IWAPO China itatokea kugawanyika kwa misingi ya kikabila na matabaka basi hilo litaanzia Xinjiang, jimbo la magharibi kabisa linalopakana na Afghanistan, Pakistan na Jamhuri tatu nyengine za iliyokuwa Urusi.
Sehemu mbili ya tano ya watu wake milioni 16 ni Waislamu wanaozungumza kituruki wanaojulikana kama Wallighur. Mapema ya 1944 wanamgambo wa kiislamu waliweza kwa muda kujitangazia jamhuri kwenye eneo la mashariki ya Turkestan, kusini magharibi mwa Xinjiang.
Wallighur wenye kupendelea kujitenga wamekuwa wakilaumiwa kwa machafuko, mauaji, magendo ya silaha na miripuko kadhaa tangu 1997. Wiki chache tu zilizopita ujumbe wa Serikali ya Xinjiang ulishambuliwa ulipokuwa Kyrgyzstan na watu wenye silaha waliotuhumiwa kuwa ni Walighur, ambapo afisa mmoja wa Serikali aliuawa.
Katika nchi, maisha Xinjiang yanaonekana kuwa ni ya kawaida. Kwenye Soko la kale la Kashgar wachuuzi wanatembeza kila kitu. Bango kubwa lenye maneno ya kiongozi wa zamani wa China, hayati Deng Xiaoping linasema sera za chama cha Kikomunist hazitayumba kwa miaka mia ijayo.
Katika mwaka 1997, maandamano ya kupinga Wachina yaliripuka kwenye mji wa Yining, yakiwaaacha watu tisa maiti na wengine zaidi ya 200 wakiwa majeruhi. Hilo na matukio mengine ndio yaliyochochea serikali kufanya misako ya mara kwa mara.
Karibuni hivi mwezi uliopita Wallighur watano waliuliwa huko Urumqi, mji mkuu wa Xinjiang kwa madai ya kutaka kuligawa taifa, wizi na mauaji.
Maelfu ya Waislamu wamewekwa kizuizini, zaidi ya mia mbili kunyongwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Afisa mmoja wa China anasema "wanaotaka kujitenga, magaidi wa kimataifa na wenye misimamo mikali ya kidini wamekuwa wakiongezeka mno katika Asia ya kati".
Kwa sasa Waislamu wenye silaha ndani ya Xinjiang ni wachache na hukimbia kutoka hapa na pale.
Xinjiang ni muhimu kwa sera za Rais Jiang Zemim katika kuipa uhai China ya magharibi kiuchumi, kwani ina utajiri mkubwa wa mafuta, madini na pamba. Jiang anafikiria kurudisha njia asilia ya Silkroad ambayo itakata katikati ya Xinjiang kuelekea Iran. Moja ya miradi inayofikiriwa ni mradi wa dola za kimarekani zipatazo bilioni 14, ni bomba la gesi litakaloiunganisha Xinjiang na bandari ya Shangh'ai umbali wa kilometa 4200.
Mji wa Kashgar una bustani yenye sanamu kubwa kuliko yote ya Mao Zedong. Wakazi wa Kashgar wanasema mamlaka husika ina mpango wa kuzivunja nyumba za jadi karibu na msikiti wa Idi Kah ambao ndio mkubwa zaidi kuliko yote kwa China ili kujenga zaidi mtindo wa Tianamen.
Wenyeji Waislamu wanalalamika kuwa wachina wanazidi kuzichukua nafasi chache za kazi zilizopo na kuharibu utamaduni wao.
Mnamo mwezi machi serikali ya China ilimhukumu kifungo cha miaka minane, mfanyabiashara milionea bibi Rabiya Kadeer, ambaye pamoja na mumewe wamekuwa wakiendesha biashara kubwa ya nguo kwa madai ya kutoa siri za nchi kwa wageni.
Mume wake bwana Sidiq Rauz alipata kutumikia kifungo cha kisiasa kati ya 1969 na 1978. Mwaka 1996 alitafuta hifadhi nchini Marekani.
Anasema mkwe amefungwa kwa sababu tu alimtumia magazeti. Serikali ya China ina wasi wasi kuwa Waislamu wa Xinjiang wanaweza wakaungana kwa nguvu zao na wapiganaji jihadi wengine mfano wachechnya ambao wamekuwa wakizipinga tawala za nchi za Asia ya kati.
Mwaka uliopita maafisa Usalama wa Kirusi waliwakamata Walighur kadhaa ndani ya Chechnya. Hata hivyo upelelezi zaidi ulionesha hawakuwa ni magaidi, bali wapishi tu wakillghur.
