongozi mbaya ni kutokana na waliopo madarakani kupuuza katiba za nchi.
"Siasa ni uwanja wa fujo", alisema mzee huyo wa makamo na kufafanua kwamba katika siasa mtu yeyote anaweza kujitosa akashawishi akapata kura, kisha mkamkuta kisha kuwa Waziri Mkuu hata kama hana elimu.
Alisema, "hawa ndio wasiojua kufuata katiba ya nchi matokeo yake ni vurugu tupu". Hivyo aliwataka watoa mada wawe wakielezea matukio ya nchi mbalimbali kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe kama vile Kosovo na Bosnia ambako amedai chanzo ni viongozi kukiuka katiba.
Mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa Nkrumah,
umeandaliwa na Idara ya Sayansi, Siasa na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam. Washiriki wa mkutano huo ni wanasiasa kutoka vyama mbalimbali
na wanataaluma wa Chuo Kikuu.
Kukamatwa kwao kulifuatia ufunguzi wa matawi uliofanywa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Prof. Lipumba na Katibu Mkuu, Bw. Seif Sharif Hamad katika wilaya ya Ilala maeneo ya Gerezani, Msimbazi, Muhimbili na Upanga.
Viongozi waliokamatwa ni Mwenyekiti wa Jimbo, Bw. Hamisi Vuai (51), Twahiri Abbas Sheshe (45) Katibu wa Jimbo, Said Mbaraka (37) Mtendaji, Said Mohamed Ndevu Mjumbe.
Wengine ni Mwenyekiti wa Tawi la wazee, Mohammed Shemdoe, Katibu wa Tawi la wazee Idd Daffa. Walifikishwa mbele ya Hakimu wa wilaya Hashim Asajile.
Viongozi hao walisomewa mashitaka kwa wao kushindwa kutoa taarifa ya mkusanyiko wa watu kati ya saa sita na saa kumi jioni Juni 27, mwaka huu. Katika shitaka la pili ilidaiwa kwamba ni kufanya maandamano yasiyo halali kati ya saa nane hadi saa kumi jioni.
Washitakiwa wote walikana mashitaka, mahakama ilitoa dhamana kwa masharti ya kutofanya vurugu yoyote wakiwa nje ya dhamana.
Akiongea na mwandishi mara baada ya kupata dhamana, mmoja wa washitakiwa Bw. Hamisi Vuai alisema, wao wamekana shitaka kwa kuwa mashitaka si ya kweli.
"Tumekana mashitaka si ya kweli, sheria ya 1992 inaruhusu kufanya mkutano katika sehemu yetu ya tawi", alisema Bw. Hamisi.
Akielezea suala la kufikishwa polisi, Bw. Hamisi ambaye ni Mwenyekiti wa jimbo alisema kwanza walipekuliwa majumbani mwao.
"Walikuja askari 9 kunipekuwa kwa madai kutafuta nyaraka za siri za muungano ambazo walidai mimi ninazo baada ya hapo hakuna kilichopatikana", alidai Bw. Hamisi.
Naye Bw. Said Mbaraka alieleza kuwa alipekuliwa nyumbani kwake na askari zaidi ya watano. "Walikuja kunisachi (polisi) kwa madai kuwa sisi ni miongoni mwa watu tunaohusika na kesi ya uhaini Zanzibar", alisema Bw. Said.
Kesi hiyo yenye Na. 832/2000 imeahirishwa hadi Julai 13 mwaka huu na washitakiwa watano wako nje kwa dhamana.
Mapema wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) alifanya ufunguzi wa matawi kadhaa katikati ya jiji na kuhudhuriwa na maelfu ya wanachama wa chama hicho.
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |