MAONI YETU

Kifo hiki kichunguzwe

WALA msiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza (kuiua) isipokuwa kwa haki (Akahukumu Hakimu kuwa mtu huyo anastahiki kuuawa na akatoa amri ya kuuawa) (17:33).

Katika aya nyingine Qur'an inasema: ... Atakayemwua mtu bila yeye kuua mtu au bila kufanya fisadi katika nchi, basi ni kama amewaua watu wote. 5:32.

Taarifa za kutatanisha za kifo cha Alhaj Swedi Mchombe si za kupita bure bure bila ya kutolewa kauli.

Wakati taarifa za hospitali zinadai kuwa kafa kutokana na ugonjwa wa kifua kikuu na ukimwi, maiti yenyewe inaonesha kuwa na majeraha makubwa na kutapakaa damu.

Hali kama hii inahitaji uchunguzi wa kina. Je, Alhaj Swedi kafa kwa TB au ni kutokana na kupigwa?

Kama ni TB majeraha yametokana na nini? Na nani kamvunja shingo?

Je, ugonjwa wa TB unapelekea mtu kuvunjika shingo na kuwa na majeraha kichwani?

Kabla ya polisi kuamua mtu huyo azikwe na Manispaa, je, walitoa tangazo kuwaarifu ndugu wahusika kwanza?

Tunadhani yapo maswali mengi yanayohitaji majibu.

Ni matarajio yetu kwamba suala hili litashughulikiwa ipasavyo na vyombo stahiki ili kujua ukweli.

Aidha, tunaungana na Waislamu wa Moshi walioazimia kufuatilia kufunguliwa Inquest.

Kwa kufanyika hilo, utata uliopo hivi sasa huenda ukapatiwa ufumbuzi na haki kutolewa.

--
JuuRUDI


Bonyeza hapa
kushriki mjadala au kutoa maoni juu ya habari hizi na masuala mengineyo ya Kiislamu kwenye Baraza ya Wasomaji

   Kutoa maoni yako kuhusu ukarasa huu: Bonyeza hapa
Au
Andika barua  kwa: webmaster@islamtz.org


An-nuur Home | Ukurasa wa Mwanzo | Islam Tanzania
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook