MWENYEKITI wa UDP Bw. John amekataa kuungana na CUF na CHADEMA kwa hoja kuwa vyama hivi vina muelekeo wa udini (yaani Uislamu). Kwa hiyo, kila chama cha upinzani kitasimamisha mgombea wake isipokuwa CUF na CHADEMA.
Mnamo mwezi Mei mwaka 2000 kulifanyika uchaguzi wa viongozi katika serikali ya Wanafunzi katika chuo cha IDM-Mzumbe. Nafasi zilizogombaniwa zilikuwa ni mbili, nafasi ya Rais wa serikali ya wanafunzi na makamu wake.
Kwa utaratibu uliopo pale chuoni kila mwanachuo anayetaka kugombea nafasi hizo basi hulazimika kuchukua fomu, kujaza na kisha kuirudisha kwa kamati ya uchaguzi (electorial commettee).
Kamati hii huchuja majina ya wagombea na kubakia wagombea wasiozidi watatu kwa nafasi ya Rais na pia kwa nafasi ya makamo.
Baada ya mchujo wa kamati ya uchaguzi kupita, yalibaki majina matatu kwa nafasi ya Rais. Wagombea hao ni Abdul Uzairu - mwanafunzi wa mwaka wa pili katika kozi ya Public Administration, mwingine ni Godwin Munyeri kutoka kozi hiyo hiyo mwaka huo huo na Bw. Cosmas Kennedy - mwanafunzi wa mwaka wa pili katika kozi ya Certified Accoutancy.
Kabla ya majina kuchujwa na kubakia matatu, wagombea wawili kutoka katika kozi ya Public Administration walikubaliana kwamba endapo majina yao yote mawili yatarudi, basi Bw. Godwin Munyeri aachie ngazi ili wasije kuzigawa kura, na hatimaye kumpa nafasi mpinzani wao Bw. Kennedy Cosmas.
Ndipo baadhi ya wakereketwa wa mfumo Kristo wakamuendea Bw. Godwin Munyeri na kumwambia asikubali kumuachia Muislamu kuwa mgombea pekee kutoka kozi yetu.
Wakiwemo wagombea wawili, Muislamu anaweza kushinda. Jazba na ushabiki wa kidini ukamuingia Bw. Godwin Munyeri na hatimaye kukaidi yale makubaliano yake na Bwana Uzairu Abdul. Ilifikia hatua Bw. Munyeri jinsi alivyokosa haya alimuendea Bw. Abdul Uzairu na kumwambia aachie ngazi kwa ahadi kuwa atampa uwaziri pindi akichaguliwa kuwa Rais wa serikali ya wanafunzi ijulikanayo kwa jina la (MIDMSO Government). Uzairi Abdul alimjibu Bw. Munyeri kwa kumwambia: Umesahau makubaliano yetu, kwa nini unichagulie nafasi? Mimi sitaachia ngazi mpaka tone la mwisho la damu yangu".
Baada ya maneno haya, Bw. Godwin akaendelea na jazba zake alizojazwa na wapenda mfumo Kristo wenzie. Kampeni za uchaguzi zikaanza, kila mgombea kati ya wale watatu alifanya kampeni kadri ya uwezo wake.
Kama kawaida yao, fitna za udini zikaanza kusambazwa dhidi ya Abdul Uzairu. Eti yeye ni Mujahidina, na akiwa Rais ataongeza idadi ya Waislamu chuoni, yeye ndiye Sheikh Mbukuzi wa Mzumbe na kadhalika.
Uchaguzi ukafanyika kwa idadi ile ile ya wagombea watatu katika nafasi ya Urais. Matokeo ya uchaguzi ni kuwa Bw. Kennedy Cosmas aliibuka kuwa Rais wa Serikali ya wanafunzi kwa kuwashinda Bw. Abdul na Godwin kwani Bw. Godwin alikataa kutekeleza makubaliano na hatimaye kura ziligawika.
Kwa hiyo, Cheyo na Mrema kamwe hawawezi kuungana na CUF. Na kama ni muungano basi asimamishwe Mrema au Cheyo kugombea Urais na Lipumba ahaidiwe nafasi ya uwaziri. Funzo tunalolipata hapa ni kuwa Mkristo hatakubali hata siku moja awe chini ya Muislamu.
Na yale yote ya IDM Mzumbe afadhali ashinde Kennedy Mkristo mwenzetu kuliko kushinda Bw. Abdul - Muislamu. Iko siku, Waislamu wote wa Tanzania watakuja gundua mbinu yenu hii. Na hiyo itakuwa hatari kubwa.
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |