Mzuka wa kikoloni
SEMINA iliyokuwa inajadili utekelezaji sheria za Kiislamu Afrika, ilimalizika juzi jijini.
Ujumbe wa Kenya katika semina hiyo uliongozwa na Kadhi wa Nairobi wakati wa Uganda ulikuwa na Waislamu wasomi walio katika harakati za Kiislamu.
Tanzania kwa upande wake iliwakilishwa na Robert V. Makaramba, Mhadhiri katika kitivo cha sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Yeye ni katika wanafunzi wawili waliokuwa wamepelekwa Uingereza kusomea sheria ya Kiislamu katika kiwango cha 'Masters' miaka ya nyuma.
Mwingine alikuwa Jaji Augustino S.L. Ramadhani, Jaji katika Mahakama ya Rufaa Tanzania.
Bw. Robert katika utangulizi wa mada yake "The Secular State and The State of Islamic Law in Tanzania" ameiita sheria ya Kiislamu ya Ndoa na Mirathi kuwa Mzuka wa Kikoloni (Colonial Ghost).
Katika kuelezea 'Mzuka' wake huo, Bw. Robert amejaribu kujenga hoja kuwa mahari ni sawa na bei ya kununua mke.
Akasema kwa kinywa kipana huku akinukuu rejea kuwa mahari katika Uislamu hulipwa katika mikupuo miwili. Wackwanza hulipwa wakati wa kufunga ndoa na sehemu iliyosalia hulipwa ndoa inapovunjika.
Yapo mengi aliyoyasema Bw. Robert ikiwa ni zao la waalimu wake na rejea zao za kistashrikina (orientalism).
Lakini tutosheke tu kwanza na hayo.
Ni wazi kwamba iwapo mtizamo wa mwalimu juu ya sheria ya Kiislamu ni huo, haitarajiwi wanafunzi wake wasalimike na muelekeo huo. Na hao miongoni mwao ndio huwa mahakimu, wanasheria wa serikali na majaji.
Kwa hakimu ambaye mtizamo wake ni kuwa sheria ya Kiislamu ni mzuka wa kikoloni, haki gani anatarajia Muislamu aipate.
Mtizamo kama huu ndio hupelekea mgogoro kama ule wa mirathi ya Hajat Aziza bint Omar ambapo mali ya Muislamu hupewa asiye Muislamu arithi.
Au wakati mwingine kwa tamaa ya mali mtu huleta wosia batili (ulio kinyume na sheria ya Kiislamu) na "akina Robert' kwa chuki zao tu wakaukubali ili tu waukomoe mzuka wao.
Lakini pengine suala muhimu ni je, Waislamu tatizo hili wanaliona? Hatua zipi wanachukua.
Kama alivyosema Jaji Augustino, haki ni lazima ionekane kutendeka.
Hatuoni ni vipi Muislamu atahisi anatendewa
haki katika mazingira haya ya dini yake kuonekana mzuka wa kikoloni?
--
![]()
|
Links | Matoleo Yaliyopita | Sign our Guestbook |