Imefasiriwa kutoka jarida la NEWS WEEK
makala iliyoandikwa na Malinda Liu.
Moja ya fani kuu za ushushushu wa iliyokuwa KGB ilikuwa ufuatiliaji wa karibu (surveillance) wa watu binafsi, makundi, viongozi wa jumuiya mbali mbali na zaidi wale waliokuwa na uwezo wa kushawishi, wageni toka nje, maafisa wa idara mbali mbali za serikali na kujasusiana wenyewe kwa wenyewe ndani ya KGB.
Maafisa wote wa KGB walilazimika kupata mafunzo ya msingi ya taaluma hii, hata hivyo kiufanisi zaidi iliundwa kurugenzi maalum iliyoratibu ushushushu huu pekee .
Kururgenzi hii ilihusika na usimamizi, uchambuzi na ufundi ulioendeshwa kwa siri kiasi kwamba hata maafisa wake hawakuwa wakifahamika kwa urahisi.
KGB ilikuwa na zaidi ya maafisa 3,500 waliokuwa chini ya kurugenzi ya surveillance wanawake kwa wanaume ambao kazi yao ilikuwa kufuatilia watu tu maeneo mbali mbali ya nchi.
Kurugenzi hiyo iligawanywa katika idara 12 kila moja ikihusika na watu wa eneo maalum.
Idara ya kwanza iliwafuatilia raia wa Marekani walioishi nchini humo. Idara ya pili iliwafuatilia raia waliotoka nchi za jumuiya za madola waliokuwa wakifanya kazi nchini humo, miongoni mwao ni waandishi wa habari, wanafunzi waliokuwa wakisoma vyuo mbali mbali na wafanyabiashara.
Idara ya tatu na ya nne zilishirikiana kufanya "surveillance" dhidi ya watu wote waliokuwa si waamerika.
Idara ya tano ilifuatilia ulinzi uliowekwa katika balozi mbali za nje ziliko nchini humo, "survaillance" ililenga kuzuia ufikaji wa mara kwa mara wa Warusi katika balozi hizo.
Idara ya sita ilihusika na kuwachungua raia wa nchi hiyo waliotakiwa kuajiriwa na KGB. Zaidi ilikuwa kupata historia, nasaba na mahusiano yao na watu wengine.
Idara ya saba ilikuwa ikihusika na ukarabati wa zana za shughuli hiyo ya ufuatiliaji. Zana hizi zilikuwa ni pamoja na transmitter zilizopachikwa kwenye magari, viatu na maofisini; surveillance camera za picha maalum na za TV kwa ajili ya utambuzi (identification), tape rekoda nakadhalika.
Idara ya tisa ilikuwa ikifanya doria mitaa na barabara ambazo zilitumiwa na viongozi au wajumbe wa chama kilichotawala kuelekea na kutoka maofisini.
Idara ya 10 ambayo ndiyo iliyokuwa kubwa katika idara kuliko zote iliweka maafisa wake maeneo maalum yaliyokuwa yakitembelewa na wageni au watu mashuhuri. Maeneo hayo ni pamoja na hifadhi za wanyama, makumbusho, majumba ya senema, stoo, vilabu vya usiku, viwanja vya michezo, viwanja vya ndege na vituo vya mabasi na magari moshi.
Idara hii ilikuwa na watumishi zaidi ya 400, waajiriwa(staff officers) na wasio waajiriwa(part time spies) wengi wao wakiwa maafisa wastaafu wa KGB. Vile vile ilikuwa ikiendesha "mradi" wa ukodishaji wa Taxi kwa ajili ya kufuatilia nyendo za abiria wa kawaida na watalii. Ilikuwa na miradi ya kusafisha viatu(Shoe shiners), hoteli, baa, bendi za muziki nakadhalika.
Kwa upande mwingine idara ya 10 ilikuwa na maajenti katika mahoteli walioshughulika na uchukuaji wa picha au "photocopy" za nyaraka au vielelezo kutoka kwa wageni iliyowashuku.
Idara ya 11 ilihusika kubuni na kutengeneza nyuso na maumbo bandia, nguo maalum za kujibadilisha, nywele na sharubu bandia kwa ajili ya maofisa walioajiriwa kwa kazi hiyo ya Survaillance.
Idara ya 12 ilikuwa ya wataalamu waliowajibika katika operesheni nyeti ambazo ni pamoja na kuwafuatilia wageni waheshimiwa au viongozi wa juu wa chama na serikali(vingunge).
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |